Makampuni ya simu yapigwa faini kwa kukiuka

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
6,562
11,083
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde amebaini kuwepo kwa wafanyakazi wa kigeni, walioletwa na kampuni za simu za mkononi kufanya kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania ikiwemo kufunga meza na viti vya kukalia.


Aidha, amebaini kuwepo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya simu ya Halotel, raia wa Vietnam, ambao wanaishi nchini bila kibali cha kazi wala cha kuishi. Mavunde aliyabaini hayo jana wakati alipofanya ziara ya kukagua vibali vya ajira kwa wageni, baada ya tangazo lililotolewa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama.


Akiwa katika kampuni hiyo ya Halotel, Mavunde alibaini kuwepo kwa baadhi ya mapungufu, ikiwemo baadhi ya wafanyakazi kutopewa mikataba ya ajira na wenye ajira kutopewa nakala za mikataba yao.


Mavunde aliagiza viongozi wa kampuni hiyo, kuhakikisha kufikia leo wafanyakazi wote wanapewa mikataba huku nakala za mikataba hiyo, ikipelekwa ofisini kwake na pia kuwataka kulipa madeni ya wafanyakazi, hasa madereva, ya saa za ziada (overtime) haraka iwezekanavyo.


“Tumegundua kuwepo kwa mapungufu mengi katika kampuni yenu, hii ni pamoja na wafanyakazi wenu kutojiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kumekuwa na makato ambayo hayapo kwa mujibu wa sheria za kazi.


"Lakini pia kuna wageni ambao wako katika hii kampuni yenu, wanafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania, kwa mfano huyu anayefunga viti, hii kazi inafanywa na vijana wetu…kibali chake kinaisha kesho, naagiza asipewe kingine na aondoke,” alisema Mavunde.


Aidha, alisema katika masuala ya usalama mahali pa kazi, pia kuna mapungufu mbalimbali, ikiwemo wafanyakazi kutopewa mafunzo ya kukabiliana na majanga, vipimo vya afya na makosa mengine ambapo kwa mujibu wa sheria aliwatoza faini ya Sh milioni sita.


Hata hivyo, wakati akiendelea kutoa maagizo hayo, mmoja wa maofisa wa Ubalozi wa Vietnam, Mai Anh Thai aliingia katika ukumbi wa mkutano na kutaka kumkatisha Naibu Waziri kwa madai kuwa hakufuata utaratibu.


Kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa huko, ilimlazimu Mshauri wa kampuni hiyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, kumshauri ofisa huyo taratibu za ukaguzi zilivyo.


Baada ya kutoka katika kampuni hiyo, Mavunde na maofisa wa Uhamiaji, Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana na askari walilazimika kufika katika nyumba ambayo iko Mikocheni, ambako inasadikiwa kuwa wapo raia wengi wa Vietnam wanaoishi hapo, huku wengine wakiwa hawana vibali vya kuishi wala vya kazi.


Walipofanya msako katika nyumba hiyo, baadhi ya raia hao walijificha na kufanikiwa kumkamata mmoja ambaye hakuwa na kibali chochote. Hata hivyo, mmoja wa walinzi wa nyumba hiyo alisema raia hao walikuwa wengi, lakini baadhi yao walitoroshwa juzi usiku.


Awali akiwa katika Kampuni ya Airtel, Mavunde aliwapiga faini ya Sh milioni nne kutokana na kuwepo na mapungufu mbalimbali katika masuala ya usalama na afya mahali pa kazi, ambazo wanapaswa kulipa ndani ya siku 14.


Aidha, aliwataka waajiri nchini kote, kuhakikisha wanasimamia sheria za kazi ili kujenga nchi ambayo haina misuguano. Mavunde alionya kuwa wanaobeza kuwa hiyo ni ‘nguvu ya soda’, wafute jambo hilo, kwani kazi hiyo ni endelevu.

MYTAKE:
1. Hii kampuni ya halotel ni bonge la jipu, wabanwe wafuate sheria za nchi hii.

2. Nchi inapoteza mapato mengi sana kwenye makampuni ya simu serikali ichukue hatua kutumbua jipu hili...

UPDATES:
Muda huu 11:20am yupo tigo/huawei anakagua.....
 
Last edited:
Duh hii nchi ilipokuwa imefikia simchezo,hili soko huria ni zaidi ya ushenzi kwa waafrika,hawa jamaa kwenye nchi zao hata kuuza biscut hawakuruhusu kabisa wala raia wao wanakuwa wakwanza kutoa taarifa,lakini hapa kwetu huwezi kulaumu raia maana hawana meno ,hawa jamaa wanaofanya kazi za local wanabaraka zote za mamlaka zetu husika
leo wachina ,wahindi ,wavietnam ndio wamehamia hapa kwa kazi amabazo tunaweza fanya wenyewe,hatuchukii wageni lakini tunataka utaratibu ufatwe na lazima wizara ya kazi ilinde ajira za local haiwezekani mchina anakuja kuanzisha kampuni ya kufyatua tofali mitaani na tuseme soko huria
 
Halotel waliletwa na Mizengo Pinda pamoja na January Makamba...hao ndio wawe wakwanza kuchukuliwa hatua kwa kuleta matapeli
Tafadhali elewa kwanza kasha ndio u comment. Lengo la kuwaleta hawa wawekezaji lilikuwa very positive, yaani kuwekeza katika huduma za mawasiliano ili Serikali ipate kodi. tatizo lilipo ni Idara yetu (Idara ya kazi) kushindwa kusimamia kikamilifu sharia ya kazi na kanuni zake na hayo ndiyo matokeo. Ifike hatua kwamba kila mtanzania awe na uchungu na nchi yake au maslahi yake binafsi kuliko kujali wageni ambao kama ulivyosikia wanafanya kazi ambazo wadogo zetu wa vijijini wasio na elimu wangefanya kubeba viti na meza
 
Kutoka Vietnam hadi kuishi Mikocheni na kufanya kazi nchini.Afisa ubalozi anamkatiza naibu waziri kwamba hajafuata utaratibu.Jiulize hiyo jeuri wanatoa wapi?.Eti tuna serikali?!!
 
Hawa Mwaziri hawana Job descriptions

si ajabu kumkuta one day anafanya kazi za makarani
 
Waende voda , Tigo na Airtel huko ndugu zetu wanavyo teseka kwenye ma call center yao
 
Hili la mikataba ni tatizo kuubwa sana, kuna jamaa niliona kashika mkataba wake ni aibu. Mkataba ni page moja alafu kampuni kubwa kichizi, humo ndani kuna mambo kibao anayostahili apewe lakini hayajaandikwa na hayapo, wengine mikataba ni kama mali ya mwajiri huku mwajiriwa akinyimwa kopi. Maeneo yaliyokubuhu ni mahoteli, vyuo binafsi, shule binafsi, hospitali binafsi n.k. Huku waajiri wamegeuka wanyonyaji waliokubuhu na mh. Mavunde aende kote huko tena amalize dar kwanza ndo waajiri wanajifanya wajuaji.
 
Kutoka Vietnam hadi kuishi Mikocheni na kufanya kazi nchini.Afisa ubalozi anamkatiza naibu waziri kwamba hajafuata utaratibu.Jiulize hiyo jeuri wanatoa wapi?.Eti tuna serikali?!!

Nashangaa hapo afisa Ubalozi anataka kumuelekeza taratibu za kufanya waziri kwenye nchi yake, hiki ni kiburi kilichopitiliza, ingekua enzi za Mzee aaah huyo jamaa na kinga yake angekiona cha mtema kuni
 
Hivi kweli Naibu Waziri ndiye anayetambua uwepo wa wafanyakazi wa kigeni wasio na vibali vya kufanya kazi nchini? Au malimbikizo ya malipo na overtime kwa wafanyakazi wa kampuni binafsi ya simu? Au mazingira hatarishi ya simu? Hapa kuna tatizo kubwa. Hali tunayoiona sasa ni ishara kuwa taasisi za serikali/regulators zimelala kabisa.
 
Kutoka Vietnam hadi kuishi Mikocheni na kufanya kazi nchini.Afisa ubalozi anamkatiza naibu waziri kwamba hajafuata utaratibu.Jiulize hiyo jeuri wanatoa wapi?.Eti tuna serikali?!!

Mkuu jipukubwa huyo Afisa wa ubalozi wa Vietnam aliyekuwa akimzuia naibu waziri halali wa nchi kufanya kazi zake bado yuko huru au yupo mahabusu anasubiria kupandishwa kizimbani? Na polisi si Inaonekana walikuwepo kwenye msafara wa uukaguzi wa Mh.Naibu Waziri? Si inafahamika Kisheria ni kosa kumzuia m2 esp.mwenye mamlaka kama waziri ku2ekeleza majukumu yake? Na huyo ni raia wa nje.Au wanasheria wasomi sheria inasemaje hapa?
 
Halotel waliletwa na Mizengo Pinda pamoja na January Makamba...hao ndio wawe wakwanza kuchukuliwa hatua kwa kuleta matapeli
Aiseeee
ImageUploadedByJamiiForums1451456783.020112.jpg
 
Hivi kweli Naibu Waziri ndiye anayetambua uwepo wa wafanyakazi wa kigeni wasio na vibali vya kufanya kazi nchini? Au malimbikizo ya malipo na overtime kwa wafanyakazi wa kampuni binafsi ya simu? Au mazingira hatarishi ya simu? Hapa kuna tatizo kubwa. Hali tunayoiona sasa ni ishara kuwa taasisi za serikali/regulators zimelala kabisa.
Hapa sasa ndo utaona kwanini Rais au mawaziri wanafanya ziara zao za kushtukiza....

Mi nawasiwasi pia kama tupo salama Maana kama mtandao wamilikiwa na jeshi la Vietnam. Je hatuchunguzwi
 
Back
Top Bottom