Makambako: Mbunge alia fidia za wananchi mbele ya Rais Samia, Waziri amjibu

Binti 1

Member
Dec 1, 2018
22
60
Mbunge wa Jimbo la Makambako, Deo Sanga amemuomba Rais Samia Suluhu amuagize Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kulipa fidia kwa wananchi ambao maeneo yao yalichukuliwa. Mbunge huyo ametoa malalamiko hayo leo hii katika ziara ya Rais jimbo la Makambako.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, kuna maeneo yalichukuliwa ndani ya jimbo lake kwa ajili ya kujenga kituo cha polisi siku nyingi zilizopita, na baadhi ya wananchi ambao maeneo yao yalichukuliwa nyumba zao zimebomoka na hawawezi kufanya chochote.

UPDATE: Waziri wa mambo ya ndani ajibu hoja
Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema kwamba, hapo awali wananchi hao wa kaya 14 waligoma kupokea fidia waliyotakiwa kulipwa ambayo ilikuwa takribani millioni 89. Masauni amesema, wananchi hao waligoma kwa sababu tathimini hiyo ilihusisha shughuli zao za kimaendeleo pekee bila kuhusisha ardhi.

Aidha, waziri huyo ameongeza kuwa Rais Samia aliagiza tathmini hiyo kurudiwa. Baada ya kurudiwa kwa kuhusisha eneo la ardhi katika eneo husika, sasa fidia imefikia kiasi cha milioni 209 na kwamba fedha hizo zipo katika bajeti ya mwaka huu wa fedha na zitalipwa wakati wowote kuanzia sasa.​
 
Hoja zote zimejibiwa na pesa zitalipwa kwenye bajeti hii.

Nimefuatilia ziara yote kuanzia Mbeya hadi Njombe, serikali imejibu hoja zote kiusahihi na Kwa ufasaha,hongera zao Sana..

Leo Rais anaingia Iringa.
 
Siasa buana, utadhani hao watu wanaoongea hapo mmoja anaishi mbinguni, mwingi duniani na mwingine kuzimu.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom