Makambo achaguliwa 40 Bora kupata timu wachezaji 23 wa timu ya Taifa DRC

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490

Mshambuliaji wa Yanga SC, Mkongoman Heritier Makambo amezidi kung’ara baada ya kuchaguliwa kwenye orodha ya awali ya Wachezaji 40 watakaounda kikosi cha timu ya Taifa ya DR Congo.

Congo ni kati ya timu zinazochuana kuwania kufuzu mashindano ya kimataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika nchini Cameroon.

Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera alisema mshambuliaji huyo yumo kwenye mchujo wa wachezaji 40 watakaounda kikosi cha Wachezaji 23 watakaoichezea DR Congo.

Zahera alisema mshambuliaji huyo ameitwa katika kikosi hicho cha awali kutokana na kiwango kikubwa ambacho amekionyesha akiwa na Yanga tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi.

“Congo tuna utaratibu wetu wa kuita wachezaji wa timu ya taifa ambao siku 15 kabla ya kutangaza timu itakayoiwakilisha nchi katika mashindano mbalimbali, tunatangaza wachezaji 40 wa awali na baada ya hapo kufanya mchujo na kufikia 23.

“Wachezaji hao 23 ndiyo watakaounda timu ya taifa na kikubwa tunachokiangalia ni kiwango cha mchezaji kutokana na nafasi anayoicheza katika klabu yake", alisema Zahera

Pia amesema kuwa kikubwa Kikubwa anachotakiwa kukifanya hivi sasa Makambo ni kuendelea na kasi yake ya kufunga mabao ili kufanikisha malengo yake aliyojiwekea ya Siku moja kuichezea timu ya taifa ambayo tayari imeanza kutimia.
 
Huyu Zahera anaaaanza kupeleka Siasa za Bongo kwenye soka la DRC. Makambo hayupo kwenye top 100 ya wachezaji wa DRC wanaostahili kuitwa Kinshansa. Hizo ni mbinu za Zahera kumpa Kick huyo Bw.Mdogo nothing else.
 
K
Zile machine za AS Vita,Tp Mazembe, Motema Pembe na zingine huko ufarasa unaziweka wapi mpaka huyo Makambo apate chance.

Mwambieni ajifunze kwanza kufunga mdomo
Kaa kimya Makambo zaidi ya wachezaji.wa Vita..aliwapiga hat trick TP Mazembe ..kuwa n adabu dogo..hata wakinifungia nakula JF
 
Eti 40 bora!wakati Kagere,Okwi,Niyo,Mulshid Juuko,Chama ni wachezaji tegemezi wa timu zao
Mkuu ni dhihaka kubwa kulinganisha Earthworm na Cobra angalia tofautisha kwanza viwango vya FIFA na upinzani kati ya mataifa wanaotokea hizo takataka za mkia na DRC ndio useme hivyo hapo sawa na kusema Samata zaidi ya suarez au salah kwa kigezo cha samata kuwazidi magoli kwenye ligi na kuwa top scorer wa ligi anayochezea
 
Zile machine za AS Vita,Tp Mazembe, Motema Pembe na zingine huko ufarasa unaziweka wapi mpaka huyo Makambo apate chance.

Mwambieni ajifunze kwanza kufunga mdomo
Unaongea kikike ..hiwezi kufananisha Wacongo Na takataka nyingine..Papii alipita Yanga akaenda Ulaya hata Makambo itakuwa. hivyohivyo
 
Yaani makombo haya haya yanayozidiwa kiwango hata na mimi??
Mikia hamna striker kama Makambo....ball control angalia magoli yenu ya tap in..dogo anaondoka mbele..Boco alishindwa majaribio Super sports SA..wachezaji wa Mikia 70% wazee nani atawanunua...
 
Taka taka zipo ile timu Vyura fc tuliyoifumua marinda kimoja cha mkwezi juzi
Kufungwa Yanga kunasababishwa na mamluki kama Yondani..Boco anapitaje kirahisi vile ...Mipango brother.. Michezaji mizee inaangalia mshiko tu.kauza Timu afukuzwe
 
Kufungwa Yanga kunasababishwa na mamluki kama Yondani..Boco anapitaje kirahisi vile ...Mipango brother.. Michezaji mizee inaangalia mshiko tu.kauza Timu afukuzwe
Brother inaonekana hujui chochote kuhusu mpira....huyo bocco ndo binadamu aliyefunga magoli mengi kwenye tpl kuliko binadamu yoyote yule...yondani ni moja kati ya mabeki wazuri sana hapa nchini
 
Brother inaonekana hujui chochote kuhusu mpira....huyo bocco ndo binadamu aliyefunga magoli mengi kwenye tpl kuliko binadamu yoyote yule...yondani ni moja kati ya mabeki wazuri sana hapa nchini
Kafunga magoli akiwa timu ndogo ya Azam ..wakicheza wadogo hakuna kukamiana..Mikia kafunga magoli mangapi??
 
Kafunga magoli akiwa timu ndogo ya Azam ..wakicheza wadogo hakuna kukamiana..Mikia kafunga magoli mangapi??
ndo mana nimekwambia hujui na hufuatilii mpira...mwaka jana bocco alikuwa mmoja kati ya wachezaji waliofunga magoli mengi ligi kuu...mwaka huu vilevile mpaka sasa katika list ya wachezaji waliofunga magoli mengi yupo...sasa sjui huyo bocco wa mwaka jana na mwaka huu bado anachezea azam
 
Mikia hamna striker kama Makambo....ball control angalia magoli yenu ya tap in..dogo anaondoka mbele..Boco alishindwa majaribio Super sports SA..wachezaji wa Mikia 70% wazee nani atawanunua...

Kagere kawachana waarabu,vyura,stand nk tena mfululuzo usimfananishe na vitu vya kijinga mkuu
 
Eti 40 bora!wakati Kagere,Okwi,Niyo,Mulshid Juuko,Chama ni wachezaji tegemezi wa timu zao
Mkuu usisahau kucheki Fifa Ranking uone hizo timu za kina Kagere na Chama zinashika nafasi ya ngapi na Congo Drc ya ngapi. Point yangu ni ngumu kwa mchezaji anayecheza ligi za Afrika kupata nafasi timu ya taifa ya Congo. Kama unakumbuka mara ya mwisho walikuja hapa Bongo na wachezaji Wanne tu toka ligi ya ndani wengine wote Mapro.
 
Back
Top Bottom