Makamba Unalia nini ?Tabata wamzomea Makamba

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Tabata wamzomea Makamba
*Ni wakazi waliovunjiwa nyumba zao
*Amnyang'anya kipaza sauti mjumbe wa shina
*Ni baada ya kupinga ushauri aliotoa kwa wakazi hao
* Wakataa kuchukua viwanja mpaka walipwe



Muhibu Said na Emmanuel Mtinangi

ZIARA ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba kwa wakazi waliovunjiwa nyumba zao katika eneo la Tabata Dampo, jijini Dar es Salaam jana iliingia dosari, baada ya kumzomea alipojaribu kuwashawishi wakubali kuchukua viwanja walivyopimiwa katika eneo la Buyuni, wilayani Ilala.

Wakazi hao wanaoishi katika mahema, walifikia hatua hiyo baada ya Makamba ambaye aliongozana katika ziara hiyo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa na wilaya, kuwahutubia katika eneo ambalo wanaendelea kuishi katika mahema kwa takriban wiki mbili sasa.

Akiwahutubia wananchi hao, aliwashauri wakubali kwenda kuchukua viwanja walivyotengewa na serikali katika eneo hilo, baada ya kuvunjiwa nyumba zao kinyume na taratibu. "Msikubali tatizo hili kuwa la kisiasa, kwani halikufanywa na CCM, ni tatizo la mtu mmoja wa ovyo," alisema na kuongeza: "Najua watakuja watu hapa, watawaambia, oneni hiyo CCM.

Msiwasikilize. Sisi ndio wenye majibu, chama kingine hakina majibu ya matatizo yenu". Alisema mtu anayewazuia kwenda kuchukua viwanja hivyo katika eneo hilo hawatakii mema. Hata hivyo, ushauri huo wa Makamba, ulianza kupingwa na Mjumbe wa Shina namba 16 wa CCM katika eneo hilo, Tauzani Mbwana, baada ya kupewa fursa ya kuzungumza katika mkutano huo.

Katika maelezo yake, Mbwana alimweleza Makamba na ujumbe alioongozana nao kuwa hawawezi kwenda kuchukua viwanja hivyo, badala yake wanachotaka, nyumba zao zilizovunjwa kwanza zithaminiwe, walipwe na waachwe waendelee kuishi katika makazi yao ya zamani (Tabata Dampo).

"Tunaambiwa twende tukachukue viwanja Buyuni. Tunachosema, kabla ya kwenda kuchukua hivyo viwanja, kwanza nyumba zetu zilizovunjwa zithaminiwe, kisha tulipwe na turejeshwe hapa hapa," alisema Mbwana huku akishangiliwa na umati wa wakazi waliofika katika mkutano huo. Hali hiyo ilimfanya Makamba kuingilia kati mazungumzo hayo kwa kumnyang'anya Mbwana kipaza sauti kilichokuwa kikitumiwa na kumkatiza kuendelea kuzungumza na kuwashawishi wakazi hao kwenda Buyuni kuchukua viwanja hivyo.

"Hivi kama mtu anataka kutandika kitanda, si lazima ashuke kwanza kitandani ndipo atandike kitanda," alisema na kuongeza: "Kama ningekuwa mimi, ningeanza kuchukua kwanza kiwanja na baadaye ndio niendelee kudai kuishi hapa hapa. Nawaomba muende mkachukue, mkikataa serikali itasema kuwa, tuliwapa viwanja lakini walikataa kuchukua".

Hata hivyo, ushauri huo wa Makamba uligonga mwamba baada ya wakazi hao kumkatiza na kuanza kuzomea na kumweleza kuwa kamwe hawawezi kwenda kuchukua viwanja Buyuni, badala yake wanachotaka watekelezewe madai yao.

Hali hiyo ilimfanya Makamba kurudi nyuma na kuwaeleza wakazi hao kuwa: "Sisi tunawapa ushauri, mna hiari kuufuata na mna hiari kutoufuata". Mbwana naye alichukua kipaza sauti na kumjibu Makamba akisema: "Huwezi kwenda vitani bila silaha"

Awali, Makamba aliwaeleza wakazi hao kuwa uvunjwaji wa nyumba zao ni moja ya mambo yaliyojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Jumanne wiki hii jijini Dar es Salaam, chini ya Uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete ambaye alisema kuwa alichukizwa na kitendo hicho. "Rais alilizungumza jambo hili, hakupenda na limemkwaza sana," alisema Makamba.

Kwa hali hiyo, alisema serikali inalijua tatizo hilo na kwamba, inalishughulikia na itahakikisha wakazi hao wanapata mahali pa kuishi na kuwataka wawe na subira. Alimtaka Kandoro kuhakikisha vigogo wa serikali waliohusika katika uvunjaji wa nyumba za wakazi hao wanachukuliwa hatua badala ya kuishia kuwachukulia hatua wadogo peke yao. "Msiendelee kuwafukuza wadogo wakati wakubwa waliofanya hivyo wapo," alisema Makamba.

Aliahidi kumkabidhi Kandoro misaada mbalimbali ya kibinadamu, ikiwamo chakula na maji kwa waathirika wa uvunjaji huo, uliofanywa na baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, kinyume na taratibu.

Naye Kandoro alisema serikali haiwalazimishi wakazi hao kuchukua viwanja katika eneo la Buyuni, bali itaendelea kuvipima na kwamba, wanaohitaji ndio watakaopewa. Hata hivyo, alisema serikali itaendelea kutoa huduma za kibinadamu na kwamba watahakikisha vigogo waliohusika na uvunjaji huo wanachukuliwa hatua.

"Kazi itafanyika haraka iwezekanavyo. Tutawahangaikia wakubwa, kote huko tutafika vilevile," alisema Kandoro. Baadhi ya viongozi walioongozana na Makamba katika ziara hiyo ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Ramadhani Madabida na Diwani wa Kata ya Hananasif, Abbas Tarimba.
 
Yeye makamba ndio ameligeuza swala kuwa la kisiasa. Sisi tunachojua ni serikali ya jakaya imebowa nyumba za waungwana pale tabata.
 
Kila kitu turned into politics, they knew this problem before demolition, wakakaa kimya, leo wamebomoa wanajidai watawasaidia watu kwa kuwapa misaada ya kila aina pamoja na viwanja! Walikuwa wapi mwanzoni?
 
Yeye makamba ndio ameligeuza swala kuwa la kisiasa. Sisi tunachojua ni serikali ya jakaya imebowa nyumba za waungwana pale tabata.

Sasa kapata alicho kitaka alidhani watu wamelala .Wao watumie mabavu tu lakini ukweli wanaujua .Makamba kweli ni kichaka duh!!
 
kuna vitu vingie vinaboa hata kufikiri tu unaona..bora tungeweka ma robot kwenye uongozi tu...sijui watu wanaangaliaga sifa gani kabla ya kumchagua mtu kuongoza kitu..huu uliofanyika ni ujinga na ndio inazidi kudhihirisha kuwa tanzania bado sana katika maeneo mengi..yani hili hata huwezi ukasema ni bahati mbaya...hawa ni kufukuza wote tu.
 
kuna vitu vingie vinaboa hata kufiri tu unaona..bora tungeweka ma robot kwenye uongozi tu...sijui watu wanaangaliaga sifa gani kabla ya kumchagua mtu kuongoza kitu..huu uliofanyika ni ujinga na ndio inazidi kudhihirisha kuwa tanzania bado sana katika maeneo mengi..yani kili hata uwezi ukasema ni bahati mbaya...hawa ni kufukuza wote tu

Wako wengi sana,tuanze kutoa elimu kwa TZ walio wengi kwanza then baadaye tuwang'oe mmoja baada ya mwingine!
 
Makamba kashindwa kujua kwamba ni Serikali ya CCM inapaswa kulaumiwa na hivyo CCM inabeba dairekti lawama? Kwa nini kasema Mwenyekiti kahuzunika na yeye kwenda kutembeza siasa kwa niaba ya mwenyekiti wake ?
 
na Lucy Ngowi, Mobini Sarya na Dauson Harold

SIKU chache baada ya wakazi kadhaa katika eneo la Tabata kubomolewa nyumba zao, zimeibuka taarifa za siri zinazoeleza kuwa, viongozi kadhaa wa Manispaa ya Ilala walihongwa kiasi kinachofikia shilingi milioni 100 ili kubariki operesheni hiyo haramu.

Taarifa hizo za kuwapo kwa rushwa katika bomoabomoa hiyo iliyowaacha watu wanaofikia 500 kukosa makazi ya uhakika, zilivujishwa kwa gazeti hili na madiwani kadhaa wa manispaa hiyo.

Aidha, dalili nyingine za wazi za kuwapo kwa ufisadi huo zilithibitishwa na kauli zilizotolewa jana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro waliotembelea eneo hilo la ‘maafa.’

Akizungumza akiwa katika eneo hilo, Makamba alisema Rais Jakaya Kikwete alikuwa amezipokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizo za bomoabomoa zilizofikishwa kwake na Kandoro.

Pasipo kutaja jina la mtu, Makamba alisema kwamba tatizo hilo lilitokana na uamuzi uliofanywa na mtu mmoja aliyemwelezea kuwa ni wa ovyo ovyo kwa maslahi yake binafsi.

Mbali ya hilo, Makamba aliipongeza hatua ya baadhi ya maofisa wa manispaa hiyo kusimamishwa kutokana na tukio hilo, na kuonya kuwa hatua hiyo isiendelee kufukuza wadogo wakati wakubwa wapo.

Katika hatua nyingine, Kandoro ambaye amekuwa akilifuatilia kwa karibu suala hili tangu lilipotokea wiki iliyopita, alisema serikali imefikia hatua ya kuundwa kwa tume huru kuchunguza tukio zima baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa Manispaa ya Ilala kuunda tume yake ya kujichunguza.

Kandoro alisema uamuzi wa kuundwa kwa tume nyingine ulifikiwa kutokana na kikao alichofanya na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Steven Wassira.

Alisema katika mkutano wao walikubaliana kimsingi haja ya kuundwa kwa tume huru ya serikali na kuachana na ile ya Manispaa ya Ilala, ambayo inatuhumiwa kuchukua uamuzi huo mbovu.

“Katika kikao hicho, tulikubaliana kuwa, kesi ya nyani haipelekwi kwa ngedere, hivyo hatukubaliani na utaratibu wa Manispaa ya Ilala kuunda tume ya watu sita, badala yake serikali inaunda tume yake, tathmini itafanyika haraka iwezekanavyo kwa kuwa tunatambua adha, shida na mateso mnayokabiliana nayo. Na kutokana na tume hiyo, tutafika huko kuwa tusihangaike na samaki wadogo,” alisema Kandoro.

Mbali ya hao, madiwani kadhaa wa manispaa ya Ilala waliozungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti jana walisema rushwa iliyotembea miongoni mwa baadhi ya viongozi wao ndiyo iliyosababisha kubomolewa kwa nyumba hizo 96 badala ya nne zilizopaswa awali.

Mbali ya hilo, taarifa nyingine kutoka ndani ya manispaa hiyo zinaeleza kuwa, hata baada ya wakazi wenye nyumba hizo kubomolewa, maofisa kadhaa wa manispaa hiyo wameendelea kunufaika na janga hilo kwa kufuja fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuwapatia chakula wahanga hao.

Habari kutoka ndani ya manispaa hiyo zinaeleza kwamba, viongozi kadhaa wasio waaminifu wa manispaa hiyo, walikula njama na mfanyabiashara mmoja anayemiliki sehemu ndogo katika eneo hilo lililobomolewa ili kufanikisha zoezi hilo ambalo sasa limegeuka kuwa balaa kubwa la kimkoa na kitaifa.

Vyanzo vingine kadhaa vya kuaminika kutoka ndani ya manispaa hiyo vililiambia Tanzania Daima kuwa, maofisa hao walitumia mwanya wa hukumu iliyotolewa kutokana na mgogoro wa ardhi katika eneo hilo iliyofunguliwa mwaka 2002 na mfanyabiashara, Allied Kargoreed.

Katika Kesi hiyo, mfanyabiashara huyo alienda Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kulalamikia uvamizi wa eneo lake, uliofanywa na wananchi wa Tabata Dampo, lakini mahakama ilishindwa kutoa uamuzi na kuwashauri waende Baraza la Usuluhishi wa Ardhi.

Habari zinaeleza kuwa, hata baada ya hukumu hiyo kutolewa, hakuna yeyote aliyekwenda katika baraza hilo la usuluhishi hadi eneo moja la viwanja hivyo lilipouzwa kwa mfanyabiashara mwingine kwa thamani ya shilingi milioni 800.

Diwani mmoja aliyezungumza na Tanzania Daima alisema kwamba, siku chache tu baada ya mtu huyo kununua eneo hilo, alianza kufanya mashauriano na viongozi kadhaa wa manispaa, lengo likiwa ni kutafuta namna ya kuwaondoa wale aliokuwa akidai kuwa ni wavamizi wa eneo lake.

Katika mashauriano hayo, mfanyabiashara huyo alikubaliana na maofisa hao kutoa kiasi cha fedha ambacho kingewawezesha waliovamia eneo lake.

Diwani mmoja aliliambia gazeti hili kuwa, awali mfanyabiashara huyo alikuwa tayari kutoa sh milioni 50, kiasi ambacho kilikataliwa na viongozi waliomtaka aongeze fedha hadi kufikia sh milioni 100, wazo ambalo hatimaye alikubaliana nalo.

Mbali ya huyo, diwani mwingine aliyezungumza na gazeti hili naye alisema kuwa, anao ushahidi unaoonyesha jinsi mchezo huo ulivyokuwa unachezwa, kwani baada ya kukubaliana na mmiliki wa kiwanja hicho, baadhi ya viongozi walifikia hatua ya kudai wao ndiyo wamiliki wa kiwanja hicho na wakafikia hatua ya kuifungulia manispaa hiyo mashtaka ya kuwapa wananchi hao leseni ya makazi.

Diwani huyo alisema kuwa baada ya kesi hiyo kusikilizwa, kwa msaada wa idara ya sheria katika manispaa hiyo, hukumu ilitolewa na manispaa ikaamriwa kubeba jukumu la kuwaondoa wakazi hao katika nyumba nne tu.

“Baada ya hukumu hiyo kutoka, viongozi hao wakakaa wakapanga namna ya kumwandikia mkurugenzi notisi ya kumtaka akawavunjie nyumba wakazi wale… Wakazi hao walipaswa kuambiwa kuwa watalipwa fidia,” alisema diwani huyo.

Kwa mujibu wa diwani huyo, katika kuhakikisha kuwa utekelezwaji wa hukumu unaharakishwa, maofisa kadhaa katika manispaa hiyo ya Ilala walipewa fedha zinazofikia wastani wa sh 500,000 kila mmoja.
Diwani huyo alisema notisi ya kubomolewa kwa nyumba nne iliyoandikwa kwa wakazi hao, ilipelekwa siku ambayo uvunjaji huo ulifanyika chini ya ulinzi wa askari.

Alipofika katika eneo la tukio siku ya uvunjaji, inadaiwa kuwa wakuu wa manispaa hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wake, John Lubuva, walisimamia ubomoaji wa nyumba nne zilizokuwa zimelengwa kabla ya kuondoka kutoka eneo la tukio.

Hata hivyo, baada ya viongozi wa juu wa manispaa waliokuwa hawana habari na ufisadi uliokuwapo kuondoka eneo la tukio, zoezi la bomoabomoa liliendelea kwa maelekezo ya mmoja wa viongozi wa manispaa hiyo.
Jitihada za Tanzania Daima kuzungumza na Lubuva, Meya wa Manispaa ya Ilala, Abuu Juma na Naibu Meya wa manispaa hiyo, Mohammed Yakubu jana kuhusu kuwapo kwa tuhuma za rushwa miongoni mwa maofisa wa manispaa hiyo, ziligonga mwamba baada ya viongozi hao wote wawili kwa nyakati tofauti kukataa kusema lolote wakisema wanaheshimu maelekezo waliyopata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa.

Wakati Luvuba alikataa katakata kuzungumza, Yakubu yeye alimwelekeza mwandishi kwa Meya Juma ambaye naye akasema alikuwa amezuiwa na Kandoro kuzungumza.

“Wewe mwandishi unajua uko makini, ukitaka taarifa nyingine nitakupatia, lakini taarifa za Tabata, Mkuu wa Mkoa ametuzuia kuzungumza na vyombo vya habari na ni yeye mwenye dhamana ya kulizungumzia suala hilo,” alisema Meya Juma kwa njia ya simu jana.

Majibu hayo yalililazimisha Tanzania Daima kuwasiliana na Kandoro, ambaye alikana kuwazuia na kusema kuwa wanapaswa kuzijibu tuhuma hizo zinazoelekezwa kwa viongozi wa manispaa.

“Hilo suala linawahusu wao viongozi wa manispaa. Sijamzuia mtu yeyote yule asiliongelee hilo suala,” alisema Kandoro kwa ufupi na kukata simu.

Naye Mwenyekiti wa Shina la CCM katika eneo hilo, Tauzani Mbwana, alisema kuwa wahanga hao hawajakataa viwanja ila wanachodai ni nyumba zao zilizovunjwa zifanyiwe uthamini.

Mbwana aliongeza kuwa, taratibu za msingi hazikufuatwa katika uvunjaji wa nyumba hizo kwa kuwa mazingira ya rushwa yalijengeka na kusababisha haki isitendeke.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Waathirika, Said Masoud alisema kuwa, tangu wavunjiwe nyumba zao katika eneo hilo, wametembelewa na viongozi mbalimbali, lakini hakuna jambo lolote jipya lililotokea.
Mosoud alirudia ombi lao ni kumuomba Rais Kikwete aingilie kati kuhakikisha kuwa haki inatendeka na kuwatimua wahusika wote waliohusika.

Katika ziara ya viongozi hao jana, wahanga hao waliwaambia kuwa hawakula chakula chochote jana kwa kuwa walikuwa wameishiwa, ndipo Makamba alipowaahidi kuwapelekea chakula.
 
makamba kachapia big time!......hakuna aliyeliita suala la kisiasa hadi yeye alipotukumbusha.
sasa tutasema kwa vichwa vipana, walioboronga ni watu wa serikali waliowekwa na ccm. kwa hiyo lawama za ccm
 
Makamba,Chiligati,Lowassa,Rostam,Karamagi,Aggrey Mwanri,John Komba,...duh I wonder CCM walipata wapi vichwa hivi...kisha KadaMpinzani,Chinga,Dar Es Salaam...hawa nao watetezi wa CCM hapa JF...

Masatu uko wapi kaka muda huu ambapo CCM inazidi kuchemsha big time?I wonder even more ka nini CCM kinawatupa mbali makada kama wewe...

kwi kwi kwi kwi kwi!!! wacha watu tutulzie mzuka tuone hawa mafisadi jinsi wanavyotapatapa,balile yu wapi nae awasaidie kuwa PR wa CCM?maana naona yuko busy tu na mfadhili wake Rostam ilhali boti yao CCM inazidi kutoboka na kuingiza maji.
 
Never b4 did I think Tanzanians, resident in this great tranquil land would 1 day be leaving for work frm shacks, when they previously lived in the comfort of houses built by their own sweat!
Na wanalipa kodi ya kununua hilo gari la Makamba, na kulipia mafuta linalo guzzle!!
SAD :(
 
Makamba analeta siasa kwenye matatizo. Watu wanalala kwenye mahema kama wakimbizi, yeye anasema nendeni mkachukue viwanja vipya kama serikali ilivyowaambia, "nasi tunawashauri hivyo". Hajiulizi huko watalala wapi? si wataendelea kuwa kwenye mahema maana hawajalipwa. Wangekuwa wamelipwa wangeenda kujenga upya. Hiyo ni one side of the coin, the second ni kwamba Makamba inabidi awaeleze nini kitakachoendelea katika eneo la Tabata dampo iwapo wao watachukua viwanja vipya. Isije ikawa ni janja, wao wakishahama basi huyo anayedaiwa kutoa hongo anahamia hapo na mchezo unakwisha.
Wakazi wa Tabata dampo, nakubali kuwa hili suala si la kisiasa lakini naona Makamba mwenyewe analigeuza kuwa la kisiasa:.
“…… �Msikubali tatizo hili kuwa la kisiasa, kwani halikufanywa na CCM, ni tatizo la mtu mmoja wa ovyo,� alisema na kuongeza: �Najua watakuja watu hapa, watawaambia, oneni hiyo CCM.


Msiwasikilize. Sisi ndio wenye majibu, chama kingine hakina majibu ya matatizo yenu�. Alisema mtu anayewazuia kwenda kuchukua viwanja hivyo katika eneo hilo hawatakii mema. Hata hivyo, ushauri huo wa Makamba, ulianza kupingwa na Mjumbe wa Shina namba 16 wa CCM katika eneo hilo, Tauzani Mbwana, baada ya kupewa fursa ya kuzungumza katika mkutano huo.

Tatizo halikufanywa na CCM, hasemi limefanywa na nani eti mtu mmoja wa ovyo. Si amtaje huyo wa ovyo tumjue? Lakini tusiwe wajinga, mtu mmoja hawezi kubomoa nyumba zote hizo, lazima ni ring au syndicate, ni watu wengi wanaohusika,na hao lazima wawe ndani ya serikali na serikali ni ya CCM!!

Anasema CCM (Chama cha siasa) ndiyo ina majibu na majibu yenyewe ndiyo hayo - hameni mkachukue viwanja vipya na mengine mtadai taratibu (another siasa) Anayewaambia msihame hawatakii mema, ila anayewaambia hameni mtoke hapo mnapoonekana mwende pembezoni msikoonekana, huyo ndiye anawatakia mema (another siasa)
Makamba, Watanzania wa leo wameanza kuamka, siyo wale wa zamani wa ndiyo mzee. Tunakubali bado tu- wadanganyika, lakini udanganyika karibu unafika mwisho - KAA CHONJO
 
Never b4 did I think Tanzanians, resident in this great tranquil land would 1 day be leaving for work frm shacks, when they previously lived in the comfort of houses built by their own sweat!
Na wanalipa kodi ya kununua hilo gari la Makamba, na kulipia mafuta linalo guzzle!!
SAD :(

JK na Makamba wote CCM ni mbele kwao . Yaani wametokea kwenye CC ndipo wanashituka na kwenda pale Kichama .Makamba analeta siasa kwenye maisha ya watu .Anasema watu watakuja hapa nakusema.Yeye pale alienda kama nani ? Mbona hakuna kiongozi yeyote wa Kisiasa kafika pale kabla ama baada ya yeye ukiachia akina Kandoro wana CCM wenzake?
 
Tabata Dampo nyumba zilizovunjwa ni zipi? Ni hizi za upande wa pili wa dampo kama unaenda Bima Flats au ule upande wa Dampo? exactly wapi? Any pics?
 
Im lost..........Hilo eneo ndio palipokuwepo dampo?............au ndio kama lile tatizo la Jangwani?
 
Deleted...Moderators please delete this message.
 
Bubu

.....jaribu kuwa unaangalia vichwa vya habari vya mada hapa JF at least page ya kwanza........kwani ukiangalia utaona Mzee Murangira alishaiweka hii thread.

....mods please unganisha
 
Im lost..........Hilo eneo ndio palipokuwepo dampo?............au ndio kama lile tatizo la Jangwani?

Hivi wana JF hakuna mtu anaweza kupata picha za Tabata akatuwekea hapa tukajua eneno hili ni lipi ?
 
Bwana Porojo kakutana na kiboko yake! Lakini naona ana point fulani, wachukue hivyo viwanja halafu waendelee kulalamika. Waswahili husema "Hamadi kibindoni", "Ulicho nacho ndicho chako". Mie pia ningewashauri wapokee hivyo viwanja, na kwa sababu sasa hivi serikali bado inaandamwa na guilt consciousness, waibane iwapatie hati kabisa kila mmoja kwa jina lake. Wakishaziweka kibindoni, kibao kinabaki palepale kuwa hatuna pa kulala, nyumba zetu zimevunjwa tunadai fidia. Wanaendelea kupigana sasa kudai ama fidia na haki yao ya kubaki Tabata. Wakipata fidia lakini wakakosa haki ya kubaki hapo, sio mbaya wataitumia kujenga kwenye viwanja vipya.

Vita unashinda kwa kuteka hatua baada ya hatua, mtaa baada ya mtaa na kijiji baada ya kingine na si kusubiri kuteka mkoa mzima. Adui aki-retreat hatua kumi unakaba nafasi hiyo asirudi, ukisubiri aondoke maili mia atakuja gundua hata hizo kumi alizoondoka alikuogopa bure, anarudi na humuwezi tena! Akisonga nyuma unaongeza kibano hadi aachie kabisa.

Nawatakia watanzania wenzangu hawa kila la heri katika mapambano.
 
NI HUZUNI SANA......UKIWA KAMA HUMAN BEING UKIPITA PALE CHOZI LAWEZA MWAGIKA.......JUST SEE BINADAMU WENZAKE WANATESEKA KWA AJILI YA MTU MMOJA.......BIG UP KWA WENZETU WALIOONA MATESO YA HAWA WATU NA KUWASAIDIA ..........."ushauri" huyo mtu aliyepewa ardhi ya wengi yeye ndo apelekwe huko kwenye mashamba na watu hawa watafutiwe namna ya kusaidiwa na fidia officially.......!
 
Back
Top Bottom