Makamba, unatumia muda mwingi kujibrand kuliko kupambana na mgao umeme

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
Abuu Kauthar

Huku ninapoishi, Mburahati Barafu, katika wiki moja, umeme ulikatika siku sita kwa saa kuanzia sita hadi 14. Katika baadhi ya siku, umeme ulikatika mara kadhaa. Kukatika huko kwa umeme sio tu ni kero kubwa, lakini pia kumeongeza umaskini wa wananchi wanaotegemea nishati hiyo katika shughuli zao.

Baadhi yetu tunanunua vitoweo kwa wingi na kuwahifadhi katika jokofu. Wengi wetu imebidi tutupe samaki na kuku hao baada ya kuharibika kwa sababu tu ya mgao! Mamia ya kaya katika ambazo zinategemea umeme nazo zimejikuta zikisererekea katika umaskini kwa kukosa nishati wakiwemo wenye saluni, wauza juisi, watoa nakala za nyaraka.

Ukiwakuta mitaani mbele ya ofisi zao, utawakuta watu hao wamekaa nje wanapiga soga hawajui hatima yao.

Ulianza mgao wa mchana tu tukaambiwa ni matengenezo lakini sasa TANESCO wanakata hadi usiku! Hutokea baadhi ya siku umeme kuchelewa kurudi hadi saa tano usiku au zaidi. Isingekuwa Mwenyezi Mungu kutusitiri kwa mvua inayosaidia kupunguza joto, baadhi ya nyumba zisingelalika na huenda tungerejea zile zama za kulala vibarazani.

Nini kimebadilika katika kipindi kifupi tangu tulipobadili awamu ya utawala kutoka ya tano hadi ya sita. Tunaelewa kuwa kuna ukame, lakini wengi wetu hatuamini kama Rais John Magufuli angekuwa hai hali ingekuwa mbaya kiasi hiki. Kwa namna tunavyoona mwenendo wa viongozi wetu, ni vigumu kujua kama ni ukame tu au ni udhaifu wa viongozi na watendaji wa TANESCO?

Tuseme ukweli, kwa hali ilivyo sasa ni vigumu sana kupembua kati ya mchango wa ukame katika kupelekea tatizo la mgao na mchango wa uzembe. Walau kipindi kile Magufuli aliwakoromea na hata kuwatimua madarakani viongozi aliowapa majukumu ya kusimamia sekta hii nyeti ya nishati. Hivi sasa, tuna viongozi ‘baridi’ na ‘waelewa’ ambao wameamua kuwa wa kwanza kutoa nadharia, visingizio na kulaumu waliopita.[ badala ya kukabiliana na tatizo na kuliondoa.

Natamani wangejua kuwa wananchi wanataka umeme sasa, sio visingizio. Natamani wangejua kuwa haijalishi nani aliyekosea, sisi tunawatathmini kwa wanachofanya sasa kwani ukichambua utagundua kuwa kila awamu ilirithi matatizo ya awamu iliyopita, lakini na mazuri pia.

Nikiangalia ukurasa wa waziri wetu wa Nishati, bwana Januari Makamba, napata hisia kuwa huyu ni mtu aliye mbali na uhalisia wa maisha ya watu, anayefikiria mustkbali wake wa kisiasa kuliko shida ya mgao, akiposti picha kwenye kumbi na maofisi na watu wa hadhi, akionesha namna alivyo mweledi na mjuvi wa hali ya nishati duniani na nadharia ya namna Tanzania tutajikomboa.

Makamba ni bingwa wa kujibrand, ukimuona anavyopozi kwenye picha utadhani ni Obama mpya, shukran kwa timu ya timu yenye weledi imayohusika kumjenga na kumuandaa kwa nafsi ya juu kabisa! Lakini itasaidia nini kama kazi ya kutatua shida za wananchi katika nafasi hii uliyonayo sasa huitendei haki?

Nilipata hamu ya kutembelea tovuti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambako unakutana tena na sura ya Waziri Makamba akiahidi ‘kuzaliwa upya kwa TANESCO’ katika habari moja na akiahidi TANESCO litakuwa shirika bora la umeme Afrika ya Mashariki kwenye habari nyingine!

Ukiangalia vizuri hii tovuti, huwezi kujua kama nchi iko gizani! Wanazungumzia kila kitu lakini sio mgao! Hata ratiba ya mgao basi? Hata ushauri? Hata kutuomba radhi basi? Au ndio nyi haliwahusu bali ni makosa ya waleeee waliokuwepo kabla!? Hali ni hiyo hiyo katika tovuti ya Wizara ya Nishati. Kuna mgogoro wa mgao wa umeme lakini kuna habari nzuri tupu ni kama vile kila kitu kipo shwari mpaka unajiuliza hizi tovuti ni kwa ajili ya kusomwa na nani?

Hizi ndio siasa ambazo wananchi tumechoka nazo. Waziri Makamba anza na kutatua hili tatizo la mgao, kabla hujawaza makubwa na kabla hujamchafua Rais Samia na kuonekana hafai!
 
Hiyo ni tabia ya kila mtanzania anayependa kukalia kile kiti...
 
hoja ni umeme hayo mambo ya kwamba anatumia mda mwingi kujibrand ni umbea tu na wivu usio na maana
 
Umeme ni tatizo maeneo kadha kwa sasa.
Lakina kwa huyu waziri mbona toka mwanzo tulishakubaliana kuwa
"Tumepigwa..."
Au hamkuelewa.
 
Ulitaka umuone kaning'inia kwenye nguzo ya umeme ndio ujue anapambana
 
Poleni, ila napoishi Kigamboni umeme upo muda wote.

Ulikatika siku moja tu masaa kama 10 hv, ila upo sana kama kuna wadau wa kigamboni wanaweza thibitisha.
 
ungekuwa wewe ungefanyaje umepata opportunity hiyo na unajua unaweza kuja kuwa rais? though kwasababu awamu hii ya sita na ya saba yupo mama, awamu inayofuata lazima atakuja mtu wa vatican ili twende sawa. Naona historia inaongea hivyo. Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete, John Pombe, Samia kadakia, mgalatia atafuata hapo. nadeclare interest, mimi ni mgalatia ila sio wale waliologwa aliowaongelea paulo.
 
Ukame ni nini
Nadhani inahusisha msimu wa mvua kupita bila mvua kunyesha
Hatujawa na ukame Tanzania kwa kipindi hichi
Lakini humu ndani kuna yale mazuzu yanayocoment ujinga nadhani yako kwenye pay roll
 
Abuu Kauthar

Huku ninapoishi, Mburahati Barafu, katika wiki moja, umeme ulikatika siku sita kwa saa kuanzia sita hadi 14. Katika baadhi ya siku, umeme ulikatika mara kadhaa. Kukatika huko kwa umeme sio tu ni kero kubwa, lakini pia kumeongeza umaskini wa wananchi wanaotegemea nishati hiyo katika shughuli zao.

Baadhi yetu tunanunua vitoweo kwa wingi na kuwahifadhi katika jokofu. Wengi wetu imebidi tutupe samaki na kuku hao baada ya kuharibika kwa sababu tu ya mgao! Mamia ya kaya katika ambazo zinategemea umeme nazo zimejikuta zikisererekea katika umaskini kwa kukosa nishati wakiwemo wenye saluni, wauza juisi, watoa nakala za nyaraka.

Ukiwakuta mitaani mbele ya ofisi zao, utawakuta watu hao wamekaa nje wanapiga soga hawajui hatima yao.

Ulianza mgao wa mchana tu tukaambiwa ni matengenezo lakini sasa TANESCO wanakata hadi usiku! Hutokea baadhi ya siku umeme kuchelewa kurudi hadi saa tano usiku au zaidi. Isingekuwa Mwenyezi Mungu kutusitiri kwa mvua inayosaidia kupunguza joto, baadhi ya nyumba zisingelalika na huenda tungerejea zile zama za kulala vibarazani.

Nini kimebadilika katika kipindi kifupi tangu tulipobadili awamu ya utawala kutoka ya tano hadi ya sita. Tunaelewa kuwa kuna ukame, lakini wengi wetu hatuamini kama Rais John Magufuli angekuwa hai hali ingekuwa mbaya kiasi hiki. Kwa namna tunavyoona mwenendo wa viongozi wetu, ni vigumu kujua kama ni ukame tu au ni udhaifu wa viongozi na watendaji wa TANESCO?

Tuseme ukweli, kwa hali ilivyo sasa ni vigumu sana kupembua kati ya mchango wa ukame katika kupelekea tatizo la mgao na mchango wa uzembe. Walau kipindi kile Magufuli aliwakoromea na hata kuwatimua madarakani viongozi aliowapa majukumu ya kusimamia sekta hii nyeti ya nishati. Hivi sasa, tuna viongozi ‘baridi’ na ‘waelewa’ ambao wameamua kuwa wa kwanza kutoa nadharia, visingizio na kulaumu waliopita.[ badala ya kukabiliana na tatizo na kuliondoa.

Natamani wangejua kuwa wananchi wanataka umeme sasa, sio visingizio. Natamani wangejua kuwa haijalishi nani aliyekosea, sisi tunawatathmini kwa wanachofanya sasa kwani ukichambua utagundua kuwa kila awamu ilirithi matatizo ya awamu iliyopita, lakini na mazuri pia.

Nikiangalia ukurasa wa waziri wetu wa Nishati, bwana Januari Makamba, napata hisia kuwa huyu ni mtu aliye mbali na uhalisia wa maisha ya watu, anayefikiria mustkbali wake wa kisiasa kuliko shida ya mgao, akiposti picha kwenye kumbi na maofisi na watu wa hadhi, akionesha namna alivyo mweledi na mjuvi wa hali ya nishati duniani na nadharia ya namna Tanzania tutajikomboa.

Makamba ni bingwa wa kujibrand, ukimuona anavyopozi kwenye picha utadhani ni Obama mpya, shukran kwa timu ya timu yenye weledi imayohusika kumjenga na kumuandaa kwa nafsi ya juu kabisa! Lakini itasaidia nini kama kazi ya kutatua shida za wananchi katika nafasi hii uliyonayo sasa huitendei haki?

Nilipata hamu ya kutembelea tovuti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambako unakutana tena na sura ya Waziri Makamba akiahidi ‘kuzaliwa upya kwa TANESCO’ katika habari moja na akiahidi TANESCO litakuwa shirika bora la umeme Afrika ya Mashariki kwenye habari nyingine!

Ukiangalia vizuri hii tovuti, huwezi kujua kama nchi iko gizani! Wanazungumzia kila kitu lakini sio mgao! Hata ratiba ya mgao basi? Hata ushauri? Hata kutuomba radhi basi? Au ndio nyi haliwahusu bali ni makosa ya waleeee waliokuwepo kabla!? Hali ni hiyo hiyo katika tovuti ya Wizara ya Nishati. Kuna mgogoro wa mgao wa umeme lakini kuna habari nzuri tupu ni kama vile kila kitu kipo shwari mpaka unajiuliza hizi tovuti ni kwa ajili ya kusomwa na nani?

Hizi ndio siasa ambazo wananchi tumechoka nazo. Waziri Makamba anza na kutatua hili tatizo la mgao, kabla hujawaza makubwa na kabla hujamchafua Rais Samia na kuonekana hafai!
Anabebwa na kundi fulani nakumbuka akiwa waziri wa JK alijichomeka Songea kuwagawia simu na kuzungumzia kilimo wakati hakuwa waziri wa kilimo, akaenda Mwanza akaropoka anayoyajua yeye kwa mapadre wakati hakuwa waziri kwenye wizara husika, ila anaonekana wazi hawezi uongozi ni kama mbambaishaji fulani
 
Ukame ni nini
Nadhani inahusisha msimu wa mvua kupita bila mvua kunyesha
Hatujawa na ukame Tanzania kwa kipindi hichi
Lakini humu ndani kuna yale mazuzu yanayocoment ujinga nadhani yako kwenye pay roll
Bwana mdogo anajitaidi kujibrand lakini ajue watu wanajua kama hana kitu cha kusaidia taifa hili, infact uwezo mdogo sema anajua kucheza ngoma na watu na hii ndio silaha yake
 
Abuu Kauthar

Huku ninapoishi, Mburahati Barafu, katika wiki moja, umeme ulikatika siku sita kwa saa kuanzia sita hadi 14. Katika baadhi ya siku, umeme ulikatika mara kadhaa. Kukatika huko kwa umeme sio tu ni kero kubwa, lakini pia kumeongeza umaskini wa wananchi wanaotegemea nishati hiyo katika shughuli zao.

Baadhi yetu tunanunua vitoweo kwa wingi na kuwahifadhi katika jokofu. Wengi wetu imebidi tutupe samaki na kuku hao baada ya kuharibika kwa sababu tu ya mgao! Mamia ya kaya katika ambazo zinategemea umeme nazo zimejikuta zikisererekea katika umaskini kwa kukosa nishati wakiwemo wenye saluni, wauza juisi, watoa nakala za nyaraka.

Ukiwakuta mitaani mbele ya ofisi zao, utawakuta watu hao wamekaa nje wanapiga soga hawajui hatima yao.

Ulianza mgao wa mchana tu tukaambiwa ni matengenezo lakini sasa TANESCO wanakata hadi usiku! Hutokea baadhi ya siku umeme kuchelewa kurudi hadi saa tano usiku au zaidi. Isingekuwa Mwenyezi Mungu kutusitiri kwa mvua inayosaidia kupunguza joto, baadhi ya nyumba zisingelalika na huenda tungerejea zile zama za kulala vibarazani.

Nini kimebadilika katika kipindi kifupi tangu tulipobadili awamu ya utawala kutoka ya tano hadi ya sita. Tunaelewa kuwa kuna ukame, lakini wengi wetu hatuamini kama Rais John Magufuli angekuwa hai hali ingekuwa mbaya kiasi hiki. Kwa namna tunavyoona mwenendo wa viongozi wetu, ni vigumu kujua kama ni ukame tu au ni udhaifu wa viongozi na watendaji wa TANESCO?

Tuseme ukweli, kwa hali ilivyo sasa ni vigumu sana kupembua kati ya mchango wa ukame katika kupelekea tatizo la mgao na mchango wa uzembe. Walau kipindi kile Magufuli aliwakoromea na hata kuwatimua madarakani viongozi aliowapa majukumu ya kusimamia sekta hii nyeti ya nishati. Hivi sasa, tuna viongozi ‘baridi’ na ‘waelewa’ ambao wameamua kuwa wa kwanza kutoa nadharia, visingizio na kulaumu waliopita.[ badala ya kukabiliana na tatizo na kuliondoa.

Natamani wangejua kuwa wananchi wanataka umeme sasa, sio visingizio. Natamani wangejua kuwa haijalishi nani aliyekosea, sisi tunawatathmini kwa wanachofanya sasa kwani ukichambua utagundua kuwa kila awamu ilirithi matatizo ya awamu iliyopita, lakini na mazuri pia.

Nikiangalia ukurasa wa waziri wetu wa Nishati, bwana Januari Makamba, napata hisia kuwa huyu ni mtu aliye mbali na uhalisia wa maisha ya watu, anayefikiria mustkbali wake wa kisiasa kuliko shida ya mgao, akiposti picha kwenye kumbi na maofisi na watu wa hadhi, akionesha namna alivyo mweledi na mjuvi wa hali ya nishati duniani na nadharia ya namna Tanzania tutajikomboa.

Makamba ni bingwa wa kujibrand, ukimuona anavyopozi kwenye picha utadhani ni Obama mpya, shukran kwa timu ya timu yenye weledi imayohusika kumjenga na kumuandaa kwa nafsi ya juu kabisa! Lakini itasaidia nini kama kazi ya kutatua shida za wananchi katika nafasi hii uliyonayo sasa huitendei haki?

Nilipata hamu ya kutembelea tovuti ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ambako unakutana tena na sura ya Waziri Makamba akiahidi ‘kuzaliwa upya kwa TANESCO’ katika habari moja na akiahidi TANESCO litakuwa shirika bora la umeme Afrika ya Mashariki kwenye habari nyingine!

Ukiangalia vizuri hii tovuti, huwezi kujua kama nchi iko gizani! Wanazungumzia kila kitu lakini sio mgao! Hata ratiba ya mgao basi? Hata ushauri? Hata kutuomba radhi basi? Au ndio nyi haliwahusu bali ni makosa ya waleeee waliokuwepo kabla!? Hali ni hiyo hiyo katika tovuti ya Wizara ya Nishati. Kuna mgogoro wa mgao wa umeme lakini kuna habari nzuri tupu ni kama vile kila kitu kipo shwari mpaka unajiuliza hizi tovuti ni kwa ajili ya kusomwa na nani?

Hizi ndio siasa ambazo wananchi tumechoka nazo. Waziri Makamba anza na kutatua hili tatizo la mgao, kabla hujawaza makubwa na kabla hujamchafua Rais Samia na kuonekana hafai!
Miaka ya mbele huyu jamaa atafungwa.
 
Alitoa siku mbili atatoa suluhisho la kudumu kukatika kwa umeme mpaka Sasa hajaonekana.
Hatutaki matamuko tunataka umeme usikatike.
Japo amemwaga wapambane jf wakumtetea,mtaangukua pua tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom