Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar: Mrithi wa Maalimu Seif Zanzibar na mwanachama mtarajiwa wa CHADEMA

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Alifukuzwa nafasi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar akiwa Bunge la Katiba Mjini Dodoma kutokana msimamo wake juu ya aina ya Katiba mpya itakayofaa Wazanzibar. Alilazimishwa kusema asiyoyaamini akaapa Kwa Mwenyenzi atotenda kinyume na Imani yake akasaliti wito aliopewa na Mwenyenzi MUNGU katika kuwatumikia Watanzania. Akarudi shamba kulimu huku CV yake ikibaki bila madoa na Wala utu wake haukupopolewa na watu wanaoamini Kwamba wote tumeletwa Duniani kuwaabudu WANADAMU.

Ni mwanazuoni na Mwanasiasa ambaye ajawahi kufeli katika Uongozi, pote alipopita amekuwa akifanya Jambo na linabaki kwenye historia. Haya siyo maneno yangu Bali ndivyo historia yake Kati Uongozi inavyosema. Moja lililowazi ni uwekaji misingi imara katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu Zanzibar.

Anatamka leo hii kwamba Kwa muda walioingia mkataba na ccm katika serikali ya kitaifa hakuna kilichofanyika; hii ni kauli yake kubwa ya pili baada ya awali kutishia kung'atuka pale CCM ilipokidhulumu chama chake Kiti Cha Ubunge Jambo lililopelekea uchaguzi kurejewa na ACT wakashinda. Anavyosema ndivyo anavyoamini na msimamo wake hauwezi kuzuiwa na magari na ving'ora vinavyomsafishia njia; Kwake yeye Taifa kwanza na anaweza Kuishi bila kuwa Makamu wa Rais na asipungukiwe kitu.

Huyu ndiye mfuasi wa nyayo za Maalimu Seif; huyu ndiye dira ya mabadiliko ya Katiba Zanzibar na ndiye kiongozi wa kweli ambaye madaraka Kwake nikutoka Kwa MUNGU siyo wanadamu.

Kiongozi mwenye sifa hizi anapaswa kusimama Kwa chama Gani kuyafikia malengo? Ndani ya CCM atoweza kusema kweli Daima labda ingekuwa TANU; ndani ya ACT hakuna vision Kwa sababu misingi ya chama imejengwa kwenye kusaka madaraka kuliko kusaka matumaini mapya ya Tanzania.

Nadhani ataenda Chadema, naamini ataenda CHADEMa, naziona dalili za kwenda CHADEMA.......huyu kiongozi sidhani kama anaamini kile Babu Duni na Zito wanachokiendea. Anaamini Nchi inahitaji Katiba mpya.
 
ACT inaenda kuvunjika kutokana na tamaa ya madaraka na kutumika ule uchaguzi wa mwenyekiti wa chama umeleta mpasuko mkubwa Hamad masoud kajitoa na anaangalia upepo aende wapi km lipumba atazichanga karata zake vizuri CUF itafufuka zanzibar na ndo kaburi la ACT huku zito akiwa bize kupewa maelekezo_Othman masoud hawaendani kimtazamo na zitto kumbuka Hawa wote walikuwa wafuasi wa Maalim seif na sio ACT ht maalim angeenda CHAUMA nao wangeenda chauma
 
ACT inaenda kuvunjika kutokana na tamaa ya madaraka na kutumika ule uchaguzi wa mwenyekiti wa chama umeleta mpasuko mkubwa Hamad masoud kajitoa na anaangalia upepo aende wapi km lipumba atazichanga karata zake vizuri CUF itafufuka zanzibar na ndo kaburi la ACT huku zito akiwa bize kupewa maelekezo_Othman masoud hawaendani kimtazamo na zitto kumbuka Hawa wote walikuwa wafuasi wa Maalim seif na sio ACT ht maalim angeenda CHAUMA nao wangeenda chauma
Lipumba angejiweka pembeni cuf I'll damu mpya iingie. Wengineo wafuasi was maalim wanapenda kurud cuf. Ila hawamuamini lipumba. Malengo ya act ya zitto yapo tofauti na wapemba wengi.
 
Anavyosema ndivyo anavyoamini na msimamo wake hauwezi kuzuiwa na magari na ving'ora vinavyomsafishia njia; Kwake yeye Taifa kwanza na anaweza Kuishi bila kuwa Makamu wa Rais na asipungukiwe kitu.
Huyu ndiye kiongozi Sasa. Hayumbi Wala kuyumbishwa. Namkubali sana huyu.
 
Wanzazibari priority katiba mpya na kipengele cha serikali tatu. Tume huru agenda ya mfukoni .
 
Back
Top Bottom