Makampuni haya ya Simu yanapimana Msuli na Rais. Dr Magufuli...

LAZIMA NISEME

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
232
260
Mpaka jana tarehe 30.7.2017 ni Makampuni matatu ya Mawasiliano pekee ndiyo hayajaonesha Ushirikiano wa kujiunga katika Mfumo wa kulipa kodi Kielekroniki kama Rais wa Tanzania Dr. Magufuli alivyo agiza mapema mwezi Juni Mwaka huu.

Makampuni ambayo yameshajiunga Katika Mfumo huu wa kulipa Kodi kielekroniki ni:-
  • Kampuni ya TTCL ambao wamesha kamilisha taratibu zote za kujiunga kwa asilimia 100% na tayari taarifa zao za Mapato zimekuwa zikipokelewa kuanzia mwezi wa sita,
  • Mtandao wa Halotel nao pia wamekamilisha kujiunga kwa asilimia 100% na tayari taarifa zao za Mapato zimekuwa zikiendelea kupokelewa tangia mwezi wa sita.

Kampuni nyingine ambazo zimesha jiunga Katika Mfumo huo kuwa ni:-
  • Kampuni ya simu za mkononi ya Smart ambayo imesha kamilisha hatua kwa kiwango cha asilimia 85%,
  • kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa asilimia 35% na
  • kampuni ya simu za mkononi ya tiGO kwa ailimia 65%.

Makampuni ya mawasilano
ambayo mpaka kufikia jana bado hawajatii amri ya mheshimiwa Rais Dr. Magufuli kama alivyoagiza wakati wa uzinduzi wa Mfumo huo kwamba makampuni yote ya simu ni lazima yaunganishwe kwenye dirisha hilo, yaani Mfumo wa kukusanya Kodi Kielekroniki (e-RCS) kabla ya mwezi wa nane ni:-.
  • Vodacom 0%,
  • Zantel 0.5% na
  • Smile 0%
Aidha Tulipo taka kupata undani wa ni kwanini kampuni za simu za Vodacom, Zantel na Smile hawajajiunga Katika Mfumo huu hatukupata ushirikiano kutoka kwa wahusika.

Hata hivyo, Kwa mujibu wa Barua yenye kumbukumbu Namba TMNOA/TRA/2017/L001 ya tarehe 28 Julai 2017, kutoka kwa “TAMNOA” ( Umoja wa Makampuni ya Simu Tanzania) iliyosainiwa na Mkurugenzi mkuu wa Vodacom Bw. Ian Feraro kama Mwenyekiti wa Umoja huo kwenda kwa Kamishona wa walipa kodi wakubwa TRA, inaelekeza kwamba watakuwa na kikao kitakacho jadili na kuamua jinsi watakavyo jiunga kwenye Mfumo huo. Hadi sasa hivi hawajaamua kujiunga katika mfumo wa e-RCS.

Hata hivyo barua hiyo haikutaja wala kusainiwa na kampuni yeyote ya Simu iliyo katika umoja wa TAMNOA, Jambo linaloashiria kwamba umoja huo haupo wala hautambuliwi na TRA kama mlipa kodi aliyesajiliwa.

e-RCS ni mfumo uliotengenezwa na wataalam wa ndani ya Serikali kutoka Taasisi mbalimbali za serikali zikisaidiana kwa karibu na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).
 

Attachments

  • 1.png
    1.png
    256 KB · Views: 83
  • 2TAARIFA YA MAKAMPUNI.jpg
    2TAARIFA YA MAKAMPUNI.jpg
    84.3 KB · Views: 90
  • 3 TAMNOA BARUA.jpg
    3 TAMNOA BARUA.jpg
    57 KB · Views: 93
  • 4.jpg
    4.jpg
    40.6 KB · Views: 81
Serikali ya awamu ya tano iliishasema haijaribiwa!!
 
Hao Vodacom ndio wenye hela ya maana.
Wajiunge tu tuchukue kodi yetu.
 
Hawa nao wapewe siku 14 kama wauza mafuta vinginevyo miambo izimwe,utaona watakavyomaliza fasta tu
 
Hivi mwisho wa siku 14 ni kesho? Vituo lukuki mikoani havijafungwa hizo mashine
Kama havijafungwa ni sababu za Mkandarasi lakini toka wiki iliyopita wauzaji wote wa mafuta walikwisha lipa hela ya kufunga hizo mashine...hivyo hakuna mgogoro tena na serikali bali ni mkandarasi mwenyewe ndio kazi ni kwake
 
Kama havijafungwa ni sababu za Mkandarasi lakini toka wiki iliyopita wauzaji wote wa mafuta walikwisha lipa hela ya kufunga hizo mashine...hivyo hakuna mgogoro tena na serikali bali ni mkandarasi mwenyewe ndio kazi ni kwake
Safi sana kma ni hivyo itakuwa mkandarasi ypo kwenye mchakato wa kuvileta kla ktu knawezekana ukiwa seriously

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pendo/Aneth/smart team
Smart wamefanya tena uhuni wao wamechukua hela zote zangu na kuniacha na zero,hawa watu ni kawaida yao na nilikuambia na kweli imetokea.Wametufanyia huu uhuni mara nyingi kesho taripoti TCRA waone huu wizi wanaofanya.kifurushi kikiisha hakuna notification,huwezi kujua balance na mengineyo.Ngoja tuone mwisho wake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom