Makampuni 49 ya Tanzania yaruhusiwa kuuza maharage soya China

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Ubalozi wa China nchini Tanzania umetangaza makampuni 49 ya Tanzania yaliyoruhusiwa kuuza maharage soya nchini China.

Hatua hiyo ya Mamlaka ya forodha kuruhusu maharage soya ni fursa kwa wakulima wa Tanzania kwa kuwa sasa wana soko la uhakika.

1624087702561.png

1624087751577.png
 
Tusiache kulima mahindi na kuhamia kwenye soya kwa kasi kwa kufanya hivyo tutaweza kulisha mifugo na sisi kukosa menu...

Anyway hio ndio hali halisi ya dunia hii iliyokaa kichwa chini miguu juu...
 
Tusiacha kulima mahindi na kuhamia kwenye soya kwa kasi kwa kufanya hivyo tutaweza kulisha mifugo na sisi kukosa menu...

Anyway hio ndio hali halisi ya dunia hii iliyokaa kichwa chini miguu juu...
Ndugu watu wanaangalia wapi watafaidika kwa jasho lao, huwezi kutumia resources kwenye kitu kisicholipa kama mahindi. Inaleta mantiki ikiwa utapeleka sehemu kubwa ya nyenzo za uzalishaji kwenye kitu kinacholipa, yaani punguza kuzalisha mahindi ongeza kuzalisha soya.
 
“Only when the last tree has been cut down, the last fish been caught, and the last stream poisoned, will we realize we cannot eat money.”
 
Misemo ya wazungu hio.

Wakulima wanataka pesa tu mifukoni mwao.

Ubalozi wa China nchini Tanzania umetangaza makampuni 49 ya Tanzania yaliyoruhusiwa kuuza maharage soya nchini China

Hatua hiyo ya Mamlaka ya forodha kuruhusu maharage soya ni fursa kwa wakulima wa Tanzania kwa kuwa sasa wana soko la uhakika
Usihofu mkuu, kilimo cha maharage na mahindi kinaweza kufanya kwa mazao yote kulimwa kwenye shamba moja sambamba kwa wakati mmoja.mkulima anaweza kupata mahindi na akavuna pesa zake kenye soya...cha msingi azingatie spacing na ushauri wa kitaalam wambegu, mbolea na rotuba ya sehemu husika.
Japo sio mtaalam wa kilimo.
 
Misemo ya wazungu hio.

Wakulima wanataka pesa tu mifukoni mwao.
Ili hio pesa waifanyie nini...,

We live in a Closed System kama kukiwa na uhaba wa mahindi kutokana na upungufu wa kilimo cha mahindi mahindi hayo yatapanda bei kupelekea hizo pesa walizopata kutokukidhi haja. Mwisho wa siku unaweza kujikuta mkulima anapewa ruzuku ili kulima hayo mahindi, ambayo itapelekea kodi zetu kutumika huko.

By the way Kama Red Indians nao ni wazungu hapo sawa..., sababu msemo huu walikuwa wanawaambia wazungu (wanaoharibu mazingira)

Anyway sio kwamba ninalaumu ndio maana nikasema ni hali halisi ya hii dunia iliyokaa kichwa chini miguu juu (Most things we do, don't make sense)
 
Ubalozi wa China nchini Tanzania umetangaza makampuni 49 ya Tanzania yaliyoruhusiwa kuuza maharage soya nchini China

Hatua hiyo ya Mamlaka ya forodha kuruhusu maharage soya ni fursa kwa wakulima wa Tanzania kwa kuwa sasa wana soko la uhakika
Unaweza yataja?
 
Ili hio pesa waifanyie nini...,

We live in a Closed System kama kukiwa na uhaba wa mahindi kutokana na upungufu wa kilimo cha mahindi mahindi hayo yatapanda bei kupelekea hizo pesa walizopata kutokukidhi haja. Mwisho wa siku unaweza kujikuta mkulima anapewa ruzuku ili kulima hayo mahindi, ambayo itapelekea kodi zetu kutumika huko.

By the way Kama Red Indians nao ni wazungu hapo sawa..., sababu msemo huu walikuwa wanawaambia wazungu (wanaoharibu mazingira)

Anyway sio kwamba ninalaumu ndio maana nikasema ni hali halisi ya hii dunia iliyokaa kichwa chini miguu juu (Most things we do, don't make sense)
Ndugu umeibua mada nyingine tena. Nimekuwa nikiangalia makala mbalimbali za video na nimeona kuna ukinzani wa hoja kwa watu wanaotamani kuishi maisha yanayoshabihiana na mazingira asili na watu waliochagua kuishi maisha ya ustaarabu wa kisasa, maisha ya mjini yanayotegemea bidhaa mbalimbali za kununuliwa ambazo zinatokana na kubadili/kuharibu mazingira asilia.

Ubaya ni kwamba primitive civilization ilipunguzwa nguvu na kuonekana kwamba 'haifai' ili kuingiza mfumo mpya wa maisha uliosababishwa na mapinduzi ya viwanda. Na hii ndio modern civilization ambayo watu wengi wanaipenda, wanatoka vijijini kwenye maisha ya asili na kwenda mjini kwenye maisha ya 'uharibifu' ya kisasa.

Wengi wetu tunatamani kuishi kwenye nyumba ya kisasa, gari nzuri, kusoma elimu inayosaidia kukidhi na kukuza modern civilization n.k; yote haya yanahitaji pesa na kwa kuwa mtindo wa maisha umebadilika si wa kale tena basi yatupasa kufanya shughuli inayoleta mantiki kiuchumi.
 
Indeed kwa sasa civilisation imeleta maendeleo ambayo kwa population ya sasa isingewezekana kabla..., watu wanaishi zaidi na kupata their wants (wants sio needs) kwa urahisi zaidi....

Ila maisha haya sio sustainable..., bila kujifunza kuishi sustainably na mazingira yetu binadamu as a specie tutakuwa extinct na kabla ya kuwa extinct tutawaachia next generation milima ya wastes na mabaki ya pollution

Ila kama ulivyosema hii ni mada ya uwekezaji, kwahio hapa its all about monetary profits no matter the consequences....
 
Ili hio pesa waifanyie nini...,

We live in a Closed System kama kukiwa na uhaba wa mahindi kutokana na upungufu wa kilimo cha mahindi mahindi hayo yatapanda bei kupelekea hizo pesa walizopata kutokukidhi haja. Mwisho wa siku unaweza kujikuta mkulima anapewa ruzuku ili kulima hayo mahindi, ambayo itapelekea kodi zetu kutumika huko.

By the way Kama Red Indians nao ni wazungu hapo sawa..., sababu msemo huu walikuwa wanawaambia wazungu (wanaoharibu mazingira)

Anyway sio kwamba ninalaumu ndio maana nikasema ni hali halisi ya hii dunia iliyokaa kichwa chini miguu juu (Most things we do, don't make sense)
Maneno meeeeeeeeengi,cha msingi pesa mkononi.Full stop
 
Ziko wapi hizo kampuni watu tuzame mashambani.
Kama kuna soko la uhakika mbona watazishindwa soya.
Tupeane koneksheni basi
 
Habari yako iko robo tu.
Ungetaja hayo makampuni na anauani zake ili tuwasiliane nazo
 
Back
Top Bottom