Makamu wa Rais amtetea Rais Kikwete kwa kupambana na ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamu wa Rais amtetea Rais Kikwete kwa kupambana na ufisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 17, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  Posted Date::4/17/2008
  Makamu wa Rais amtetea Rais Kikwete kwa kupambana na ufisadi
  Na Mwandishi Wetu
  Mwananchi

  MAKAMU wa Rais, Dk Ali Mohammed Shein, amesema hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali hivi sasa katika kushughulikia masuala ya ufisadi, ni kielelezo thabiti cha utekelezaji wa dhamira ya kweli ya Rais Jakaya Kikwete na serikali yake kupambana na rushwa.

  Kile ambacho kinaendelea hivi sasa katika kukabiliana na ufisadi nchini, kinakwenda sambasamba na dhamira ya kweli ya Rais na serikali katika vita dhidi ya rushwa, alisema Dk Shein.

  Alisemaa Rais Kikwete aliahidi katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge kuwa mapambano dhidi ya rushwa yataimarishwa na hicho ndicho kinachoedelea.

  Dk Shein alisema hayo jana asubuhi alipozungumza na Waziri Mkuu wa Denmark, Anders Fogh Rasmussen kabla ya kuanza kikao cha kwanza cha Tume ya Afrika iliyoundwa na serikali ya Denmark.

  Alisema vita dhidi ya ufisadi, ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuimarisha utawala bora unaozingatia sheria.

  Hatua ya Rais kuunda Tume ya kushughulikia urejeshaji wa fedha za EPA na Waziri Mkuu kuunda Kamati ya kushughulikia mapendekezo ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu suala la Richmond sio tu inadhihirisha umakini wa serikali kupambana na ufisadi, lakini pia inatoa ujumbe kwa wahusika kuwa hakuna atakayekwepa mkondo wa sheria, alisisitiza.

  Kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Tume ya Afrika, Makamu wa Rais alimwambia Rasmussen kuwa Tanzania inaunga mkono kazi ya Tume na itayapa kipaumbele majukumu ya Tume ili iweze kufikia malengo yake.

  Aliishukuru serikali ya Denmark kwa misaada yake ya kimaendeleo ambayo nchi hiyo imekuwa ikiitoa kwa Tanzania na kuchangia katika mafanikio ambayo Tanzania imeyapata hivi sasa.

  Dk Shein alitumia fursa hiyo kumueleza Waziri Mkuu wa Denmark kwa kifupi hali ya uchumi na kisiasa ilivyo hivi sasa nchini ambapo alisema uchumi unafanya vizuri huku hali ya kisiasa ikiwa ni shwari.

  Wakati huo huo, Rasmussen alisema serikali yake imezipokea hatua za awali zinazochukuliwa na serikali katika kushughulikia sakata la fedha za EPA na zabuni ya ununuzi wa mitambo ya kufua umeme wa dharura ya Richmond.

  "Mchango wa vyombo vya kidemokrasia kama vile Bunge na vyombo vya habari katika vita dhidi ya rushwa ni wa kupongezwa na hii ni ishara ya kuimarika kwa taasisi za kidemokrasia nchini Tanzania, alifafanua.
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Shein naye ni fisadi by proxy, Kikwete is worse than Zaphod Beeblebrox wa HHGttG!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,171
  Trophy Points: 280
  Hata aibu hawana kusema uwongo!
   
 4. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Jamani hivi ile tume ya raisi ya swala la EPA nani ana Hadidu za rejea maana inawezekana tunawalaumu wanakamati hawajafanya kazi kumbe hadidu za rejea hazijawawezesha kukamata mafisadi, katika ndo tunaweza kuamua kama kikwete yuoko serious au la!
   
Loading...