Makamu Mwenyekiti Taifa mstaafu (TLP) ahamia CHADEMA

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
SAKATA la wimbi la viongozi wa vyama vya siasa nchini kujiunga na Chadema, limeendelea mkoani hapa baada ya Makamu Mwenyekiti mstaafu wa TLP, Tanzania Bara, Westgate Rumambo kujiunga na chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati hivi karibuni, Rumambo alisema amejiunga Chadema baada ya kubaini ndicho chama pekee kinachotetea wanyonge.

“Jamani hivi sasa TLP haina mvuto tena, kwa wana mageuzi nchini kimeonekana ni chama cha mtu mmoja kuliko Chadema ambacho kina malengo mazuri ya kukomboa Watanzania hasa wa ngazi ya chini,” alisema Rumambo.

Alisema atatumia uzoefu wake wa harakati za kuongoza mageuzi nchini, kuhamasisha jamii na kuiimarisha Chadema mkoani hapa, ili uhuru na mabadiliko ya kweli vipatikane.

Katibu Mwenezi wa Chadema Babati Mjini, Zahir Musa alisema wanampokea kwa mikono miwili Rumambo kwani ni mtu makini mwenye uchungu na mabadiliko.

Musa alisema watashirikiana na Rumambo katika uendelezaji wa Chadema mkoani hapa na wanatarajia kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwake kwani ana uzoefu wa uongozi wa mageuzi nchini.

“Tumempokea mwanachama mpya wa Chadema na tunatarajia kumkabidhi kadi ya Chadema na kuanza mapambano ya kuhakikisha mwaka 2015 tunachukua jimbo la Babati Mjini,” alitamba Musa.

Rumambo hakukabidhi kadi yake ya TLP kwa madai kuwa ilishapotea muda mrefu na baadhi ya wafurukutwa wa Chadema mjini Babati walimpongeza kwa uamuzi wa kujiunga Chadema.

Walisema hivi sasa chama pekee cha upinzani kilicho na nia ya mabadiliko makini na chenye lengo la kuwafikisha wananchi wanakotaka ni Chadema pekee na ndiyo sababu vijana wengi wanaiunga mkono.

Source HabariLeo.
 
Source tu ndiyo imenifurahisha
 
acheni ngano na magugu zimee pamoja siku ikifika watachujwa tu kujua ngano ipi na magugu yapi!!
 
hata maji yanapokuja mengi baharin huwa na vng, mawimbi hufanya kaz kuchambua.
 
Hongereni makamanda kwa kazi nzuri.
Mh. Lema kazi yako inaonekana, ila kuna tatizo bado huku kwenye ukanda wa pwani (Tanga - Mtwara). Nao wanahitaji elimu vile vile.
Tukipambana kwa nguvu zote, 2015 tunawafukuza walanguzi na majambazi wa magogoni...
 
...

Rumambo hakukabidhi kadi yake ya TLP kwa madai kuwa ilishapotea muda mrefu na baadhi ya wafurukutwa wa Chadema mjini Babati walimpongeza kwa uamuzi wa kujiunga Chadema.

...

Source HabariLeo.

CHADEMA, kemeeni upuuzi huo hapo kwenye
red; misemo ya kimagamba. Misamiati ya magamba na makuwadi zao isiruhusiwe kuingizwa wala kuhusishwa kwa namna yoyote na mfumo wa ukombozi wa taifa letu.

Ukiangalia kwa jicho makini, hilo neno halijaingia kwa bahati mbaya kwenye habari husika, bali limeingizwa kwa makusudi na mwandishi (wa HabariLeo) kwa malengo maalumu.

Neno, itikadi, mtazamo, falsafa, au chochote chenye malengo au kinachofungamana kwa namna yoyote na yeyote au lolote lililo kinyume na NGUVU YA UMMA na falsafa au itikadi zake yapasa kukemewa mara moja.

Chadema haina na wala haijawahi kuwa na magenge ya wakereketwa au wafurukutwa (naona hata kinyaa kuyaandika) ambayo kimsingi ni magenge ya kijambazi na kihuni. Ndio hawa hawa wanaofanya uhuni wa ajabu ikiwemo kuchochea fujo mitaani na hata kutuulia viongozi wetu!

Nguvu ya Umma ni muunganiko wa umma mzima kwa ajili ya kudai haki, usawa, na hatimaye ukombozi wa taifa zima dhidi ya tabaka dogo la watawala na familia zao almaarufu kama "mkoloni mweusi". Ni harakati za kupigania heshima ya utu wa mwanadamu kwa faida ya kizazi kilichopo na kijacho.
 
Mkuu
Usikonde, hilo gazeti ndio linatumia lugha hizo!!

HabariLeo=Magamba!!!

Mkuu nimekuelewa vizuri sana ila kwa bahati mbaya ni wachache kama wewe wanaoelewa lugha za hilo gazeti. Haya mambo yasipowekwa vizuri, misemo na lugha za aina hiyo inaweza kutumika kuuhadaa umma wakaishia kuona kumbe Chadema ni sawa tu na wale "wengine". Hapana, kila wapatapo nafasi kama kwenye mikutano n.k. viongozi wafafanue mambo haya.
 
Back
Top Bottom