Makampuni ya simu yanatutapeli.

Vawulence

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
1,928
2,101
Imekuwa ni kawaida kwa makampuni mbalimbali ya simu kujinadi kuwa wao peke ndio waliofika kila kona ya nchi. Nilifunga safari ya kwenda Semunge kwa babu ila katika siku 3 nilizoishi kule sikufanikiwa kupata mawasiliano ya mtandao wowote ule. Hii ni sehemu moja tu kati ya nyingi tusizozifahamu kuwa na shida ya namna hii. Kujinadi ni jambo moja ila kujinadi kitapeli ni jambo lingine. Hakuna jinsi yoyote ile ya kujinadi bila kudanganya wajeja wenu? Uongo wenu unatugharimu sana kwani unatukwamisha mambo mengi ya msingi. Kuna mambo mengi ya kitapeli kama vile makato ya muda wa maongezi yasiyoeleweka bila maelezo.
 
duh! Ila ilikuwa shughuli hasa kwa wale walioachwa na magari na huku hawawezi kuwasiliana na ndugu zao walioko duniani.
 
Imekuwa ni kawaida kwa makampuni mbalimbali ya simu kujinadi kuwa wao peke ndio waliofika kila kona ya nchi. Nilifunga safari ya kwenda Semunge kwa babu ila katika siku 3 nilizoishi kule sikufanikiwa kupata mawasiliano ya mtandao wowote ule. Hii ni sehemu moja tu kati ya nyingi tusizozifahamu kuwa na shida ya namna hii. Kujinadi ni jambo moja ila kujinadi kitapeli ni jambo lingine. Hakuna jinsi yoyote ile ya kujinadi bila kudanganya wajeja wenu? Uongo wenu unatugharimu sana kwani unatukwamisha mambo mengi ya msingi. Kuna mambo mengi ya kitapeli kama vile makato ya muda wa maongezi yasiyoeleweka bila maelezo.

Mkuu unamatatizo gani?
Pole, vipi khali yako baada ya kikombe?
 
Mkuu.

Unashangaa ya makampuni ya simu? serikali inapowatapeli wananchi wake utasema nini?
sasa Jiulize je utapeli haufanywi hapa TZ?
Malipo ya DOWANS? Sio utapeli ?na inapigiwa debe kuliko yanavyofanya hayo makampuni ya simu?
Umeme wa dharuka kila mwaka......huu sio utapeli?

Mkuu...tuna safari ya maili 1000 kwa mguu!
 
ila kweli mkuu

Huu ni zaidi ya utapeli bali ni udanganyifu, kwa sababu wanatudanganya kuwa waemenea kila kona ya Tanzania. Unaposafiri bila kujipanga kama yaliyokukuta huko kwa babu unakuta mambo yako yanakwama.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom