Makampuni ya huduma za mawasiliano yamejikuta yakijisahau kabisa katka suala zima la costumer care

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
2,658
2,804
Naomba salami hizi ziwafikie vodacom Tanzania na mitandao mingine ya simu.

Katika Siku za hivi karibuni haya makampuni ya huduma za mawasiliano yamejikuta yakijisahau kabisa katka suala zima la costumer care kiasi hadi kufikia kuondoa huduma ya kuzungumza moja kwa moja na muhudumu wa huduma kwa wateja.

Unaweza ukapatwa na shida na unataka kupata ufumbuzi wa kina,ukipiga namba zao za huduma kwa wateja ,wanakuunganisha na huduma za ujumbe was sauti.

Kwa hakika ,vodacom na mitandao mingine kwa hili mnatukosea sana ,na hii inatokana na hulka ya ubahili waliyonayo haya makampuni katika kutia ajira za watu was huduma kwa wateja.

Ukipiga no yao ya huduma kwa wateja hadi ufike kuungwanishwa na mtoa huduma hiyo unaweza ukajipata umeshasahau kabisa shida yako.

Tunawataka vodacom Tanzania na mitandao mingine mbadilike haraka katika hili,la sivyo nitaenda kufungua kesi mahakamani kwa huu ujinga mnaoufanya
 
Wanazingua vibaya sana, kina huduma muhimu sifanyi na Voda, ukipata shida ya dharura imekula kwako aisee
 
Now nimegundua njia rahisi ya kuwapata ,unapiga number yao then chagua 5,chagua 3,ndio utawapata kirahisi
 
Back
Top Bottom