Makamu Mkuu wa Shule asimamishwa kazi kwa tuhuma kujihusisha mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha 4

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,302
5,439
Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Singida, Manispaa ya Singida, Thomas Ngiracha, amesimamishwa kazi kwa muda usiojulikana kwa tuhuma za kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne (jina tunalihifadhi) wa shule hiyo.

Mkuu wa Shule hiyo, Joseph Shani na Mkurugenzi wa Shule, Matliga Makuza walithibitisha kuchukuliwa kwa hatua hiyo dhidi ya mwalimu huyo.

Mwalimu Ngiracha (mtuhumiwa) alipoulizwa kwa njia ya simu alikiri kusimamishwa kazi kutokana na kuhusishwa na tuhuma hizo na kwamba suala hilo linashughulikiwa na vyombo vingine vya sheria.

"Ni kweli suala la kunihusisha mimi na tukio hilo zipo, lakini kimsingi sio za kweli, kwa sasa linashughulikiwa na vyombo vingine vya sheria," alisema.

Naye, Mkuu wa Shule huyo, Shani amesema mwalimu huyo ambaye pia alikuwa Mwalimu wa Nidhamu alisimamishwa kazi Mei 28, 2022 baada ya kikao cha uongozi wa shule kilichofanyika Mei 27, 2022 ambacho alimshirikisha Mkurugenzi wa Shule.

Shani alisema uongozi wa shule ulipata malalamiko kutoka kwa mwanafunzi Mei 23, 2022, kwa kuandika barua kuelezea usumbufu anaoupata kutoka kwa mwalimu huyo ambaye alimlazimisha awe na uhusiano naye na kufanya naye mapenzi mara kadhaa.

Alisema baada ya barua hiyo, uongozi wa shule ulimuita mwanafunzi na wenzake kuwahoji kuhusu suala la mwalimu huyo kuwa na mahusiano ya mapenzi na mwenzao ambao walithibitisha jambo hilo.

"Nilivyopata malalamiko kwa maandishi kutoka kwa mwanafunzi tulikaa kikao na Mkurugenzi wa Shule tukaamua kumsimamisha kazi Mei 28, 2022," alisema.

Alisema suala hilo lilifikishwa hadi kwa Ofisa Elimu wa Mkoa, Jeshi la Polisi na Dawati la Jinsia ambao wanaendelea kulifanyia kazi kwa taratibu nyingine za kisheria.

Alisema uwezekano wa mwalimu huyo kurejea shule hapo kuendelea na kazi haupo kwa sababu tayari uongozi wa shule umeshachukua hatua za kuajiri walimu wengine ambao wameziba nafasi yake.

Taarifa zaidi kutoka katika shule hiyo inadaiwa awali mwanafunzi huyo baada ya kuwa amelalamikia kitendo anachofanyiwa na mwalimu huyo na uongozi wa shule kutochukua hatua, alilazimika kwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kupeleka malalamiko yake kwa Ofisa Elimu wa Mkoa.

Kabla ya taarifa kufikishwa mkoani, mwalimu anayetuhumiwa kufanya kitendo hicho alianza kumzushia makosa mwanafunzi huyo na kumpa adhabu kadhaa, ikiwa ni mbinu ya kumdhibiti asieleze suala la mahusiano yao kwa watu wengine.

"Mwalimu alianza sana kumwandama mwanafunzi (anatajwa jina) na kwa kumpa adhabu ya kulima majani, alimpiga hadi mkono ukavimba, visa vilikuwa haviishi," kilisema chanzo kimoja cha habari.

Taarifa zaidi zimedai kuwa mwanafunzi huyo aliitwa kwa mwalimu huyo usiku na kuamua kuwachukua wenzake ili washuhudie.

"Huyo mwanafunzi baada ya kuitwa kwa sababu aliona imekuwa kero alikwenda na wenzake wawili, mmoja alisimama dirishani na mwingine mlangoni, mwanafunzi alipoingia tu ofisini mwalimu alizima taa kwa hiyo mwanafunzi aliyekuwa mlangoni akagonga mlangoni na kujifanya ana shida ndipo mwalimu akaamua kuwasha taa na hakufanya lolote," kilieleza chanzo hicho.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa siku moja mwalimu huyo baada ya suala hilo kujulikana kwa kuwa alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya Shule, aliamua kuitisha kikao cha kamati yeye mwenyewe mtuhumiwa, lakini baada ya kugundua suala hilo halijakaa vizuri kwa upande wake aliamua kukiahirisha ghafla wakati kilikuwa kimeshaanza.

Chanzo: IPP
 
Huyu mwalimu mbona kama anasingiziwa? Mwanafunzi anasema alishafanya naye mapenzi mara kadhaa sasa iweje alalamike? Kwani alikuwa anavutwa kwa kamba? Pia mkuu wa shule inaonyesha ana chuki na huyo mwalimu. Anasema uwezekano wa huyo mwalimu kurudi shuleni haupo maana tayari nafasi yake imeshajazwa, sasa inajazwaje wakati kesi haijaisha? Mkuu wa shule ni kama keshatoa hukumu.
 
Walimu tafuteni pesa za kutosha mbona mabinti wamejaa tele mtaani hata bikra zipo nyingi tu,achaneni na wanafunzi mnaowafundisha mtakuja kuinamishwa bure kwa tamaa na ujinga wenu.
 
Walimu tafuteni pesa za kutosha mbona mabinti wamejaa tele mtaani hata bikra zipo nyingi tu,achaneni na wanafunzi mnaowafundisha mtakuja kuinamishwa bure kwa tamaa na ujinga wenu.
Mkuu,hawa hawa wanafunzi ndo ambao wakibadilisha sare zao nakuingia mitaani unasema mabinti wamejaa mtaani.Nikwamba baadhi yao wana tabia zakupenda ngono nawakistukiwa wanajificha kwenye kivuli Cha uanafunzi.
Pole mwalimu kwa kupoteza kibarua,japo huna kesi yakukufunga
 
  • Thanks
Reactions: y-n

Una uhakika gani kama hana kesi ya kufungwa?
 
Sio rahisi mwanafunz kuandik barua y kusumbuliwa na kukiri kufanya mapenzi mara kadhaa, alilazimish kuandik kama ushahid wa kumtia hatia mwl
 
Mtoto wa kinyiramba huyo inaonekana amepata bwana mwingine anaejua kumkaza vizuri mpaka mapenzi yake kwa ticha wa nidhamu yameisha.
Ticha wa nidhamu nae akaamua kufosi mapenzi kwa kutumia mamlaka yake vibaya, hatimae toto la kinyiramba likaamua kupindua meza kwa kushirikiana na bwana wake mpya ambae atakua ni kiongozi hapohapo shuleni.
Hapa kuna dalili za mateachers kugombea demu.
 
Mwalimu mpya aliyeajiriwa na serikali wiki chache zilizopita mpwayungu village, akiona mada kama hizi mate yanamtoka mdomoni! 😋

Hata hajui kama kuna kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la mwalimu kumbaka mwanafunzi wake.
 
Ukiwa na macho matatu hapa,kilichoelezwa Ni tofauti na kilichopo!inawezekana kweli mwalimu alikuwa anadate na huyo mwanafunzi Ila Ticha ana kabifu Fulani na mkuu wake wa kazi😞😞.
Kama ushahidi ndiyo hayo maelezo yaliyotolewa hapo juu nachelea kusema MWALIMU HANA KESI YA KUJIBU.

Waalimu wa kiume tuache utani wa kijingajinga na hivi vibinti vya shule kwani Unaweza kupoteza kibarua chako eti kisa mbususu ya kitoto Cha Form Four.
 
Walimu tafuteni pesa za kutosha mbona mabinti wamejaa tele mtaani hata bikra zipo nyingi tu,achaneni na wanafunzi mnaowafundisha mtakuja kuinamishwa bure kwa tamaa na ujinga wenu.
Labda ungewashauri waache Ngono,maana atakachotafuta mtaani,mwanafunzi pia anacho,maana huko mtaani pia kuna utaratibu wake,
 
Back
Top Bottom