Makamu Rais:Wabunge wa CCM acheni vijimbe, Wapinzani wako makini.

mwembemdogo

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
2,282
1,252
Jana Makamu wa Rais,Mama Samia amewapasha Wabunge wa CCM mjini Dodoma wanatakiwa kuacha Vijembe bungeni badala yake wapewe elimu ili waweze kupambana Na Wapinzani kwani Upinzani una watu makini.Hakika Makamu wa Rais anaonekana amekerwa Na tabia ya wabunge wa CCM badala ya kuchangia hoja wao ni Vijembe utadhani nyimbo za taarabu.Mfano ni Mbunge wa Ulanga Mtoto wa marehemu Selina Kombani .Kijana huyu amediriki kuwatukana wabunge wa upinzani Na cha ajabu udhaufu wa Kiti cha Spika ulishindwa kukemea matusi hayo.Tabia ya maneno ya kuudhu Na vijimbe vya Wabunge wa CCM imekuwa Sugu watanzania tunapaswa kuikemea Na tabia hiyo ndio iliyotuvurugia Bunge la Katiba.Wito kwenu Wapinzani endeleeni ni Umakini wenu waacheni hao wasio Na hoja.
HAPA KAZI TU.
 
Naona pia angemwambia Tulia aache ukada kwani ndio anapwaya na yule mwenzake ambae wamefungia vyombo vya habari bungeni.Mama Samia washauri hao ni wachanga kisiasa
 
Ni jambo la kusikitisha kijana aliyeingia bungeni kwa mgongo wa "mwanamke" anapotumia udhaifu wa "mwanamke" kuwatukana "wanawake" wa upinzani asijue "wanawake" hao ndio waliyemhudumia na kumzika mama yake mzazi ambaye ni "mwanamke" mwenzao...Heshima kwa wakina mama wote duniani!!Happy Mothers day
 
Huyo jamaa amejitukanisha sana ila tumeujua upeowake aachwetu maana historia itamhukumu
 
Tunataka Mbowe atusomee report ya mapato na matumizi wakati Wa kampeni.

Haiwezekani watu wazalendo kwa chama wanajitolea kuchangia chama alafu hatusomewi matumizi.!!!
Inaonyesha hela nyingi zilichangwa lkn cha ajabu mawakala Wa chadema hawajalipwa hela zao hadi Leo!!!
Hatuwezi kuhubiri mabadiliko huku matendo yetu ni mabovu afadhali ya ccm.!!!
Mbowe tunaomba report ya matumizi ya hela zetu.
 
Back
Top Bottom