Elections 2010 Makame anataka kujiuzulu kwa aibu!

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Nasikia Makame anataka kujiuzulu kwa aibu, baada ya kubaini alipotoshwa na UWT -- ila tu baadhi ya makamishna wazee wengine wanamsihi abakie madarakani hadi zoezi la kutanbgaza matokeo liilshe. Bila shaka anaanza kutubu kwa madhambi aliyowafanyia Watz.

Naye Kiravu tangu ashinikize kutangazwa kwa matokeo ya Segerea amekuwa haonekani katika vikao kadha vya Tuyme na taarifa zinasema anasumbuliwa na sukari.
 
kaazi kweli kweli..!

kamaliza kazi aliotumwa ya kuchakachua...! awe makini huko uraiani lakini..!
 
Nasikia Makame anataka kujiuzulu kwa aibu, baada ya kubaini alipotoshwa na UWT -- ila tu baadhi ya makamishna wazee wengine wanamsihi abakie madarakani hadi zoezi la kutanbgaza matokeo liilshe. Bila shaka anaanza kutubu kwa madhambi aliyowafanyia Watz.

Naye Kiravu tangu ashinikize kutangazwa kwa matokeo ya Segerea amekuwa haonekani katika vikao kadha vya Tuyme na taarifa zinasema anasumbuliwa na sukari.

Hawezi kujiuzulu ameisha sema, hata mlie machozi ya damu mpaka muda wake kisheria uishe na naisikia ni 2016 , ambapo uchaguzi wa 2015 atakuwepo tena tume ya uchaguzi
 
Mungu alie juu atawalipa kwa yale wanayoyatenda kwa viumbe vyake
 
Watz wanaumia sana kuona haya mambo yakiendelea, wasione wamekaa kimyaa lakini kuna wakati watavunja ukimya wao na kila aliyeiba hatakuwa na amani tena. Wala hizo wanazoziiba zitageuka zero zote.
Binadamu hatujifunzi kutokana na makosa yaliyofanywa na sehemu kadha wa kadha, ipo siku kitatokea kitu cha ajabu sana na watashangaa sana.
 
Hawezi kujiuzulu ameisha sema, hata mlie machozi ya damu mpaka muda wake kisheria uishe na naisikia ni 2016 , ambapo uchaguzi wa 2015 atakuwepo tena tume ya uchaguzi
Wewe unakuwa wa kwanza kupinga kila kitu bila utafiti, sasa hivi umetoka kupinga data zilizokosewa na NEC walipokuletea evidence ukatoweka, jaribu kuwa mstaarabu.
 
Hakika ni vigumu kuzipinga tuhuma za Slaa -- kuna dosari nyingi mno, tena za wazi wazi. Hawezi kuzipatia maelezo moja moja, labda ajikinge tu kwa kusema ni typing error, au akiri bayana kwamba amepotoshwa na wasimamizi wake vituoni.

By the way, hawa anaodai ni wasimamizi wake -- ni kweli ana mamlaka nao -- yaani Tume yake ndiyo iliwateua? Hawa ma-DED si wateule wa Mwenyekiti wa chama tawala -- CCM -- kwa nini Tume inataka kutufanya Watanzania mafala?
 
Wamesha tufanya tayari.
 
sisi kujiuzulu kwake hakutatusaidia ,sisi tunataka wabunge wetu walioibiwa kura majimboni wapate haki zao, na tunataka uchaguzi wa uraisi urudiwe maana huu ni upumbavu, etii ajiuzulu amalize matatizo yetu kwanza ndooo aende kufilia mbali kujiuzulu . mi napata hasira sana hii nchi washafanya yao
 
The animal is ignorant of the fact that he knows. The man is aware of the fact that he is ignorant.
 
Hakika ni vigumu kuzipinga tuhuma za Slaa -- kuna dosari nyingi mno, tena za wazi wazi. Hawezi kuzipatia maelezo moja moja, labda ajikinge tu kwa kusema ni typing error, au akiri bayana kwamba amepotoshwa na wasimamizi wake vituoni.

By the way, hawa anaodai ni wasimamizi wake -- ni kweli ana mamlaka nao -- yaani Tume yake ndiyo iliwateua? Hawa ma-DED si wateule wa Mwenyekiti wa chama tawala -- CCM -- kwa nini Tume inataka kutufanya Watanzania mafala?

Sheria ya uchaguzi ipo hivyo, cha msingi mngeenda kubadilisha sheria bungeni na sio humu kwenye JF
 
sisi kujiuzulu kwake hakutatusaidia ,sisi tunataka wabunge wetu walioibiwa kura majimboni wapate haki zao, na tunataka uchaguzi wa uraisi urudiwe maana huu ni upumbavu, etii ajiuzulu amalize matatizo yetu kwanza ndooo aende kufilia mbali kujiuzulu . mi napata hasira sana hii nchi washafanya yao

Kuziuzuru hawezi kujiuzuru ameisha sema , na 2015 bado atakuwa MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI. MUDA WAKE WAISHA 2016
 
Mzee makame kwa nini hakujifunza yale ya Kivuitu wa kenya? Tena humuhumu JF watu walianza kuandika mapema kabisa kumtahadharisha yeye na tume nzima. Kama aliona mambo ya uhuni wa ccm asingeyaweza, kwa nini hakujiudhuru mapema? Kujiuzuru sasa haitatusaidia kwa sababu kitendo alichokifanya tayari kimeumiza watu wengi na - tuseme - taifa zima. Atawezaje kuponya vidonda vya watanzania wanaonung'unika na kulia. Hakika atakufa kifo cha aibu. Kitendo hiki kitaisumbua sana nafsi yake.
 
Back
Top Bottom