Inanambo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2011
- 3,985
- 2,770
Kuna tabia ya wizi na unyonyaji wa jasho la vijana wetu wanaopata kibarua kwenye kampuni za usafi. Kampuni hizi zilianza kutoa huduma ya usafi, Chakula na ulinzi katika taasisi mbali mbali baada ya kuondoa ajira ya Mesenja.Huajiri vijana kufanya usafi wa choo, nje na ndani ya majengo. Vijana hujituma kufanya kazi lakini huishia kulipwa 80000 hadi 100000 kwa mwezi.
Hawalipwi nauli wala chai au lunch ni kujitegemea. Huu ujira ni kidogo sana ukilinganisha na kazi vijana wanazofanya. Waajiri wao huwatumikisha tangu jumatatu saa 11:30 asubuhi -10:30 jioni hadi Jumamosi. Wakidai ujira zaidi wanafukuzwa. Ni haki kumlipa mtu elfu 3 kwa siku? Vyama vya wàfanyakazi mko wapi? Fuatilieni Unyonyaji huu.