Makamba: Waislamu, nafasi za kazi hazigawanywi kama Njugu, someni!!

Status
Not open for further replies.
Muna tufunga kamba za miguu than munataka tukimbie tutaweza wapi ? Acheni siasa kwenye serious issue.
 
Wachangiaji ndio mnaopotosha jambo hilo. Sioni kama Makamba amekosea kitu. Nalinganisha na Mzazi anayewaasa watoto wake kufanya bidii ya masomo ili wafaulu mitihani. Kwangu mimi hiyo ni changamoto kwetu waislamu na wala sio kebehi. Wachangiaji ndio mnaotaka kuifanya hiyo kauli ya Makamba ionekane kama kebehi au dharau kwa waislamu. Nafikiri yeye amewasomesha watoto wake vizuri tu kwa hiyo hata sisi wengine tufanye hivyo. Big up Mzee Makamba!!
 
Makamba aseme waislam hawakusoma kipindi kipi?
Pia ataje ratio ya hao waislam wachache ambao wamesoma ndio ratio ya waislam kwenye ajira?
Yusuf makamba ndo mana waislam wanamwita joseph makamba kutokana na huu ujinga wake wa kuwakebehi waislam.
Hii takwimu makamba kaitoa wapi?
Mbona waislam walivyotaka kuweka hiki kipengele katika sensa wakristo na serikali yao walipinga.
Makamba acha kuwakebehi waislam, hii dunia tunapita tu!
kumbuka ipo siku utakufa na utahukumiwa kutokana na huu upuuzi unaofanya.
Makamba mbona hajasema kuwa NECTA ndio machinjio makuu ya waislam!

walewale wa ponda. jitambue. tafuta elimu, uboreshe maisha yako. hizi kelele hata wkt wa mtume zilikuwepo
 
Majuzi nimepita pale Mkwajuni stand..asbuhi saa mbili naona vitoto vidogo vimevishwa nguo nyeupe za karate na ustaadhi mmoja wamejipanga pale stand wanapiga karate. Kwanini wasikae darasani kujifunza kusoma na kuandika? Ombwe wanalijenga wenyewe bila kujua
 
Wewe sasa ndio unaeleta Udini! Kama huna cha kukoment kaa kimya sio lazima utafute watu wakubaliane na mtazamo wako.
Kwani wapi umeona Uislamu au Ukristo umekashifiwa!? Makamba kawaeleza Waislamu ukweli na kuwashauri kuwasomesha watoto shule wapate elimu Akhera na Dunia,ili waweze kuajiriwa na serikali pale inapo tokea Fursa na wasibaki tu kulalamika kuwa Wakristo wanapendelewa kitu ambacho sio kweli!

MAKAMBA amekuwa mkuu wa mikoa kadhaa nchini kama Morogogoro, Kigoma Dsm. Kwa mfano wa Makamba kasoma kiasi gani hata kudai Waislamu wasome kupata vyeo? Waislamu wa aina gani wasosoma? Acheni pumba hizo. Hao kina GUNINITA darsa la saba ndoo wamesoma nini mpaka kuwa mkuu wa wilaya
 
Katibu mkuu mstaafu wa CCM Yusuph Makamba amewaasa waislamu kusomesha watoto elimu akhera na Dunia, ili waweze kuajiriwa na serikali ktk nafasi mbalimbali.

Amesema kuwa anashangaa Waislamu wakidai kuwa Serikali inawapendelea Wakristo huku wao (Waislamu) wengi wakiwa hawana elimu na kwamba nafasi za kazi haziwezi kugawanywa kama njugu hivyo ni lazima sasa waislamu wahakikishe wanasomesha watoto wao ili waweze kuwa na elimu ya kuweza kuajiriwa.

Source; Radio Free Afrika tuzungumze magazeti.

umeeleweka babu makamba, big up kwa sana.
 
Katibu mkuu mstaafu wa CCM Yusuph Makamba amewaasa waislamu kusomesha watoto elimu akhera na Dunia, ili waweze kuajiriwa na serikali ktk nafasi mbalimbali.

Amesema kuwa anashangaa Waislamu wakidai kuwa Serikali inawapendelea Wakristo huku wao (Waislamu) wengi wakiwa hawana elimu na kwamba nafasi za kazi haziwezi kugawanywa kama njugu hivyo ni lazima sasa waislamu wahakikishe wanasomesha watoto wao ili waweze kuwa na elimu ya kuweza kuajiriwa.

Source; Radio Free Afrika tuzungumze magazeti.

Kwenye ukweli ni vema tuambiane kuliko kukaa kimya tu. Babu makamba komaa nao naamini siku moja utaeleweka vema.
 
Binafsi naona mzee Makamba hajakosea kitu chochote, yeye katoa ushauri kulingana na jinsi anavyoelewa.
Pia ni vyema tuelewe ameongea maneno haya akiwa sehamu gani, kuna maeneo ambayo bado mwamuko wa elimu bado ni ndogo sana hasa kwa watoto wa kike, na hawa wototo wanaozwa hata kabla ya kumaliza elimu ya msingi.
Maeneo mengi ya namna hii wakaazi wake wengi ni Waislamu.
Cha msingi ni kujua haya maneno ameyaongea akiwa wapi, uenda alikoyaongelea haya yakawa yanawahusu.
 
Someni na hii wapenda Amani.

Annur 287

Uthibitisho wa njama dhidi ya Waislamu nchini

HII ni sehemu ya kumi ya mfululizo wa makala ambazo ni sehemu ya muswada wa kitabu "Mwalimu Julius K. Nyerere, Kanisa Katoliki na Uislamu: Dola na tatizo la Udini Tanzania" kitakachotoka hivi karibuni. Kitabu hicho kimeandikwa na mwandishi maarufu wa masuala ya historia hasa ya Tanganyika BWANA MOHAMMED SAID.

KWA nchi ambayo inajigamba kuwa inajali usawa kwa wananchi wake inashangaza kuona kuwa Waislamu wanabaki nyuma na juhudi zozote ambazo Waislamu watafanya ili kuondoa upogo kati yao na Wakristo na kujiletea maendeleo zinapata upinzani na uadui kutoka na mfumo ule ule unaojidai kuwa unasimamisha usawa na haki.

Kitu cha kusikitisha ni kuwa hakupata kusimama hata Muislamu mmoja katika wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kumuunga mkono Profesa Malima kwa dhulma ambayo wote walikuwa wanafahamu kuwa imedumu kwa kipindi kirefu. Hata ndani ya Bunge hakuna Muislamu aliyekuwa na ujasiri wa kumtetea Profesa Malima. Muislamu mmoja, Mwenyekiti wa Mkoa wa Pwani, Masudi Mtandika, aliungana na kambi ya Wakristo katka Kamati Kuu ya CCM kumshambulia Profesa Malima. Msimamo wa Mtandika ulikuwa sawa na ule wa Rajab Diwani na Selemani Kitundu walipomshambulia Bibi Titi Mohamed wakati Kamati Kuu ya TANU ilipokuwa ikijadili EAMWS mwaka wa 1963.

Kampeni ya chuki na propaganda dhidi ya Profesa Malima ikaanzishwa na vyombo vya habari ambavyo vyote vilikuwa chini ya miliki ya Wakristo na hivyo chini ya Kanisa.
Aboud Jumbe, rais wa zamani wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Tanzania, amefanya utafiti kuhusu nafasi ambazo wameshika Waislam katika serikali, Bunge na vyuo vya elimu ya juu. Takwimu alizoonyesha Aboud Jumbe zinatisha. Katika baadhi ya taasisi Waislamu wanaonekana kwa kutokuwepo katika taasisi hizo. Utafiti wa Jumbe ulikuwa wa pili katika kueleza tatizo hili la Waislamu na kuliweka wazi kwa matumaini ya kuwa labda serikali ingeweza kuhisi kuwajibika na kujaribu kusahihisha makosa hayo.

Majaribio mengine yamewahi kufanyika huko nyuma na watu kama Sheikh Abubakar Mwilima, wakati huo akiwa Mwenyekiti wa JUWATA na katika Kamati Kuu ya chama tawala CCM, alijaribu kuieleza serikali tatizo hili la Waislamu.
Kitu kimoja mashuhuri kwa wote waliojaribu kuliweka tatizo hili mbele ya serikali wote hao walimalizwa kisiasa. Maisha yao katika siasa yalikatizwa - Chifu Abdallah Said Fundikira, Tewa Said Tewa, Bibi Titi Mohamed, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Mussa Kwikima, Sheikh Abubakr Mwilima, Profesa Kighoma Malima na wengine wengi. Ilikuwa kuanzia hapa ndipo Waislamu walianza kunong'ona kuhusu njama dhidi yao.

Kuwepo kwa njama dhidi ya Waislamu kulikuja kudhihirishwa pale watafiti wa Kikristo walipoanza kufanya utafiti kuhusu athari za Ukristo katika utawala wa dola; na bila kujali matokeo ya utafiti kwa hisia za Waislamu wakawa wanaeleza jinsi Waislamu kwa hila na msaada wa serikali walivyowekwa pembeni katika kugawana madaraka na Wakristo.

Hivi sasa kuna vitabu viwili vilivyoandikwa na Wakristo wenyewe vinavyothibitisha kuwa Wakristo wametumia nyadhifa zao katika serikali kuuhujumu Uislamu na Waislamu.

Jan P van Bergen katika kitabu chake, Development and Religion in Tanzania, (1981) ametoboa siri kuhusu uadui aliokuwa nao Nyerere dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Kitabu kinaeleza kwa ufasaha jinsi Nyerere wakati alipokuwa madarakani alivyokuwa akifanya mikutano ya siri na viongozi wa Kanisa kuweka mikakati ya kuupa nguvu Ukristo. Katika mikutano hiyo Nyerere aliwahakikishia viongozi wa Kanisa kuwa anaaunga mkono Ukristo.
Kitabu hicho kinaeleza jinsi Nyerere alivyotimiza ahadi yake hiyo kwa Kanisa kwa kuhakikisha kuwa anawapa Wakristo nafasi za juu katika serikali na chama.
Kitabu hiki kilikuwa kikiuzwa Catholic Bookshop, Dar es Salaam. Lakini ilipokuja kudhihirikia Kanisa kuwa kitabu hiki kilikuwa kinatoa habari nyeti na siri za Kanisa kuhusu njama dhidi ya Waislam, kwa haraka sana kikaacha kuuzwa. Hadi hivi sasa kitabu hicho ni marufuku kuletwa tena Tanzania.
Kitabu cha pili ni cha Dr John C. Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985 (1992).
Kitabu hiki kinaeleza njama ndani ya serikali kuuhujumu Uislam. Sivalon anafichua kuwa kuanzia mwaka 1961 baada ya Tanganyika kupata uhuru, Kanisa lilikuwa na hofu mbili. Hofu ya kwanza ilikuwa umoja wa madhehebu za Kiislamu kati ya Sunni, Bohora, Ismailia na Ithnasheri. Hofu ya pili ilikuwa kuhamishwa kwa makao makuu ya EAMWS kutoka Mombasa kuja Dar es Salaam. Kanisa lilikuwa linahofu kuwa mali walizokuwanazo Waasia Waislamu zikitiwa katika shughuli za Waislamu ambao walikuwa na nguvu kubwa katika uwanja wa siasa zitaathiri maslahi ya Ukatoliki katika Afrika ya Mashariki. Kwa ajili hii Kanisa likatanganza kuwa Uislamu ni adui wake na ikaanza mikakati ya hujma dhidi ya Uislamu ili kuudhoofisha.
Kuna kazi mbili zilizoandikwa na Waislamu kuhusu uhusiano baina ya serikali na Waislamu. Kazi ya kwanza ni tasnifu ya Kiwanuka, 'The Politics of Islam in Bukoba District' (1973); kazi ya pili ni makala ya utafiti 'Islam and Politics in Tanzania' (1989) iliyoandikwa na mwandishi wa kitabu hiki.
Ilikuwa baada ya kusoma tasnifu ya Kiwanuka na kuona jinsi ukweli wa kuvunjwa kwa EAMWS kulivyopoteshwa ndipo kama Muislamu na kama ada ya Uislamu inavyodai kuwa pande mbili za mgogoro zote lazima zisikilizwe, ndipo nilipoamua kufanya utafiti na kuandika tatizo lile kwa mtazamo wa Waislamu. Ukweli ambao kwa miongo miwili ulizuiwa usifahamike kwa Waislamu.
Kiwanuka anadai na kuafiki kuwa Nyerere alikuwa na haki ya kutumia vyombo vya dola dhidi ya Waislam kwa kuwa kama asingefanya hivyo nchi ingekuwa na mamlaka mbili, yaani ya Waislam na ya serikali. Kwa ajili hii aliamua kuivunja EAMWS ili 'kulinda umoja wa kitaifa'.
Halikadhalika ipo 'Kwikima Report' (1968) ambayo imeeleza kwa ufasaha tatizo la EAMWS, chanzo chake na mchango wa serikali katika kuhujumu umoja wa Waislamu. Taarifa hii inafaa kutumika leo kama dira ya kuelewa tatizo la Waislamu wa Tanzania kama ilivyokuwa wakati ule ilipotolewa kwa mara ya kwanza.
Taarifa ya Kwikima inaeleza jinsi TANU, serikali na Waislam wachache katika TANU walivyodanganyika kudhani kuwa katika kuisaidia serikali kuivunja nguvu EAMWS walikuwa wanatimiza uzalendo na maslahi ya taifa.
Rejea hizi tano ni muhimu kwa wanafunzi wa historia ya siasa Tanzania; na kwa mtafiti yeyote anaetaka kujua chanzo cha chuki baina ya Waislam na serikali na chanzo cha hisia kali za kidini zinazoikumba nchi yetu kuanzia miaka ya 1980.
Rejea zote hizo za vitabu, makala za utafiti na taarifa mbalimbali, ingawa zimeandikwa na waandishi tofauti na kwa muelekeo tofauti zote hizi zinadhihirisha kitu kimoja - kuwepo kwa njama zinazoendelea kwa zaidi ya karne moja dhidi ya Uislamu na Waislamu, kwanza zilikuwa zikifanywa na wakoloni walioitawala Tanganyika na sasa zinafanywa na Wakristo wananchi kuhakikisha kuwa Uislamu haupati nguvu. Kama hali ndiyo hii vipi Uislamu hadi leo bado upo Tanzania na unazidi kupata nguvu kila kuchao? Jibu lipo ndani ya Qur'an.
Hivi sasa Waislamu wanamshutumu Mwalimu Nyerere na uongozi wa Kanisa kwa kusaliti dhamana aliyokabidhiwa na Waislamu ambao ndiyo waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Waislamu wa Tanzania hivi sasa ni kama wanazaliwa upya. Kila kukicha wanatafakari hali yao na mustakbali wao katika Tanzania huru Walipambana na wakoloni, kuanzia vita vya Maji Maji mwaka 1905 hadi kuanzishwa kwa African Association mwaka 1929 na TANU mwaka 1954; hadi uhuru ukapatikana mwaka 1961.
Waislamu wanaamini kuwa baadhi ya majibu ya matatizo yanayowakabili hivi sasa yapo kwenye hii historia yao ya kudai uhuru.
--
 
Me naonaaaa majanga tyu jaman maaana huky kwety znz unaangaliwa asil yako ili upate kaz
 
Get education,look for it wherever and forget who dishes it,haya mambo ya vyuo vya dini sijui dhehebu gani hachana nayo ,na ndio maana Makamba anasisitiza hilo sababu ananufaika na ku-enjoy na elimu ya watoto wake ...ofcourse his kids are flying!
Taja vyuo vinavyomilikiwa na wakristo au waislamu?
 
matoto yake yalikua na qualifications gani kupata kazi ikulu ya ccm? aache unafiki huyo mzee anazeeka vibaya
 
Ndugu zangu

Hii habari haijakamilika, ningependa kujua aliyaongea haya lini, wapi na mazingira gani.
Huo ulikuwa ni udondozi wa magazeti, ila kama Mzee Makamba aliyaongea haya katika hadhira ya waislam kama ujumbe kwa waislam wenzake sioni tatizo kwa hili, mjumbe hauwawi, wachukue mchele waache pumba wakale mbele ya safari.

Respect !!!
 
Makamba aseme waislam hawakusoma kipindi kipi?
Pia ataje ratio ya hao waislam wachache ambao wamesoma ndio ratio ya waislam kwenye ajira?
Yusuf makamba ndo mana waislam wanamwita joseph makamba kutokana na huu ujinga wake wa kuwakebehi waislam.
Hii takwimu makamba kaitoa wapi?
Mbona waislam walivyotaka kuweka hiki kipengele katika sensa wakristo na serikali yao walipinga.
Makamba acha kuwakebehi waislam, hii dunia tunapita tu!
kumbuka ipo siku utakufa na utahukumiwa kutokana na huu upuuzi unaofanya.
Makamba mbona hajasema kuwa NECTA ndio machinjio makuu ya waislam!

Mabingwa wa kupotosha maana tayari mmeingia, kipengere cha kwenye sensa hivi kilitaka idadi ya Waislamu wasiosoma Vs Waislamu waliosoma au ilikua idadi ya Waislam bila kujali status zao? Hivi hapo Makamba kaongea uongo gani? Kama nitakumbuka vizuri, hili swala pia hata Sheikh Ali Hassani Mwinyi nae akiwa rais aliwahi kulisema, Ustaadhi Juma Athuman Kapuya nae aliwahi kusema the same kipindi akiwa waziri wa elimu, tena mara 2 kwenye graduations za shule za kiislamu pale Kinondoni, well, mkutano wa Abuja NIgeria mwaka 1992 Masheikh wakubwa waliazimia kulisema hili kwenye nchi zao, Tanzania iliwakilishwa na Rashid Idd Athuman Njeja, kubali ukweli huo mkuu!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom