Makambako Njombe: Polisi amtwanga risasi hadi kufariki mpenzi wake ambaye ni Mwanajeshi

Habari za asubuhi wana JF

Katika mji Mdogo wa kibiashara uitwao Makambako ulio mkoani Njombe asubuhi ya leo Askari polisi ajulikanae kwa majina ya Zakayo Dotto Kileka amemtwanga risasi na kumsababishia umauti mpenzi wake ambae ni mwanajeshi ajulikanae kwa jina la Neema.

Neema alikua akifanya kazi JWTZ Camp ya Makambako na Zakayo nae ni Polisi Makambako.

Inasemekana Zakayo alichukua silaha kituoni asubuhi ya leo tayari kwa kwenda lindo katika benk ya NBC Makambako na ndipo aliponyoosha hadi nyumbani kwa neema na kumsababishia umauti huo.

Zakayo ametoroka na juhudi za kumsaka zinaendelea. Chanzo cha ugomvi hakijajulikana bado zaidi ya kuhisiwa kua ugomvi wa mapenzi.

NB: Naomba CCP waongeze kozi ya saikolojia kwa askari wetu. Matukio kama haya yanajirudia sana kwa polisi na askari magereza.
Kama kweli hii story ni ya kweli basi,kuna uzembe mkubwa umefanyika ,nimachojua Mimi askari huwa wanakuwa kwenye escort za pamoja wanapoenda lindoni ,sasa cha kushangaza huyu polisi anawezaje kutoka na silaa akiwa peke yake na mpaka kufikanayo geto? Sina uzoefu na mambo ya jeshi lakini hii kwa akili ya kawaida tu hainiingii hakilini. Wanaojua sheria za jeshi mtusaidie hapa mtu anawezaje kwenda na silaha getoni ?
 
kama kasepa na silaha, na hicho kifo kimesababishwa na ishu za mapenzi labda kusalitiana huyo mwanaume mlamba asali ya mwenzake ajiandae..!
 
Zakayo maanake alizidiwa nguvu na Neema.... Ndani Kuna kila Aina ya silaha... Kama visu, vijiko... Umma Nk...
Aisee Zakayo unanikumbusha ya bushoke
 
Ni wivu wa kimapenzi au tatizo ni nini
Cyo polisi wala jwtz waliojitokeza kutoa habari kamili na kisa cha mauaji haya hadi sasahivi.

Kwasasa maiti ipo katika chumba cha upasuaji katika hospitali ya mji Makambako kufanyiwa postimotum
 
Kuishi na askari inahitaji moyo sana sijui.hua wanapewa nini wakishaingia kambini na wakitoka wanakua sio wao tena hapo hamna kingine zaid ya ugomvi wa mapenzi...labda jamaa kahisi au kaambiwa au kaona mwenzie anamsaliti pengine kwa vibosile wa huko ujedani

Inasemekana japo siyo rasmi kua Neema alikua na kabwana kengine kamabakamabaka
 
Mkuu uweledi, hekima na busara za askari wa jwtz aliehitimu form four huwezi linganisha na akili ya polisi wa form four. Polisi bado ovyo sana. CCP inahitaji kitu cha nyongeza
waongezewe mda wa mafunzo
kama miaka 3 hv ingependeza
 
Maadili yao Yana mapungufu makubwa Sana ,unaweza vip kutoka sehem Moja ukiwa na silaha bila kiongozi wako wa zamu kujua Hilo? Jes silaha imepatikana au ameenda kuanzisha kikundi cha wasiojulikana? Maswali mengi yata kosa majibu
 
Ndio huyu kwenye picha?
5d1e01f7010d3a9ae738071a7f40bbc5.jpg
Yap, jamaa ndiyo huyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom