Makamu Mwenyekiti wa Yanga ' Tumbo Tumbo ' Fredrick Mwakalebela tafadhali acha ' Kudanganya ' Hayati Mkapa hakuwa Shabiki wa Yanga SC

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,877
Juzi ulipokuwa ukilialia kama ambavyo ' Voice Note ' yako ime ' trend ' kweli kweli kuhusu ' Kusakamwa ' na wana Yanga kwa kile walichodai kuwa ulikuwa ' ukiwahujumu ' nilikuonea Huruma na Kudhani wanakuonea ila kwa ' Uwongo ' uliousema Leo kuhusu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa nimeamini kuwa ' Kutokupendwa ' Kwako na wana Yanga ni sahihi mno.

Akizungumza bila Aibu wala Uwoga leo hii Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC Fredrick Lugano Mwakalebela a,k,a Tumbo Tumbo ' alidanganya ' na hadi ' Kuwadanganya ' wana Yanga SC na wana Umma kuwa Hayati Rais Mstaafu Mkapa alikuwa ni Mshabiki ' lia lia ' wa Yanga SC wakati ukweli ni kwamba Hayati Mkapa hakuwa Mpenda Soka wala Michezo.

Wakati wa Uzinduzi wa Uwanja wa Taifa ( sasa Uwanja wa Mkapa ) akihojiwa na aliyekuwa Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC wakati huo Abdallah Idrisa Majura kuwa Yeye ni Shabiki wa Timu hapa nchini Tanzania alisema kuwa hana Timu, hapendi Mpira na pia si Mwanamichezo kivile ile aliamua tu Kuwaachia Zawadi ya Uwanja Watanzania baada ya Kuona jitihada zao katika Michezo.
 
Mwaka 1995 baada ya kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea uraisi, Benyamin William Mkapa akiwa kwenye kampeni za urais aliutangazia umma kuwa yeye ni shabiki wa Yanga, ili kunogesha kampen sisi wanamichezo tukamshauri mpinzani wake, mzee wa kiraracha Lyatonga Mrema na yeye ajitangaze kuwa shabiki wa simba lakin mzee akakataa ‘wahenga’ wenzangu nadhani mnalikumbuka hili....
 
Yanga hawaishiwi vituko wanasema shabiki wao mkubwa hawataji hata kadi yake ya uanachama ingawa shabiki hatakiwi kuwa na kadi lakini mkapa kama shabiki mkubwa lazima angekuwa mwanachama.
Yanga wangeachana na mambo ya mpira wakawa wanatengeneza series waziite utopolo series
 
Mwaka 1995 baada ya kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea uraisi, Benyamin William Mkapa akiwa kwenye kampeni za urais aliutangazia umma kuwa yeye ni shabiki wa Yanga, ili kunogesha kampen sisi wanamichezo tukamshauri mpinzani wake, mzee wa kiraracha Lyatonga Mrema na yeye ajitangaze kuwa shabiki wa simba lakin mzee akakataa ‘wahenga’ wenzangu nadhani mnalikumbuka hili....
Hadi waambiwe alikuwa shabiki wa Mikia.
 
Back
Top Bottom