Makamu mkuu wa SAUT na Wassira ndani ya Star tv wakijadili muswada wa sheria ya Katiba

Anasema Nyerere alikuwa na madaraka makubwa na alipenda madaraka hayo ili kuendeleza nchi,si kama viongozi wa sasa wana madaraka makubwa na wanayatumia vibaya
 
Anaongea wasira,anaulizwa umuhimu wa kuhairishwa muswada,yupo pia Felix Mkosamali
 
Wasira anasema msomi ni uwezo wa kuelewa mambo,anasema msomi kwenda upande mmoja ni kudanganya wananchi
 
Wasira kweli kazeeka huyu mzee,haeleweki anachoongea.....anasema muswada ulishawakilishwa kwa mara ya kwanza na anasema wananchi walishatoa maoni...yaani huyu mzee pumba tu
 
Anavyoonekana kweli huyu mzee anaweza kulala,mwandishi anauliza kwa nn wachangiaji wanajadili chadema badala ya muswada
 
Wasira anasema kujadili chadema si kosa kwa vile ni wanasiasa,sasa ni zamu ya mkosamali
 
Mkosamali anasema hawezi kukaa bungeni kwa kujadili kitu ambacho si halali,huyu mzee wasira cjui vipi anasema muswada ukishafika mezani ni tayari umesomwa mara ya kwanza
 
Anasema chadema wanasema eti wanawasemea wananchi na wakati wanaongelea mawazo yao wenyewe,hivi huyu mzee ana elimu gani?
 
mkosamali anasema ilibidi waanze na green paper,white paper halafu ndo mswaada.lakini wasira anasema huo utaratibu ni wakisheria eti unapoteza mda.akatoa mfano;chadema walisema wakati wa uchaguzi waliahidi watatengeneza katiba ndani ya siku 100.je kwa mtindo wanaoufanya si siku mia zingeisha bila la maana?anasema huu ni mswaada jinsi ya kukusanya maoni sio katiba.mia
 
Pls more updates,
Kiukweli nionavyo CCM walifikiri wangeweza kucheza rafu lakini sasa wanafikiria jinsi ya kuweza kuuondoa muswada huo na wabunge wao wasiwe mbongo.
Shame on CCM,
 
katika list ya wajinga nchii hii wasira ni nambari 2...

Hata huyo mtangazaji wa startv aliyemualika wassira studio kuzungumzia muswada wa katiba mpya atakuwa na matatizo.

Kwamba katika mawaziri wote wa JK wassira ndiye anaweza kuongea kitu substantive? wakati kila siku anatema pumba tu!
 
Wasira anasema muswada uliotafasiriwa ni ule ule uliowasilishwa mara ya kwanza,jamaa lina sura mbaya ,
 
Usiondoke sasa kwenye tv ili utujuze sisi wa madongo kuinama na mia yako aminia.
 
mkosamali anasema mswaada wa tarehe15/4/2011 ulikuwa wa kingereza na ulirudishwa wautafsiri kwa kiswahili.lakini baada ya kuutafsili wameleta kitu kingine kabisa tofauti na kile cha 15/4.so ilitakiwa wasome kwa mara ya kwanza kwa kuwa una mambo yanayotofautiana na ule wa mala ya kwanza ambao ulirudishwa utafsiriwe.lakini wasira anang'ang'ania mswaada ndo uleule eti hakuna kilicho haribika.anajihami kwa kusema eti mkosamali ametoka shule hivi karibuni asitake kuchanganya watu.mia
 
Back
Top Bottom