Makamu Mwenyekiti BAVICHA akamatwa na jeshi la Polisi kwa kutoa kauli za kichochezi

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
Tayari Jeshi la Polisi limemkamata Makamu M/kiti wa BAVICHA muda huu hapa Iringa Mjini baada tu ya kumaliza Mahafali ya CHASO.

Kosa ni la uchochezi wa Kisiasa ambalo alilitenda akiwa Dar Es Salaam katika Mahafali ya CHASO ya tarehe 18/06/2016.

Hivyo atasafirishwa kutoka Iringa kwenda DSM kwaajili ya mahojiano na baadae Mahakamani.

Imetolewa June 26

Edward Simbeye
Katibu Mwenezi BAVICHA Taifa
=============

ALICHOSEMA OLE SOSOPI KWA JESHI LA POLISI

''Sasa kama vijana tuna wajibu mkubwa sana. Nitoe wito nikiwa kama kiongozi wa vijana.

Hili jeshi la polisi, hii salamu iwafikie polisi. Hili jeshi la polisi linaendelea kutumika na Chama Cha Mapinduzi, wakati 90% ya jeshi la polisi tunaishi nao mtaani na hawaishi kwenye makambi yao. Sasa ifike mahali tuseme INATOSHA... Tunaanza na wao kule mtaani (Makofi yanarindima).

If you do me, I do you (shangwe). Hii ndio iwe iwepo ama tukubali km vijana, hili jukumu ni la sisi, sio la akina mzee Lowassa tena.

Ninaomba nitoe wito kwa vijana popote. Na kwa sababu waandishi wa habari mko hapa msichakachue. Tunasema ‘Sasa Inatosha’... Sasa...? (Inatoshaaaaa).

Na kama wanafikiri nafanya uchochezi, maana sasa hivi ikitokea umesifia serikali ya Magufuli unahojiwa, ikitokea umeweza kukosoa unahojiwa.

Vijana wa CHADEMA tunasema, Kama Mbwai na iwe Mbwai – Tunaingia mtaani'' (shangwe).
 
kijana hachomoki hapo....hakuzingatia nini cha kuongea kwenye public.
kiusalama alikosea sana kuongea yale maneno.sitashangaa wengine wakimtetea tena humu.mimi ni mpinzani lakini kiukweli alikosea sana kulingana na nafasi yake
Hebu wapige kidogo kwenye miguu ndio ataelewa nini cha kuongea siku nyingine. Hata Isimani alitupuuzia sana wakati wa uchaguzi na kujiona yeye ndo yeye na kutamka kauli mbofu mbofu sana kwa sisi wanaharakati.
 
Wameanza kutekeleza agizo la "faza house '. Ila tuwe macho hawakawii' kumpandisha cheo" ili wapande cheo!
 
kijana hachomoki hapo....hakuzingatia nini cha kuongea kwenye public.
kiusalama alikosea sana kuongea yale maneno.sitashangaa wengine wakimtetea tena humu.mimi ni mpinzani lakini kiukweli alikosea sana kulingana na nafasi yake
Hebu wapige kidogo kwenye miguu ndio ataelewa nini cha kuongea siku nyingine. Hata Isimani alitupuuzia sana wakati wa uchaguzi na kujiona yeye ndo yeye na kutamka kauli mbofu mbofu sana kwa sisi wanaharakati.
Kwanini asikamatwe siku ile ile aje akamatwe leo? Polisi wa Dar walishindwaje kumkamata? Wameona Mahafali yamefanyika kwa Amani wakakosa cha kufanya hivyo wakaona wamkamate Sosopi ili kuondoa nuksi sio?
 
usihoji na kujijibu kiushabiki....!
 
kijana hachomoki hapo....hakuzingatia nini cha kuongea kwenye public.
kiusalama alikosea sana kuongea yale maneno.sitashangaa wengine wakimtetea tena humu.mimi ni mpinzani lakini kiukweli alikosea sana kulingana na nafasi yake
Hebu wapige kidogo kwenye miguu ndio ataelewa nini cha kuongea siku nyingine. Hata Isimani alitupuuzia sana wakati wa uchaguzi na kujiona yeye ndo yeye na kutamka kauli mbofu mbofu sana kwa sisi wanaharakati.

...una chuki binafsi toka siku nyingi,huna lolote!
 
Kwanini wamewaacha Meya wa Jiji na Kamanda Lowassa waliokuwa wazungumzaji wakuu ?
 
kijana hachomoki hapo....hakuzingatia nini cha kuongea kwenye public.
kiusalama alikosea sana kuongea yale maneno.sitashangaa wengine wakimtetea tena humu.mimi ni mpinzani lakini kiukweli alikosea sana kulingana na nafasi yake
Hebu wapige kidogo kwenye miguu ndio ataelewa nini cha kuongea siku nyingine. Hata Isimani alitupuuzia sana wakati wa uchaguzi na kujiona yeye ndo yeye na kutamka kauli mbofu mbofu sana kwa sisi wanaharakati.
Aliongea nini? Na kwanini hakukamatwa pale pale.
 
Ni uonevu tu unaofanywa wa kuwaweka Watanzania roho juu wa kushindwa kukemea maovu na utendaji mbovu ndani ya Serikali hii na Serikali zilizopita.
 
Back
Top Bottom