Makamu wa Rais atoa siku 30 Sera Mpya ya Kilimo kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,120
7,701
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Mpango ameiagiza wizra ya Mazingira kutafasiri Sera Mpya ya Mazingira 2021 pamoja na mpango mkakati kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili ndani ya siku 30.

ameyasema hayo alipo kuwa anazindua Sera hiyo mpya ya mazingira Jijini Dodoma ambapo Sera hiyo pamoja na Mpngo mkakati zote zilikuwa zimeandikwa kwa Lugha ya kiingereza.

Heko kwake Mh. Makamu wa Rais kwa kuipa heshima lugha ya Kiswahi ambayo ndio tunu na urithi wa watanzania.

Tuwaelimishe watanzania kwa Lugha yao ya kiswahili.....tuache kujikomba na lugha za kiingereza, sina maana kiingereza kupuuzwe la hasha! bali ni muhimu mambo yetu tukayaendesha kwa lugha yetu ya Kiswahili, huduma za kijamii zitolewe kwa kiswahili n.k.

Kama SDAC wameamua kutafasiri sheria zao pamoja na mikataba yao mbalimbali kwa lugha ya kiswahili sasa iweje sisi mambo yanayo wahusu watanzania yaandikwe kwa lugha ya kizungu?
Chanzo Chanel ten Habari 12/2/2022
 
Hao wakalimani sasa
Acha tuingizwe chaka
Tunasubiri itakavyoandikwa hapahapa baada ya mwezi
 
Naona Makamu pamoja na PM wamedhamiria haswa kiswahili kitumike kikamilifu ktk shughuli mbalimbali za kijamii, ila tatizo lipo kwa watendaji wetu bado wanasuasua, sielewi kwa nn haswa na kwa malengo gani haswa!
mbali na agizo la waziri Mku lkn bado utekelezaji wa matumizi ya Lugha ya Kiswahili unasuasua.




 
Back
Top Bottom