Makamu wa Rais aagiza kumbukumbu zote za Serikali ziandikwe kwa lugha ya Kiswahili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,406
2,000
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisha huduma na kumbukumbu zote muhimu za nchi zinatolewa kwa lugha ya Kiswahili na akahimiza haja ya mamlaka kuja na Sera ya Kiswahili.

Aidha, Rais John Magufuli leo anatunukiwa tuzo maalumu ya Shaaban Robert kutokana na mchango wake katika kukuza lugha ya Kishwahili.

Akifungua maadhimisho ya Siku ya Kiswahii jijini Dodoma jana, Samia alizitaka Wizara za Habari Tanzania Bara na Zanzibar zikae na wataalamu kubaini maeneo na nyaraka za kiserikali ambako bado Kiswahili hakitumiki.

“Nataka mbaini ni maeneo gani na nyaraka zipi za kiserikali bado hazitumii Kiswahili na mueleze ni hatua gani zinaenda kuchukuliwa ili kufikia hatua ambapo huduma na kumbukumbu zote muhimu za nchi zinatolewa kwa lugha adhimu ya Kiswahili.”alisema na kuongeza; “Nampongeza mheshimiwa Mwigulu Nchemba (Waziri wa Sheria na Katiba) kwa kuanza kuchukua hatua ya kuhakikisha hukumu za mahakama zinatolewa kwa Kiswahili ili kuhakikisha wananchi wanyonge wanapata haki zao, matumaini yangu wizara zingine zitajiongeza kuhakikisha wanatumia Kiswahii kwenye kazi zote zinazohusu wananchi.

Alisema kwa sasa Kiswahili ni bidhaa inayopiganiwa duniani kote, hivyo amezitaka wizara zote mbili na kupitia mabaraza ya kiswahili kwa kushirikiana na wadau wengine kuja na mikakati ya kukitangaza, kukifundisha na kukiendeleza Kiswahii nje ya Tanzania ikiwa kuwa na orodha ya vyuo vikuu vyote duniani ambako Kiswahili kinafundishwa ili kuweza kutoa ushuari wa kitaalamu.

Mwenyekiti wa Bodi ya BAKITA, Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Taifa la Kiswahili (BAKITA), Dk Method Samwel alisema katika madhimisho ya mwaka huu, Tuzo ya Shaaban Robert itatolewa kwa Rais Magufuli na pia kutatolewa tuzo za matumizi sanifu na fasaha ya lugha ya kiswahili na wanafunzi waliofanya vizuri kweye mitihani kwenye somo la Kiswahili.
 

DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
794
1,000
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amesema mkakati wa serikali ni kuhakikisha huduma na kumbukumbu zote muhimu za nchi zinatolewa kwa lugha ya Kiswahili na akahimiza haja ya mamlaka kuja na Sera ya Kiswahili....
Ni bidhaa inayopiganiwa duniani kote? Kweli? Tusijipe moyo tu. Vijana wengi Tz wanashindwa kujiajiri hata in tourism na wengine wanatoa huduma mbovu sababu ya kutofahamu English proficiently. Nchi ambayo ina vivutio vya utalii vingi sana ilitakiwa iwekeze kwenye international languages pia. Lakini sisi tunakazia tu swahili yetu. Haya bhana
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,494
2,000
Ni bidhaa inayopiganiwa duniani kote? Kweli? Tusijipe moyo tu. Vijana wengi Tz wanashindwa kujiajiri hata in tourism na wengine wanatoa huduma mbovu sababu ya kutofahamu English proficiently. Nchi ambayo ina vivutio vya utalii vingi sana ilitakiwa iwekeze kwenye international languages pia. Lakini sisi tunakazia tu swahili yetu. Haya bhana
Ndio mkakati huo sasa wa kuboresha Kiswahili maana vijana wenzetu wanapiga Kimalkia tuuu ilhali watalii wanataka full exposure ya kufahamu lugha yetu. ^Mofimu^ unaijua wewe!?
 

DocJayGroup

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
794
1,000
Ndio mkakati huo sasa wa kuboresha Kiswahili maana vijana wenzetu wanapiga Kimalkia tuuu ilhali watalii wanataka full exposure ya kufahamu lugha yetu. ^Mofimu^ unaijua wewe!?
Watalii wanataka TOP CUSTOMER SERVICE (Huduma ya wateja ya hali ya juu). Exposure kwa kiswahili ipo nchi nzima, haina haja ya kuufanyia kazi. Kitu cha kufanyia kazi ni kuboresha huduma kwa watalii kwa kuboresha ufahamu wa lugha za kigeni nchini sababu mawasiliano mabovu siku zote yanaathiri huduma kwa wateja. Hio ndio sababu kubwa iliyotolewa na watalii waliokuja Tz inayowafanya wasitake kurudi tena kufanya utalii Tz. Halafu nchi inaongozwa na watu wasiotaka hata kutembelea nchi za magharibi kufahamu watalii wana mahitaji gani. Ila wanataka tu hela ya utalii.

 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom