Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Arfi) atupa kadi kikaoni, atishia kujiondoa chamani!

Bado hujaona kama kuna tatizo ndani ya chama?

Matatizo yapo, absolutely. Na yataendelea kuwepo (kwa vyama vyote). The question is, njia bora ya kutatua tatizo is storm out? Hivi ukiwa na mgogoro kwenye familia yako unafungasha virago vyako na kuondoka?
 
Sasa vyama vitakua kama madhehebu ya dini!Ukimkorofisha anaenda kuanzisha chama chake!
 
Vijana tupunguze mihemko ya kisiasa,tamaa za madaraka na kutumiwa na vijana wenzetu wajanja wenye maslah yao kuwadhalilisha na kuwatukana wazee wetu wanaokipigania chama.
 
chanzo: Gazeti la mwananchi

chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kimezidi kuandamwa na migogoro baada ya jana kuibuka mwingine mkubwa katika kikao chake cha ndani mkoani katavi kiasi cha kumfanya makamu mwenyekiti wa chama hicho taifa, said arfi, kutupa kadi yake ya uanachama.

huu ni mgogoro wa pili mkubwa kuripotiwa katika kipindi cha juma moja lililopita baada ya ule wa wilayani karatu ambako pamoja na mambo mengine uliishia kwa kamati kuu kuusimamisha uongozi wote wa chama hicho wilaya.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa arfi ambaye ni mbunge wa mpanda mjini, alitishia kujitoa chadema jana, katika kikao cha kamati ya ushauri ya chama hicho mikoa ya katavi na rukwa kilichoketi namanyere, nkasi na kufikia uamuzi wa kumsimamisha mwenyekiti wa baraza la vijana mkoa wa rukwa, laurent mangweshi.

Katika kikao hicho, arfi anadaiwa kuichukua kadi yake ya chadema na kumtupia mwenyekiti wa chadema mkoa wa rukwa, john mallack akitangaza kuachia nyadhifa zote alizonazo, kisha kuondoka ukumbini, kabla ya kufuatwa na wazee wa chama hicho na kumsihi aichukue kadi yake hiyo.

Alifikia hatua hiyo baada ya kutokea sintofahamu kati ya wajumbe wa kikao hicho katika uamuzi huo uliofikiwa kwa kupiga kura za ndiyo na hapana.

Vyanzo vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vilifafanua kuwa arfi alikerwa na kauli iliyotolewa na mangweshi kuwa katika uchaguzi mkuu uliopita, alipokea rushwa kutoka kwa waziri mkuu, mizengo pinda.

Vyanzo hivyo vya habari vimeeleza kuwa kutokana na hali hiyo, arfi alipandwa na hasira na kuamua kumrushia kadi mallack kisha kutoka nje ya ukumbi.

“hatua hiyo ilifanya wajumbe wa kikao hicho nao kutoka nje ya ukumbi na kuanza kumbembeleza ili asichukue uamuzi huo na kisha wakamwekea kadi yake ya uanachama katika mfuko wake wa shati,” alisema mmoja wa makada hao.

Arfi mwenyewe hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo baada ya simu ya mkononi kuita muda wote bila kupokewa na hata alipotumiwa ujumbe, hakujibu.

Mallack akizungumza na gazeti hili kwa simu alikiri arfi kurusha kadi mezani kisha kutoka nje ya ukumbi, lakini akasema suala hilo lilishughulikiwa na wazee na kumalizwa.

“ni kweli unajua huyu ni makamu mwenyekiti wetu wa taifa, sasa inapotokea vijana wadogo wakamtuhumu kwa tuhuma za uongo na ambazo hazipo inatia hasira, ndiyo maana huyo kijana tumemvua uongozi,” alisema mallack.

tuhuma za mangweshi
mangweshi alisimamishwa uongozi baada ya kutuhumiwa kwa mambo mbalimbali ya kiutendaji ndani ya chama hicho ikiwamo kumkashifu arfi.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, mallack alisema kuwa magweshi amevuliwa uongozi baada ya chama hicho kujiridhisha kuwa alitenda makosa hayo.

Alisema kamati ya ushauri ilimwita ili kujibu tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikimkabili ikiwamo kutoa taarifa zisizo rasmi bila kufuata taratibu za chama.

“pia amepatikana na hatia ya kuandika barua za kashfa na kuzipeleka makao makuu ya chama kumkashifu arfi pamoja na viongozi wengine wa chama akiwamo katibu mkuu, dk willibrod slaa.

Katibu mwenezi wa chadema mikoa ya rukwa na katavi, john matongo alisema kabla ya kupewa adhabu ya kusimamishwa, amewahi kuonywa mara kadhaa lakini ameshindwa kujirekebisha.

pole sana makamu ,nimeanza kusikia unahujumiwa mda mrefu,nina ushahidi wakutosha kuwa kuna dada mmoja ambaye kajiunga chama mwezi wa tatu mwaka huu ndiye katumwa na kiongozi mtendaji wa juu wa chama kuja kukuhujumu uonekane haufai ili huyo dada ndiyo agombee ubunge mpanda 2015
wanasahau kwamba wewe ndio umekijenga chama mpanda mpaka kimefika hapo.
Makamu sikushauri ususie chama,wewe ni kiongozi na mbunge unapaswa kupambana mpaka mwisho kuhakikisha dhuluma na uonevu wowote kwenye chama unafika kikomo.
Askari bora ni yule asiyekimbia vita.
Okota silaha yako,mapambano yanaendelea.jipe moyo mkuu,yana mwisho.
 
Cc.. Nicolas, Kimbunga, chama, Nguruvi3, Mohamedi Mtoi, Pasco, Mwita Maranya, Jasusi, Mzee Mwanakijiji, FJM, Mingoi,
 
Last edited by a moderator:
Unakurupuka utadhani umefumaniwa hujui nilikuwa na mjibu nani.
Ndio tabu ya ndoto za mchana , jamaa wanaweweseka hao .. leo nimeelewa kwa nini wengine bado wanamiliki kadi za CCM kwa sababu wanajua Chadema ni kama barafu jua likiwaka itayeyuka na kupotea
 
pole sana makamu ,nimeanza kusikia unahujumiwa mda mrefu,nina ushahidi wakutosha kuwa kuna dada mmoja ambaye kajiunga chama mwezi wa tatu mwaka huu ndiye katumwa na kiongozi mtendaji wa juu wa chama kuja kukuhujumu uonekane haufai ili huyo dada ndiyo agombee ubunge mpanda 2015wanasahau kwamba wewe ndio umekijenga chama mpanda mpaka kimefika hapo.Makamu sikushauri ususie chama,wewe ni kiongozi na mbunge unapaswa kupambana mpaka mwisho kuhakikisha dhuluma na uonevu wowote kwenye chama unafika kikomo.Askari bora ni yule asiyekimbia vita.Okota silaha yako,mapambano yanaendelea.jipe moyo mkuu,yana mwisho.
acha upotoshaji, chanzo cha mgogoro Katavi ni kutowajibika kwa Arfi kisa anapumzika 2015(hagombei tena 2015)
 
pole sana makamu ,nimeanza kusikia unahujumiwa mda mrefu,nina ushahidi wakutosha kuwa kuna dada mmoja ambaye kajiunga chama mwezi wa tatu mwaka huu ndiye katumwa na kiongozi mtendaji wa juu wa chama kuja kukuhujumu uonekane haufai ili huyo dada ndiyo agombee ubunge mpanda 2015
wanasahau kwamba wewe ndio umekijenga chama mpanda mpaka kimefika hapo.
Makamu sikushauri ususie chama,wewe ni kiongozi na mbunge unapaswa kupambana mpaka mwisho kuhakikisha dhuluma na uonevu wowote kwenye chama unafika kikomo.
Askari bora ni yule asiyekimbia vita.
Okota silaha yako,mapambano yanaendelea.jipe moyo mkuu,yana mwisho.

Juliana,

Unaweza kutaja jina la huyo dada na huyo kiongozi aliyemtuma? Na je, uliwahi kuwasilisha malalamiko yoyote kwa makamu mwenyekiti wenu au kwa chama chako baada ya kupata huo ushahidi unaoeleza kuwa nao kabla ya tukio hili la jana la Arfi na kadi yake?

PM
 
pole sana makamu ,nimeanza kusikia unahujumiwa mda mrefu,nina ushahidi wakutosha kuwa kuna dada mmoja ambaye kajiunga chama mwezi wa tatu mwaka huu ndiye katumwa na kiongozi mtendaji wa juu wa chama kuja kukuhujumu uonekane haufai ili huyo dada ndiyo agombee ubunge mpanda 2015
wanasahau kwamba wewe ndio umekijenga chama mpanda mpaka kimefika hapo.
Makamu sikushauri ususie chama,wewe ni kiongozi na mbunge unapaswa kupambana mpaka mwisho kuhakikisha dhuluma na uonevu wowote kwenye chama unafika kikomo.
Askari bora ni yule asiyekimbia vita.
Okota silaha yako,mapambano yanaendelea.jipe moyo mkuu,yana mwisho.
Yana mwisho. Nasema yana mwisho. Watanzania makumi kwa makumi wanakufa kila siku kwa sababu ya unafiki wenu nyie wanasiasa. Ni kweli kwa sasa mnawezi kupewa visenti vya kuwatosha kutanua kwa kazi ya usaliti mnayofanya lakini kumbukeni yule MKUU WA VIUMBE VYOTE, ambae hadanganywi, wala hadhihakiwi ana namna nyingi za kutenda miujiza. Na nina uhakika ameshavisikia vilio vya Watanzania na atavijibu. Ole wako kama unafanya yote haya kwa faida yako wakati watu wanakufa. Nasema ole wako Juliana, ole wako Juliana , ole wako Juliana!!!! Wako wapi kina Gadaf na utukufu wao? Dunia hii tu wapitaji hivyo tujaribu kutenda mema kwa kadiri ya uwezo wetu. Elimu uliyopewa sio ya kuwaangamiza Watanzania wanyonge wasio na mtetezi na wasiojua kinachoendelea. Siku ya siku yaja Bwana wa Majeshi ataamua kuwatetea! Haya maneno kuna siku utayakumbuka!!!!

Tunahitaji kuvuka mipaka ya kidini, kikabila na kisiasa na kujadili taifa letu. Vyama hufa lakini taifa litaendelea kuwepo.

Kijana alikuwa na haki ya kutuhumu kama tunavyotuhumu walioweka fedha Uswiss bila kujali nafasi zao kitaifa.

Arfi alitakiwa kujenga hoja kupangua tuhuma dhidi yake.
 
Pandikizi hapo nani sasa? Arfi au huyo kijana aliyemzulia Arfi kama kapokea rushwa toka kwa Pinda? kama Arfi pandikizi wa CCM kwa nini Pinda atoe rushwa kumpa Arfi?
Kiongozi anayekimbilia kutupa kadi au kujivua uanachama chama chake kinapokuwa na matatizo si kiongozi kitu bali mzigo. Hivi kila mwanandoa atakimbilia talaka baada ya ndoa kukumbwa na misukosuko ya kawaida si wote tutakuwa wahuni? Arfi atafute sababu nyingine ya kujiondoa chamani na wakati muafaka. Vinginevyo ataonekana sawa na mapandikizi na wachumia tumbo na mapandikizi wengine. Rafiki wa kweli utamjua wakati wa dhiki na si mwisho wa mwezi. Kama Arfi kafanya hivyo basi CDM wamtue haraka kabla hajawaozea.
 
Acha hizo kaka.Mbinu yenu na mnaowatumia wanajulikana.

Wewe mwenyewe ben unatumiwa kukivuruga chama chetu bt tunakuambia hatuvurugiki abadan utaondoka wewe chadema kama kina lukosi na wanafik wengne chadema imara haitingishiki
 
pole sana makamu ,nimeanza kusikia unahujumiwa mda mrefu,nina ushahidi wakutosha kuwa kuna dada mmoja ambaye kajiunga chama mwezi wa tatu mwaka huu ndiye katumwa na kiongozi mtendaji wa juu wa chama kuja kukuhujumu uonekane haufai ili huyo dada ndiyo agombee ubunge mpanda 2015
wanasahau kwamba wewe ndio umekijenga chama mpanda mpaka kimefika hapo.
Makamu sikushauri ususie chama,wewe ni kiongozi na mbunge unapaswa kupambana mpaka mwisho kuhakikisha dhuluma na uonevu wowote kwenye chama unafika kikomo.
Askari bora ni yule asiyekimbia vita.
Okota silaha yako,mapambano yanaendelea.jipe moyo mkuu,yana mwisho.

Dada Juliana mwaga vitu vyote hadharani.

Haiwezekani chama kiwe miliki ya watu.

Pamoja sana
 
Vipi tena makamu mwenyekiti wetu! Inakuwaje tena kukimbilia kujivua uanachama kwa kukashifiwa na mtu mmoja tu? Ingekuwaje kama hiyo ingekuwa ndiyo kauli ya chama? Inatia wasiwasi sana maana ukomavu wa uongozi ni pamoja na kujua njia sahihi za kukabiliana na misukosuko unayokumbana nayo ikiwa ni pamoja na uwezo wa kutunza hasira zako. Ni kweli kwamba inaudhi sana kusingiziwa kitu ambacho hujakifanya, lakini usikubali hasira zikuamulie hatua za kuchukua, bali kama mtu mkomavu, tawala hasira zako na ruhusu busara na hekima zikuamulie hatua za kuchukua. Hasira mara nyingi mwisho wake ni hasara. Ningependa kukuhakikishia kwamba hakuna popote utakapokwenda usikutane na maudhi. Kutupa kadi kikaoni ni fedheha mbaya sana kwa kiongozi wa ngazi ya juu kama wewe. Vijana wanaolelewa kisiasa katika chama chako watachukua mfano gani kwa wewe kurusha kadi? Tawala hasira zako Mhesimiwa au labda una lingine jambo basi itakuwa vema ukaliweka wazi ili unapoondoka chadema ijulikane wazi. Ni fedheha wewe kuondoka kwa kukashifiwa na mtu ambaye hata sasa amesimamishwa uongozi.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom