Makamishna wastaafu wa Polisi wataka jamii iwatumie kwa ushauri, pia wako tayari kutangaza utalii

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
39,999
2,000
Makamishna wastaafu wa jeshi la polisi wamesema kupitia umoja wao wako tayari kuitumikia jamii kwa kutoa ushauri na kutumia elimu yao kuisaidia jamii.

Kamishna mstaafu Mohamed Mpinga amesema jamii isisite kuwaendea kwa ushauri popote walipo.

Naye kamishna mstaafu Jamal Rwambo ameiomba serikali iwatumie katika kuutangaza utalii wa nchi yetu.

Umoja wa makamishna wastaafu wa jeshi la polisi ulitembelea familia ya hayati Moringe Sokoine na kuzuru kaburi lake.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
 
chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,297
2,000
Mnoooo . Watulie ni wakati wa kuisogelea foleni ya kuhesabiwa.

Hapo ndio napompendea Mungu, fanya ubabe , dhulma na uonevu lakini muda utafika utasinyaa na kuzeeka nguvu zitaisha. Vyeo na mamlaka vitakaliwa na wengine wale waliokuwa wanyonge na watu wa kawaida ambao walikuaa hawaruhusiwi na ma-ps kumfikia mwenye mamlaka ndio watarudi kuwa rafiki na jirani wa kweli.

Wenye mamlaka wa wakati huo huja msibani kusaini kitabu na pole ya vijipesa na kuwahi kuondoka wakisema wanamajukumu mengi na misiba huachiwa wasio na lolote na ndio wanamsitiri marehemu aliyekuwa na kibri kwa hao wanyonge.

Hili ni fumbo kubwa sana la Imani.

Watulie hao makamishna
Damu na dhulma za wanyonge zinawalilia.
 
MoseKing

JF-Expert Member
Jul 5, 2017
1,632
2,000
Nashindwa kuelewa jamii itake ushauri gani kwa makamishna wastaafu, wakati wananchi walikuwa wanatendewa sivyo na wao wakiwa kazini wameshindwa kuliona hilo. Sasa wataishauri vipi jamii?
Hapo ni Njaaaaaaaaa imewapiga, wanatafuta namna watoke vipi ???

Nchi hii unafanya kazi mpaka unastaafu ukiwa na hali ngumu sanaaa kiuchumi hata kama ulikuwa na nafasi kubwa.
 
kurlzawa

JF-Expert Member
Jan 23, 2018
13,242
2,000
Makamishna wastaafu wa jeshi la polisi wamesema kupitia umoja wao wako tayari kuitumikia jamii kwa kutoa ushauri na kutumia elimu yao kuisaidia jamii.

Kamishna mstaafu Mohamed Mpinga amesema jamii isisite kuwaendea kwa ushauri popote walipo.

Naye kamishna mstaafu Jamal Rwambo ameiomba serikali iwatumie katika kuutangaza utalii wa nchi yetu.

Umoja wa makamishna wastaafu wa jeshi la polisi ulitembelea familia ya hayati Moringe Sokoine na kuzuru kaburi lake.

Source Star tv

Maendeleo hayana vyama!
Police yeyote ninaemuona huwa akili inaniambia uyu form four hakufanya vizuri.
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,413
2,000
Wakaombe walishauri kundi la watu wasiojulikana maana hao ndio wanahitaji ushauri wa kidhalimu. Jamii haihitaji ushauri wao. Huyo anayesema atoe ushauri wa utalii, hakuna ushauri wa utalii unatolewa na wazee.
Aiseee watu mna roho mbaya sana!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom