Makamu wa kwanza wa Rais ni nani Zanzibar?

Nduka Original

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,012
816
Hii kitu huwa inanisumbua kidogo naomba kusaidiwa.

Muda wa Dkt. Mohamed Shein kulikuwa na Makamo wa pili wa Rais Balozi Seif Ally Eid lakini hakukuwa na Makamo wa kwanza wa Rais.

Hivyo hivyo Dkt. Mwinyi keshateua na kumuapisha Makamo wa pili wa Rais ndugu Hemed Suleiman Abdulla.

Je, Makamo wa kwanza wa Rais ni nani?
 
Makamu wa kwanza kwa mujibu wa Katiba hataki nafasi hiyo, anataka yeye ndio awe Rais wa Zanzibar wakati Wazanzibar wanamkataa kuanzia 1985 lakini kang'ang'ania kama ruba
 
Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar makamu wa kwanza wa Rais anatokana na ushindi wa pili wa Urais kwenye uchaguzi mkuu, kwa Zanzibar ni Maalim Seif.
 
Makamo wa kwanza wa Rais anatakiwa awe mmoja pekee, na anatakiwa awe alieshika nafasi ya pili kwenye uchaguzi uliofanyika. Hii nafasi imewekwa kama geresha tu ya kuwadanganya wapinzani wawe wanakubali matokeo yasiyo halali ya uchaguzi wa Rais.

Kitendo cha CCM kutengeneza nafasi ya makamo wa pili wa Rais, kinaonesha jinsi ambavyo CCM hawako tayari kufanya kazi na upinzani Zanzibar, huyo makamu wa kwanza wa Rais anageuka kuwa pambo tu.
 
Maalim anakwambia kama huo umakamu urais wa kwanza ni mzuri kwanini Mwinyi hautaki yeye huo umakamu?
 
Makamu wa kwanza anatakiwa awe mshindi wa pili wa Urais wa Zanzibar, hivyo ni Maalim Seif, bado anazuga zuga kuonyesha ana msimamo na sio mroho wa madaraka ila baada ya miezi michache atakuwa anapita na ving’ora kama Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar.
 
Back
Top Bottom