Kujua kuwa watu wanakufa kwenye nchi nyingene nimejua kupitia vyombo vya habari mfano equado na brazil watu wamekufa sana, ninavyo elewa hii ni miradi ya watu ambao wanataka watajilike kupitia ugonjwa huu, kama vitendea kazi wanatupa wao posibility ya kuweka corona kwenye vifaa nikubwa so watu wanaweza wakawa wanaambukizwa kipindi wanavyo pima Me siamini kama JMP ni mjinga kiasi hicho
Wangonjwa wa corona tz wapo ila kuendelea kutoa takwimu hofu inaongezeka so me kama church boy maandiko yananiambia hofu huleta giza kwaiyo hatuwezi tukamuacha giza (corona) aendele kutawala kama tulimwomba Mungu tuamini ivyo ivyo Mungu katuponya
Kujifungia ndani au paricial lockdown ni ukichaa kwani corona ipo usiku pikee yake, taadhali ni muhimu sana so sio kila kitu tu copy na ku pest kwenye nchi yetu kila mtu anambinu zake kama USA wamejitoa WHO maana yake hawafuati maelezo yao sisi ni nani tuendelee kushilia non sense toka kwao
Mkuu nchi zote zinatangaza takwimu za ugonjwa kwa maana njema tu ya kujiweka katika namna nzuri zaidi ya kupambana nao.
Habari za Ecuador na Brazil ulizosikia kwenye vyombo vya habari asili yake (source) ni takwimu tokea katika serikali husika.
Kwamba takwimu zinaleta hofu? Si kuwa takwimu zinawafanya watu kuchukua tahadhari zaidi?
Fikiria, eneo fulani kuna hatari ya simba anayezagaa huru. Wewe unaona ni vyema unyimwe taarifa hiyo ili ukakutane naye ana kwa ana tu huko huko bila taarifa yoyote?
Kwamba kuna miradi ya watu ili watajirike kupitia ugonjwa huu?
Mkuu haipo nchi hata moja duniani yenye mawazo kama haya. Zipo jumla ya nchi takribani 195 duniani. Ni Tanzania tu ndiyo imestukia huo mchezo kuwa kuna watu tu wanashadadia huu ugonjwa ili kutajirika? Kama hivyo ni kweli hao unaowasikia kuwa kweli wanakufa huko Ecuador na Brazil tena inakuwa vipi?
Kuwa aliyestukia kuwa hili ni dili la utajiri, kwa hiyo ina maana mlengwa au mwathirika wa dili hilo ni Tanzania peke yake? Kwa uchumi upi?
Mengi unayoyasikia ni mbwembwe tu kujaribu kuficha takwimu. Tuliowapa dhamana wanajua kuwa hatuko katika njia salama wala sahihi. Takwimu ilikuwa muhimu kujua tuelekee wapi kibaya ni kuwa haiyumkiniki wakizitoa wanaogopa kuwa zitawaumbua.
Misahafu inasema, "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa."
Zaidi pia, imeandikwa tusimjaribu bwana Mungu wetu!