Makamu Mwenyekiti CCM, Mzee Mangula: Bagamoyo tuliahidi kujenga Gati sio Bandari

Tuliwaambia toka mwanzo watenganishe kofia hizi wakagoma, sasa unapata wapi nguvu ya kumpinga Mwenyekiti wako wa chama ambaye ndiye Rais wa nchi na amri jeshi mkuu nje ya vikao vya chama.

Huyu mzee naona waliomshauri wamekosea sana.
Hatuna Raisi, nchi ipo kwenye auto-pilot
 
Suala la bandari ya Bagamoyo ni suala la kitaifa, yaani ni maslahi ya taifa. Ikiwa na maana kwamba mradi ukipitishwa ukafanikiwa utakuwa na manufaa kwa taifa, ukiwa na hasara, huo mzigo wa hasara wanabebeshwa wananchi.

Ikiwa kweli mkataba ulijadiliwa na wabunge 60 tu, je kwa nini wengine hawakushirikishwa? Kwa nini iwe hivyo? kuna siri gani?
 
Weee! Atakifanyia wapi? Kwa nguvu gani?

Alisulubiwaga na Kikwete huyu mzee akaenda kulima nyanya kwao Matibhila Iringa huko. Mbona hakuthubutu kumwondoa Kikwete?
Why alirudishwa?

Za chinichini ni kuwa Kikwete alitaka kupinduliwa, Mangula na wazee kadhaa wakasaidia jahazi...
 
Huyu mzee badala ya kuongelea mambo ya msingi ya hitaji la nchi yaani Katiba mpya, yeye anamshambulia mwenyekiti wake tena hadharani - protocol gani hii.
 
Bible inasema Maisha ya Mwanadamu ni miaka 70. Kuwaachia watu wafanye kazi beyond their life span ndiyo tatizo linapokuja.

Kama Mangula anajua kuna tatizo kwenye huo mradi si aseme wazi wazi tu. Yaani yeye ni mtu kweli wa kumuogopa Maza. God forbid!
Kufikia hatua ya kutoa kauli kama hiyo hadharani basi jua hiyo bandari haitajengwa ,huyu katumwa kusema aliyoyasema na nimsimamo wa chama na vyombo vya ulinzi itakua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😆😆😆😆 mzee Mangula hapimi alama za nyakati anafikili Mzee Mkapa bado yuko hai au Magufuli.

Anapaswa atambue kuwa waliopo na wenye nguvu chamani ni Mzee wa Msoga na Mama mwenyewe.

Hebu ajikumbushe bifu lake na Mzee wa Msoga lilivyokuwa mpaka ukatupwa nje ya ulingo.

Mzee Mangula acha hizo usije ukajiharibia wakati unafikia mwishoni, acha insurbodination kwa Mama, utaishia kubaya.

Hivi Kikwete au sijui Mzee wa Msoga yeye ni immortal ? Yaani hawezi kufa au hatofariki ? Kwa nini mnaweka matarajio mengi sana kwa Binadamu ambaye ana nyama na damu tu ?

Chochote kinaweza kutokea, hao Wazungu wanaweza kuwachenjia muda wowote tu, …
 
Wenyeviti watatu,tangu kwa JK

Kauli ya JPM na CAG inamajibu,
Kauli zilizofuata zina maswali mengi kuliko majibu
1.Tupo kwenye mazungumzo kuona mapungufu yako wapi
2.Waziri,hakuna mkataba uliwahi sainiwa na hakuna nyaraka yoyote.
3.Ilani yetu inaonyesha kujenga gati.
Gati la nini?
Kwanini bunge huwa halichambui mikataba nakuwekwa wazi kama walivyofanya kwenye Tozo.
Tusubiri tuone may be with our noices and concern wanaweza kufanya hivyo kwa nia na lengo la kuonyesha kuwa wao, yaani Bunge na Serikali, ni WASIKIVU!
 
Bible inasema Maisha ya Mwanadamu ni miaka 70. Kuwaachia watu wafanye kazi beyond their life span ndiyo tatizo linapokuja.

Kama Mangula anajua kuna tatizo kwenye huo mradi si aseme wazi wazi tu. Yaani yeye ni mtu kweli wa kumuogopa Maza. God forbid!
Waliomuwekea sumu si hao hao viongozi wenzake, lazima awe na hofu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Waliomuwekea sumu si hao hao viongozi wenzake, lazima awe na hofu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Tatizo la kuendeleza Madaraka wakati muda ushapita.

Hapo alipowekwa ni strategy ya CCM kuonyesha kuwa bado kuna Wazee wanaipa direction CCM. But in reality this is not happening, wanatumiwa. Anachofanya ni kujitutumua kuonyesha kuwa bado yupo na ana nguvu but in reality wote tunajua kuwa Mwendazake alishawamaliza.
 
Tatizo la kuendeleza Madaraka wakati muda ushapita.

Hapo alipowekwa ni strategy ya CCM kuonyesha kuwa bado kuna Wazee wanaipa direction CCM. But in reality this is not happening, wanatumiwa. Anachofanya ni kujitutumua kuonyesha kuwa bado yupo na ana nguvu but in reality wote tunajua kuwa Mwendazake alishawamaliza.
Acha uzushi ww........
 
sahau ndugu, sahau kabisa, kwa mfumo wetu na katiba yetu Rais huwezi kumfanya chochote, sana sana utaishia kuumia.

Kama unabisha kamuulize Mzee Membe alikwama wapi kupiga kampeni hata moja, na majuzi kaomba kujisalimisha mwenyewe, mikono juu mwendo wa mateka.


Ni hivi, nguvu ya Rais ni kubwa sana lakini pia inategemea, chama chako kiko na wewe, asilimia fulani ya wananchi wako na wewe. Ukipoteza hivi viwili Chama na Raia utategemea kitu kimoja Jeshi, usalama, polisi.

Hao pia ni raia, wanaona ugumu wa maisha, ubaguzi, kiburi, wanatukanwa kila siku directly or indirectly, wenyewe na ndugu zao wanaumia na ugumu wa maisha kwa maamuzi yasiyo sahihi.

Watavumilia, ila itafikia sehemu, wakati(Tipping, critical point) mambo yatakuwa hayavumiliki.
 
Mzee Mangula anasema kwenye ilani ya CCM 2020-25 hawakuahidi bandari ya bagamoyo bali waliahidi ghati tu.

Hivyo anashangaa mjadala wa ujenzi wa bandari bagamoyo unatoka wapi.

Mzee Mangula hapa nadhani wa kumuuliza zaidi ni mwenyekiti wake ambae alisema ana habari njema kuwa wamefufua mazungumzo mradi wa bandari Bagamoyo.

Huu mshangao wa mzee Mangula una walakini ndani yake.

Chini nimeweka video Mama Samia akisema ana habari njema kuhusu ujenzi wa bandari bagamoyo, ngoja tuone panapovuja.

---

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Philip Mangula amewataka Watanzania kutohangaika na upotoshaji unaofanya na baadhi ya watu mitandaoni kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, na kwamba wamuache Rais Samia Suluhu Hassan afanye kazi yake ya kutekeleza mipango ya maendeleo.

Amesema hayo akizungumzia ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani ambapo amebainisha kuwa bandari hiyo haijapitishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya 2020-2025, hivyo hakuna sababu ya kuwapotosha wananchi, badala yake waunge mkono utekelezaji wa miradi iliyoahidiwa.

“Nashangaa huu mjadala unatokea wapi kwa kuwa mradi huo haupo. Hakuna haja ya watu kupotosha wananchi,” amesema Mangula akizungumza na Gazeti la Uhuru na kueleza kwamba kilichoahidiwa ni ujenzi wa gati ya Bagamoyo.

“Ipo miradi ya maboresho ya bandari, lakini kwa upande wa Bagamoyo kilichopitishwa ni ujenzi wa gati, sio bandari,” amesema Mangula.

Juni mwaka huu akizungumza na wafanyabiashara, Rais Samia Suluhu Hassan aliweka wazi kuwa serikali imeanza mazungumzo ya kufufua mradi wote wa bagamoyo ambao unajumuisha bandari na eneo la maalum la uwekezaji.

Akiwa madarakani, Hayati Rais John Magufuli alikataa kuendeleza mradi huo ambao mkataba wake ulisainiwa wakati wa uongozi wa mtangulizi wake, Rais Dkt. Jakaya Kikwete, kwa maelezo kwamba masharti yake hayakuwa rafiki na kwamba yangeliingiza Taifa matatizoni.

Nape Nnauye amjibu Mangula, ni Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo


Hiki chuma cha puwa kina itwa Mangula ni moja ya chuma kina tisha sana. Yani hata akiondoka nikama ccm inakaribia mwisho. Sijuwi ana siri gani.
 
Back
Top Bottom