Makamu M/kiti BAVICHA taifa ni pandikizi au kapewa pesa haramu?

hivi nyie mashabiki wa chadema mmesoma shule za wapi!?bora mngekuwa wanachama mngeyajua haya,moja humjui kama ni kiongoz wa chama kwahy viongoz unawajua wale wa jukwaani tu!?hebu jaribu kufikir kwanin SHONZA kaongea vile,ni BAVICHA imekaa kikao na kutolea uamuz ambao umepewa baraka!kwa kuijadili kauli ya HECHE ambayo alikurupuka na kuifanza kauli ya BAVICHA..hili suala haliitaji elimu ni tafakuri tu,na hata kama unaipenda chadema jaribuni kuwa unahudhuria chaman ujue mambo yanayohusu chama chako na sio kupata magezitini
 
Nadhani watu wanazidisha huu moto bure. Watu wanatofautiana katika siasa kila kukicha. Hapa watu wanamshambulia Shonza kwamba katumwa au kapewa mlungula. Siyo kila anayetofautiana na wenzake chamani basi ametumwa. Hizi ni changamoto katika chama chochote cha siasa na hapo bado kuelekea mwaka 2015.
 
Hakuna shaka binti huyu kapata vidonge vyake na sasa anajutia kitendo chake! Sasa tumpe muda wa kujirudi na kuwa mpambanaji anayeitikia wito wa kamanda wake. Ametambua kuwa miluzi mingi hupoteza mbwa mawindoni.
 
Alichosema hukumuelewa? mbona ni simle and clear? Kauli ya Heche sio ya BAVICHA huo ndio upandikizi?

Nashangaa sana kwa nini mizizi ya maafisadi inamtetea huyu Binti, Kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.. Mwenyekiti wa CDM Taifa ndiyo msemaji mkuu wa Chama na kwa Upande wa Bavicha msemaji mkuu wa Bavicha ni mwenyekiti kwa sababu mjumbe yeyote anaweza kumpa maoni yake muda wowote na mwenyekiti akaona swala hili lina uzito akalitolea ufafanuzi... mfano ni swala la Nasari alipoteleza kule Arusha,,, Mbowe akatoa kauli kwa kufuta ile kauli ya Dogo Janja ma kutoa msimamo wa Chama alikaa kikao cha Halimashauri Kuu au cha wanacha gani kufanya vile? Mimi nafikiri huyu Binti na shibuda lao Mmoja tu au ana hofu fulani au na yeye ni miongoni mwa waropokaji ambao wanatakiwa watoke CDM na waende kwenye vile vyama vya waropokaji na si CDM.

Mimi namshangaa sana mtu ambaye anashabikia kauli ya Shibuda, Kama Shibuda anaitakia mema CDM atasemaje Hakuna Mtu ambaye anaweza kugomea na kushinda Nafasi ya Urais ndani ya CDM zaidi ya yeye? na Kampeni meneja lazima atoke CCM la sivyo hashindi?... Na kwa nini akaseme kwenye vikao vya CCM? Kama amefikia kusema yote aliyoyasema, je ni mangapi yanaendelea kisiri siri?.....

Anapokemewa mropokaji na mhujumu kama huyo wanajitokeza wehu wengine na kuanza kumtetea, embu huyo binti atoke kauli ya Bavicha, au alichokisema ndiyo kauli ya Bavicha?

Mimi nataka viongozi wa CDM waelewe hawa Vibaraka washughulikiwe mara mmoja na chama kisafishwe vizuri ... Next time tusi intertain hawa Vibaraka wa CCM fukuzeni mtu hata kama anaondoka na Mkoa mzima msijali hata kidogo kwani kwa hali ilivyo mtu mmoja hawezi kubadilisha maisha haya ya Mtanzania... Watu wana matumaini na CDM kwa maana ya Chama na Si mtu mmoja mmoja... Watanzania wanaelewa zaidi hata ya hao vibaraka kwa sasa zaidi ni hali yao ya maisha kubadilika na si kutoka kwa njia ya kugeuka kuwa Kupe au Mchwa kama huyu Binti wa Bavicha anavyofikiri...

Huyu Binti bado anaugua machungu ya Boy frend wake kukosa Umwenyeki kwa hiyo ana chuki binafsi na Heche..

NOTE: Heche ameungwa mkono na Wenyeviti wa Shinyanga, Arusha, Mwanza, Pwani etc....
 
Huyu dd sujui cdm imetokana naye wapi. hivi kwa busara za kiuongozi hata kama Heche alianza kukosea kwa hiyo naye akaona ni busara aendeleze kukosea kwa kuita press conf.........nadhani hapo kuna kitu nyuma ya pazia la huyu dada.

Tusimkawize apashwe ukweli wake kwenye kikao cha 24/05 ili ajifunze uongozi kama kweli tupo pamoja naye aombe radhi vinginevyo mlango upo wazi aende huko kwa mafisadi wanaomdanganya
 
Ninachoshukuru ni kwamba CDM ni chama cha watu na kinapiganiwa na watu na kina akiba ya wapenda mabadiliko wengi walio nje ya mfumo wa uongozi,hivyo kusafisha wale wote wanaotia mashaka katika uongozi wao sio tatizo hata kidogo,japo watu wanamtetea huyu M/Kiti lakini to honest ni akili gani ya kulipiza kosa kwa kosa,fine Heche kafanya kosa,na wewe msaidizi wake unaibuka unafanya kosa ambalo tayari limeshaonekana,hiyo ni upuuzi.lazima tuwe wakweli huyu dada kapandikizwa.na amejikoroga mtakuja kuona matokeo.
 
hakuna dada nisiyempenda kama shonza,ninamfahamu maana nimesoma nae na ndo maana kwenye uchaguzi niliwaambia watu wawe makini sana na huyu dada lkn hawakunisikia.Ni mnafiki sn ninafaham A-Z siyo shibuda aliyemtuma kuna kigogo mwenye matatizo kama yake ndani ya cdm ndo kam2ma kwa kumuogopa heche ktk mipango yake.Hivi alilolitamka heche linaubaya mpk kumpinga kupitia waandishi wa hbr? shonza ulipofikia sio mwisho wa ndooooto zako tutakutana kwenye uchaguzi.kila la kheri kamanda heche:A S embarassed::A S embarassed:
 
  • Thanks
Reactions: FJM
shibuda hana uwezo wa kuumiza mtu kichwa ila anajiumiza yeye mwenyewe kwa upumbavu wake uliokomaa...!!namuunga mkono Hofstede hili jamaa ni la kupuuza na BAVICHA wakae kimya kubishana na tahira na wewe utaonekanika tahira vilevile.
 
!
hivi nyie mashabiki wa chadema mmesoma shule za wapi!?bora mngekuwa wanachama mngeyajua haya,moja humjui kama ni kiongoz wa chama kwahy viongoz unawajua wale wa jukwaani tu!?hebu jaribu kufikir kwanin SHONZA kaongea vile,ni BAVICHA imekaa kikao na kutolea uamuz ambao umepewa baraka!kwa kuijadili kauli ya HECHE ambayo alikurupuka na kuifanza kauli ya BAVICHA..hili suala haliitaji elimu ni tafakuri tu,na hata kama unaipenda chadema jaribuni kuwa unahudhuria chaman ujue mambo yanayohusu chama chako na sio kupata magezitini
kwani wewe umesoma wapi!msemaji wa bavicha taifa ni mwenykit na sio makamu halafu acha kukurupuka kama SHONZA ni ndg yko kamtafute umweleze huo ugoro wko na si hapa jamvini ma****yako.
 
Woote wtatokea dirishani wlupoingilia.
Nilisema mwnzo kwamba tamko la BAVICHA was unnecessary!
Kwa Shibuda!!?? Kweli!!??

Hata mie nashangaa sana, Shibuda c wa kuhangaisha watu, hata Heche mwenyewe mkurupukaji hakuwa na sababu ya kutoa tamko lolote at first place
 
Wote humu ndani tulio CDM na Magamba wanajua kuwa Shibuda ni mropokaji tu hivyo kulikuwa hakuna sababu yoyote ya kumjibu kwani ndo anachokitaka kuwapumbaza wapambanaji wa kweli. BAVICHA watch out, achaneni na kutoa matamko kama kuna tatizo andaeni mashitaka na kuyapeleka kunakohusika.
 
Makamu mwenyekiti hajakosea kitu bali amejaribu kuona hata kama watasawazisha hilo swala ndani ya vikao itakua ni kwa upande mmoja kwani kauli imetolewa kwa umma na umma itabaki na kauli ya Heche kama kauli ya BAVICHA so ili kutopotosha umma na kuweka mambo sawa lazima alitakiwa kupinga au mlitigemea heche ndo arudi na kusema kauli haikua ya BAVICHA mbona Mbowe hakusubiri kikao cha ndani ili afute kauli ya Nassari badala yake aliifuta mbele ya umma na kusema sio msimamao wa chama.

ukweli ni huu kauli ya Makamu mwenyekiti imetoka kwa wakuu ili kuisafisha Bavicha kwa roho safi na sio kumjibu mtu.

nawasilisha
 
Juliana Shonza angetoka kinamna nyingine lakini alivvyotoka kudharilisha Bavicha amejipaka mavi usoni sijui atafuta kwa sabuni gani nadhani kama hajui kuwa wananchi wamekuwa overprotective juu ya chadema basi hafai kuwa Makamu Mwenyekiti kuna idadi kubwa sana ya wananchi ambao ni loose allie wa chadema zaidi ya wale wenye kadi hawa ni wale wasiopenda kuona mtu kwa namna yeyote ile anachelewesha mabadiliko

Wakati wa uchaguzi wao kuna uzi ulipita hapa kuwa alikuwa amepandikizwa na mimi naamini sasa ni pandikizi lisilo na akili angetumia forum nyingine sio hii ya mpuuzi shibuda Kumsafisha mtu amekuwa akidhalirisha chama mara zote halafu yee anajitokeza bila aibu kwamba ni mpambe wake, mwanamke amejishusha hadhi Kuonekana anamlinda pandikizi Shibuda asiestahili kujadiliwa hata na panya
Nafikiri ni vizuri zaidi ungemshauri kuwa once Mwenyekiti akishatoa kauli, basi busara kusubiri kikao kumshauri Mwenyekiti wake kuwa ni vizuri kabla ya kutoa tamko wahauriane namna ya kuenda public.Ni bahati mbaya waandishi wa habari wa Tanzania si wajuzi wa kujenga mshikamano wanapenda uandishi wa kuchonganisha na kuleta migogoro ili auze habari yake especially yakihusu watu maarufu.Huyu binti nilipata habari zake aliposhiriki uchaguzi mdogo wa diwani wa Kiwira na mzaliwa wa eneo la forest Jiji la Mbeya.
 
Makamu mwenyekiti hajakosea kitu bali amejaribu kuona hata kama watasawazisha hilo swala ndani ya vikao itakua ni kwa upande mmoja kwani kauli imetolewa kwa umma na umma itabaki na kauli ya Heche kama kauli ya BAVICHA so ili kutopotosha umma na kuweka mambo sawa lazima alitakiwa kupinga au mlitigemea heche ndo arudi na kusema kauli haikua ya BAVICHA mbona Mbowe hakusubiri kikao cha ndani ili afute kauli ya Nassari badala yake aliifuta mbele ya umma na kusema sio msimamao wa chama.

ukweli ni huu kauli ya Makamu mwenyekiti imetoka kwa wakuu ili kuisafisha Bavicha kwa roho safi na sio kumjibu mtu.

nawasilisha

Kibaraka wa Shibuda at work
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom