Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar: Naombeni mkafanye kazi kwa kuwatumikia Watanzania

Ojuolegbha

Member
Sep 6, 2020
22
75
“NAWAOMBENI MUKAFANYE KAZI KWA KUWATUMIA WATANZANIA” MHE. HEMED

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abulla amewataka Mabalozi walioteuliwa karibuni kuendana na kasi ya viongozi wakuu wa Serikali wakati wakiwakilisha Tanzania katika nchi zao walizopangiwa.

Mhe.Hemed alieleza hayo alipofanya mazungumzo na mabalozi hao walipofika Ofisini kwake Vuga Jijini Zanzibar kwa lengo la kuagana nae.

Alisema Imani ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyonayo kwa Mabalozi hao ni ishara kuwa na wana uwezo na vigezo vizuri vya kuiwakilisha Tanzania katika maneo yao ya kazi waliopangiwa.

Makamu wa Pili wa Rais Aliwataka balozi hao kutumia fursa hiyo kwa kujenga ushawishi na kuvutia wawekezaji tofauti na ili waje kuekeza nchini Tanzania kutokana na vivutio mbali mbali vilivyopo.

Aliwaasa kuzingatia miongozo waliyopewa na viongozi wakuu hasa maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwaapisha.

Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi wenzake, Balozi Grace Afraid Olotu Balozi wa Tanzania nchini Sweden alisema miongoni mwa maeneo watakayokwenda kuyasisimia ni kukuza hadhi ya bidhaa zinazozalishwa nchini Tanzania ili ziweze kukubalika katika soko la kimataifa hasa nchi za Umoja wa Ulaya.

Balozi Grace alieleza kuwa watatua dhamana zao walizokabidhiwa katika kuhakikisha wanajenga Diplomasia ya Uchumi kwa lengo la kukuza uchumi wa Tanzania.

Mabalozi waliofika Kumuaga Makamu wa Pili wa Rais ni pamoja na Balozi wa anaewakilisha Tanzania nchini Sweden, Balozi wa anaewakilisha Tanzania nchini Marekani, Balozi wa anaewakilisha Tanzania nchini Italia, Balozi wa anaewakilisha Tanzania nchini Geneva pamoja na Balozi wa anaewakilisha Tanzania nchini Rwanda.

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Septemba 21, 2021.
IMG-20210921-WA0027.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom