Makamu wa Rais azuia meli yenye hitilafu isiondoke Zanzibar.


Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Messages
10,945
Likes
232
Points
160
Ndibalema

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2008
10,945 232 160
Makamu wa pili wa rais, Balozi Ally Seif, jana usiku alilazimika kuizuia meli ya MV Serengeti ambayo hufanya safari zake Unguja na Pemba, kuendelea na safari yake ikitokea Unguja kuelekea Pembaimeelezwa sababu ya kuizuia meli hiyo ni itilafu iliyojitokeza kwenye injini.
Hata hivyo mara baada ya abiria kugundua hitilafu hiyo walitaka kushuka lakini wahusika wa meli hiyo waliwazuia wasishuke.
Haikujulikana mara moja mheshmiwa makamo wa rais alizipataje taarifa za tukio hilo lakini bila kutarajia mheshmiwa huyo alitoa amri kali ya kuizuia meli hiyo isitoe nanga mpaka itengenezwe, kitu ambacho kilifanyika.
Meli hiyo iliendelea na safari kesho yake baada ya matengenezo.

Source: Radio one Habari.

My take:
Mpaka amri inatolewa na mheshmiwa makamu wa Rais, inamaanisha nini?
Vyombo husika havina 'meno'?
 

Forum statistics

Threads 1,237,521
Members 475,533
Posts 29,291,783