Kichwa Kichafu
JF-Expert Member
- Apr 13, 2017
- 44,565
- 188,768
Apumzike kwa amani.
Oooooooh kumekucha sasa lol.Saiz kuna maswali ya yupo wap waziri Mpango, mama salma kikwete, Kabudi na mkuchika?
MKUU tuendelee kuchukua tahadhari
Oooooooh kumekucha sasa lol.
Ila nimecheka😁Tuko kwenye msiba unatuletea masuala ya ununuaji wa sarafu? Wee vip wee jamaa..alaaah
Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Mkuu siasa kitu kibaya sana hata lisu na yeye angekubali kutibiwa Tanzania na yeye angekuwa tushamsahau walivyoona zanzibar mechi ngumu ikapelekwa taifa mechi maana marefa wao mungu awalaani wote waliohusika kwenye zoezi hili.Hata Kama hatuipendi serikali lakini tusiisingizie kwa Jambo lisilo na uhakika naamini pamoja na changamoto za JPM hawezi kufanya huu upuuzi maana uwepo wa seif kwenye serikali ya umoja wa kitaifa ulikuwa unampa sifa yeye JPM na serikali yake. Kwa hili namtetea Magufuli.
huku pia ni muhimu kujua mustakabali wa maisha yetu.Bora tungeendelea kusikia zile skendo za akina paula huku kwa TANZIA hakufai kabisa
Sio tetesi ndo ukweli wenyewe huu.Unaweza kuta stone amejipiga chanjo kimya kimya hana maana yule mwamba
Nimewahi kufika huko.Barabara zao ni za nyoka sana na nyembamba kupita kiasi.Wangejua mwaka wa kufa Seif basi wangezitengeneza kidogo.ishu si usafiri wa meli, changamoto ninayoiona mimi ni usafiri wa barabarani utakuwa wa tabu sanaaa na vurugu huko Pemba.
Wameshasema haifai huku kwetu ya nini tena.Hata hizo nyengine baada ya mwaka zitakuwa hazina maana tena kwani wanasema hicho kiddudu kinabadili sura kila siku.Bora tuchukue msimamo wetu huu huu na Mungu atatulinda.ninahisi huenda pasiwe na gari kabisa na watu wakausindikiza kwa miguu kutoka Airport mpaka Gombani kusaliwa na kutoka hapo mpaka kijijini kwake. Huu Mkusanyika utakuwa mkubwa kupita maelekezo na watu hawatakuwa na tahadhari yoyote. Na tunajua kuwa kuna watu wanabeba hivi virusi, kwenye umma huo watakuja kuumwa wengi mno ambao wengi wao watakuwa wazee na kuanza kuona idadi ya vifo ikikuwa kwa kasi ya ajabu sana. Kutokana na udogo wa visiwa hivi na watu kuwa karibu karibu bila tahadhari, haitoshangaza ikawa 80% ya wazanzibari wakajikuta wanaumwa na hii kitu.
Zanzibar ina Wizara yake ya Afya, wangefanya mazungumzo na S.A wakatupatia tu hio chanjo ilofeli kwao.
Msiba mzito huu mpaka umenitoa chimbo.Leo kweli kumefiwa.... mzee wa nalog off nimekuona.!!! Haya tuwe pole. Tunashkuru kwa kila hali
Kwa hyo unataka kusema wamemuua na s ugonjwa?Kwanza nashangaa nani aliyemshawishi atangaze ana corona.Na baadae raisi wa Zanzibar alipoulizwa akasema hawezi kutaja ugonjwa anaougua makamo wake.Halafu ni familia nzima kiasi kwamba ni rahisi kuelezwa wakati wa kifo chake hakukuwa na ndugu yoyote wa karibu kutokana na karantini.
Natamani nisikie maalim Seif kafufuka kabla kuzikwa leo jioni ili atupe mkanda wote wa kifo chake. Maeelezo yake baada ya kufufuka yanaweza kuwa kama hivi " Loo ! washenzi sana hawa. ...Niwaambia mimi niacheni hapa hapa nyumbani sina haja kwenda hospitali kwani sina tatizo la kupumua na hata homa ilishaacha. .Wakanibeba juu juu mpaka Mnazi mmoja na mimi na madaktari wangu tukakataa kuwekewa oksijen. Ikaendelea hivyo mpaka tarehe 9 waliponipandisha kwenye ndege usiku bila kufuatanishwa na ndugu yoyote mpaka Darisalama . Tangu siku hiyo ikawa tunavutana na kuminyana nami ili waniwekee mipira ya oksijen.Wale madaktari wa mwanzo wakaingiwa na huruma wakaondoka .Asubuhi yake wakaja wengine na hawa wa mwisho ndio wakanizidi nguvu mpaka nikazimia ..... Mumenifahamu sawa sawa ....".