Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar aapishwa

Hayo ni mawazo yako, kwa akili ya kawaida haiwezekani Marais wa nne wawili Zanzibar na wawili bara wote wasiwe na huruma na watu hao. Angalia kwa jicho la sheria kuliko hisia za ukaidi
Sisi ni nchi huru, Hili suala la masheikh wa uamsho ni purely sovereign issue.
Wako katika mahakama zetu na jela zetu, na wala hawajashitakiwa kwenye mahakama za kimaitaifa.

Hao kosa lao kuu ni kuohoji muungano, wanataka wawafanye mfano kwa mtu yeyote atakayechallenge muungano kwa kiasi kikubwa kama walivyofanya wao
 
Sisi ni nchi huru, Hili suala la masheikh wa uamsho ni purely sovereign issue.
Wako katika mahakama zetu na jela zetu, na wala hawajashitakiwa kwenye mahakama za kimaitaifa.

Hao kosa lao kuu ni kuohoji muungano, wanataka wawafanye mfano kwa mtu yeyote atakayechallenge muungano kwa kiasi kikubwa kama walivyofanya wao
Unaweza kuwa sawa, lakini unahoji muungano na njia gani?
 
I guess shein anajutia nafsi yake na wale mahasidi walio taka kuuza Zanzibar kwa bei ya milion 100 Dodoma
 
Wasifu wa Mh. Othman Masoud Othman Sharif, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar

  • Mwanafunzi bora Chuo Kikuu ktk mwaka wa darasa lake UDSM
  • Ajiunga kazi Wizara ya katiba
  • Kwenda Uingereza na Italy kwa mafunzo zaidi
  • Mbobezi wa taaluma ya sheria LLB (UDSM) LLM (London) LLM (University of Turin Italy)
  • Member : Network of African Constitutional Lawyers for 1 year and 9 months https://ancl-radc.org.za/user/2206
  • Katibu Mkuu wizara
  • Mkurugezi wa Mashtaka - DPP Office, Zanzibar
  • Mwanasheria Mkuu wa Serikali - AG Zanzibar
  • Kutimuliwa mwaka 2014 toka utumishi wa serikalini wakati wa serikali ya Dr. Ali Mohamed Shein
  • ACT-Wazalendo chama kikuu cha upinzani Zanzibar chapendekeza jina lake kwa Mh. Rais Hussein Ali Hassan Mwinyi ili ateuliwe kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
  • Ateuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais (mteule) Zanzibar ktk serikali ya Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi. Sasa mara baada ya kuapisha kesho tarehe 2 March 2021 atakuwa mshauri mkuu wa Rais wa SMZ ili Rais atimize majukumu yake kama yalivyo matumaini ya waZanzibari na WaTanzania wengi wanaotaka mfumo bora wa maridhiano kuwa msingi mkubwa ktk uongozi na utawala.
  • 02 March 2021 aapishwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi
 
ACT wamechanga karata zao vizuri sana japo ni mapema kupredict kama huyu nae hatanywea. Ni muda sasa wa kuwastaafisha baadhi ya watu ambao wameng'ang'ania kuviongoza vyama vyao (a.k.a taasisi zao) tangu mwaka 1992 huko
Humjui vizuri huyo jamaa, yeye alikuwa ccm, ndio alikuwa mwanasheria mkuu wa Zanzibar, kwenye bunge la katiba alisimama kidete na msimamo usiyoyum a kupinga kuburuzwa na ccm ya Tanganyika, hii ilipelekea kuvuliwa nyadhifa zake zote ccm na uanasheria mkuu wa Zanzibar.

Hapo ndipo akaungana na Maalim Seif CUF na sasa ACT, huyo ni mtu sahihi aliyepatikana kwa wakati sahihi, huyo anamuogopa Mungu tu na si binadamu yeyote yule.
 
Chadema hawana mikakati ya muda mrefu chama kina mamiaka kibao hakijawahi toa waziri wala makamu wa Raisi wanakuja kupitwa na cha zitto kabwe chenye wafuasi ujiji kigoma tu tu.Chadema iko nchi nzima ila mikakati zero Zitto kabwe mwenye wanachama wengi ujiji tu katoa makamu wa Raisi Zanzibar!!!
 
02 March 2021
Ikulu
Mnazi Mmoja Unguja
Zanzibar

HAFLA NZIMA YA KUAPISHWA KWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR

 
Akili za Kitanganyika hizi, huyu kama ni ulaji alishaukataa tangu bunge la katiba, msimamo wake wa kutetea maslahi ya Zanzibar alikuwa anajuwa dhahiri shairi nini kitamkuta, hizi kauli za kijinga za ameula ndio zimesababisha Watanganyika na Wazanzibar waliopo ccm kuishi kinafki badala ya kusimama katika kweli, unafki unamfanya mtu mpaka anaogopa kuvaa barakoa kwa afya yake kwa kuogopa kumuudhi mtoa ulaji. Ni zaidi ya ujinga.
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemuapisha Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Othman Masoud Othman Sharif kutoka chama cha ACT-Wazalendo ameapishwa kushika wadhifa huo baada ya kuteuliwa hapo jana na Dkt. Mwinyi, zikiwa zimepita siku chache baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad.

Hafla ya kuapishwa kwa Sharif imefanyika Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Rais Dkt Mwinyi amemteua Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, baada ya kushauriana na chama cha ACT Wazalendo.

View attachment 1715334

TBC

Pia soma >>> Othman Masoud Othman Sharif ateuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Chama kinateua au rais anateua?
Mimi nadhani rais ANATHIBITISHA! Baada ya chama kuteua!
 
Back
Top Bottom