Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar aapishwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,776
2,000
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemuapisha Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Othman Masoud Othman Sharif kutoka chama cha ACT-Wazalendo ameapishwa kushika wadhifa huo baada ya kuteuliwa hapo jana na Dkt. Mwinyi, zikiwa zimepita siku chache baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad.

Hafla ya kuapishwa kwa Sharif imefanyika Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Rais Dkt Mwinyi amemteua Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, baada ya kushauriana na chama cha ACT Wazalendo.

1614672820833.png

TBC

Pia soma >>> Othman Masoud Othman Sharif ateuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,407
2,000
Mengi na mkubwa kumbuka wanashaurina mambo mengi msingi akili zbar moja na utulivu wa kisiasa lazima wakubaliane mambo mengi soon utaona wale masheikh wakiachiwa ...yapo mengi
Kwahiyo kazi ya Makamu wa kwanza ni kumshauri Mwinyi? over
 
All TRUTH

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
4,717
2,000
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemuapisha Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Othman Masoud Othman Sharif kutoka chama cha ACT-Wazalendo ameapishwa kushika wadhifa huo baada ya kuteuliwa hapo jana na Dkt. Mwinyi, zikiwa zimepita siku chache baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad.

Hafla ya kuapishwa kwa Sharif imefanyika Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Rais Dkt Mwinyi amemteua Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, baada ya kushauriana na chama cha ACT Wazalendo.

View attachment 1715334

TBC

Pia soma >>> Othman Masoud Othman Sharif ateuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Hongeraaaa kwake

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,979
2,000
Mengi na mkubwa kumbuka wanashaurina mambo mengi msingi akili zbar moja na utulivu wa kisiasa lazima wakubaliane mambo mengi soon utaona wale masheikh wakiachiwa ...yapo mengi
Ikiwa ni hivyo, Maalimu amehudumu nafasi hiyo kwa miaka kumi angeweza kuwatoa hao Masheikh. ni rahisi kupiga mbinja ukiwa nje ya mfumo lakini ukiingia na kwa Viapo vinavyoapishwa, ndipo unapogundua ni vigumu kutekeleza mawazo yako. Swala la Masheikh liko kisheria sana na lilishawahi kutolewa ufafanuzi ukizingatia Ugaidi una mikataba ya Kimataifa unaweza kukuta ufuatiliwaji si wa nchi moja.
 
Mwanamena

JF-Expert Member
Feb 4, 2020
658
1,000
Unavyoingia kwenye mfumo, mfumo ndiyo unaodictate nini kifanyike na siyo wewe. Kuna weza kuwa na ugumu Kama Jambo lile ni la kimfumo. Vinginevyo iwe Kama ya babu seya
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,420
2,000
ACT wamechanga karata zao vizuri sana japo ni mapema kupredict kama huyu nae hatanywea. Ni muda sasa wa kuwastaafisha baadhi ya watu ambao wameng'ang'ania kuviongoza vyama vyao (a.k.a taasisi zao) tangu mwaka 1992 huko
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
8,800
2,000
Ikiwa ni hivyo, Maalimu amehudumu nafasi hiyo kwa miaka kumi angeweza kuwatoa hao Masheikh. ni rahisi kupiga mbinja ukiwa nje ya mfumo lakini ukiingia na kwa Viapo vinavyoapishwa, ndipo unapogundua ni vigumu kutekeleza mawazo yako. Swala la Masheikh liko kisheria sana na lilishawahi kutolewa ufafanuzi ukizingatia Ugaidi una mikataba ya Kimataifa unaweza kukuta ufuatiliwaji si wa nchi moja.
Hakuna anachoshindwa kufanya Rais Magufuli kuhusu kuwatoa wale watu, ni ukaidi tu wa viongozi wa CCM kuanzia Kikwete mpaka huyu Magufuli.

Ugaidi gani ambao mwaka wa nane huu hakuna ushahidi wa kumaliza kesi?
 
NORTHERNIST

Senior Member
Feb 10, 2021
104
225
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemuapisha Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Othman Masoud Othman Sharif kutoka chama cha ACT-Wazalendo ameapishwa kushika wadhifa huo baada ya kuteuliwa hapo jana na Dkt. Mwinyi, zikiwa zimepita siku chache baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad.

Hafla ya kuapishwa kwa Sharif imefanyika Ikulu jijini Zanzibar na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Rais Dkt Mwinyi amemteua Othman Masoud Othman Sharif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu namba 39(3) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, baada ya kushauriana na chama cha ACT Wazalendo.

View attachment 1715334

TBC

Pia soma >>> Othman Masoud Othman Sharif ateuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
ameula
 
Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
3,979
2,000
Hakuna anachoshindwa kufanya Rais Magufuli kuhusu kuwatoa wale watu, ni ukaidi tu wa viongozi wa CCM kuanzia Kikwete mpaka huyu Magufuli.

Ugaidi gani ambao mwaka wa nane huu hakuna ushahidi wa kumaliza kesi?
Hayo ni mawazo yako, kwa akili ya kawaida haiwezekani Marais wa nne wawili Zanzibar na wawili bara wote wasiwe na huruma na watu hao. Angalia kwa jicho la sheria kuliko hisia za ukaidi
 
Kifoi

JF-Expert Member
May 12, 2007
1,159
1,500
Hayo ni mawazo yako, kwa akili ya kawaida haiwezekani Marais wa nne wawili Zanzibar na wawili bara wote wasiwe na huruma na watu hao. Angalia kwa jicho la sheria kuliko hisia za ukaidi
sheria gani labda sheria ya uharo kwa mujibu wa hiyo sheria hao walikuwa washtakiwe Zanzibar sio tanganyika
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom