POTOSHI Makamu mwenyekiti CHADEMA Zanzibar ametoa shukrani kwa serikali?

POTOSHI Makamu mwenyekiti CHADEMA Zanzibar ametoa shukrani kwa serikali?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2


1781168174727.png
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na video inayosambazwa mtandaoni ikiwa imeambatanishwa na Taarifa inayosema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika kikao chake cha ndani kilichokaa Zanzibar chini wa makamu wenyeviti wake wawili kimedhihisha ukomavu wa kisiasa hasa baada ya kufanya tathimini ya kina ya mwenendo wa uendeshaji wa chama chao na namna wanavyojipanga sasa kushirikiana na Serikali iliyopo madarakani ili kwa pamoja kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa makamu mwenyekiti wa Chadema Zanzibar kwa niaba ya chama hicho ameipongeza Serika kwa namna inavyoendelea kushughulikia changamoto za chama chao na ameahidi yeye na chama chake ikiwa pamoja na kuwaagiza viongozi wa Chadema nchi nzima kuendelea kushirikiana na Serikali ili kuwaletea Maendeleo watanzania.


Je,ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck imejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa kwa kukata na kuunganisha vipande visivyohusiana hiyo kutengeneza ujumbe tofauti na video halisi.

Katika video halisi makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar, Said Mzee aliagiza kufunguliwa kwa ofisi za chama hicho Zanzibar baada ya chama hicho kushinda kesi ya Zuio la Kisiasa nchini.

Aidha Said Mzee aliwashukuru wafuasi wa chama hicho kwa kuwa na imani na chama hicho huku akiwasisitiza kuendelea kukiunga mkono.

"Tunatoa shukrani kwa uamuzi na wanachama wetu kwa kuendelea kuwa na imani na wanachama wetu, tunasisitiza kuwa tutakuwa imara kupigania maslahi ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Tunatoa wito kwa wazanzibari wote na watanzania kuendelea kuiunga mkono CHADEMA kwa sababu ndiyo chama sahihi kitakachofikia malengo ya wazanzibari kuwa na serikali yao yenye uhuru na yenye maamuzi kamili kwa wazanzibari wote"

Aprili 15, 2026 Mahakama ya Rufani Kanda ya Dodoma, ilitengua maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyokizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanya shughuli za Siasa nchini, kufuatia kesi iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar), Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya chama hicho.
Back
Top Bottom