Makamba Unalia nini ?Tabata wamzomea Makamba

Sasa wanamzomea nini wakati ikifika wakati wa kupiga kura wote wanachagua Chama Cha Majambazi(CCM) huku wakipiga vigeregere. Hizo NYUMBA zao zimevunjwa kutokana na sera bora za CCM zinazosaidia kila mwenye nacho. Waache tu waendelee kuvunjiwa nyumba zao na waishie kukaa kwenye mahema kwani waliyataka wenyewe.
 
Samahani Jamani, Kwani Makamba Ana Cheo Gani Siku Hizi? Na Alienda Kumuwakilisha Nani? Kwa Hiyo Makatibu Wakuu Wa Vyama Vyote Vya Siasa Tanzania Waende Hapo Tabata Na Kutetea Vyama Vyao Kwamba Haviusiki. Bongo Bwana!! Halafu Hakuona Hata Aibu Kuanza Kuongelea Mambo Ya Chama Hapoo? Mhmmm, Lakini Sitashangaa Kuona Bado Wanashinda Uchaguzi. God Bless Tanzania!!
 
Kwanza kabisa naomba kwa yeoyote mwenye CV ya makamba ailete hapa JF tuione.

Nawashauri waathirika wa Tabata wasichukue hivyo viwanja hadi kieleweke.Sasa kama watavichukua hivyo viwanja bila ya kuwepo muafaka,hizo gharama za ujenzi watazitoa wapi au wanapewa kama mapambo? na ktk A/C zao ni NIL balance.Serikali iwalipe kwanza.

Waathirika(WAMEDHARILISHWA) wanatakiwa kuishtaki Halmashauri ya Ilala kwa kosa la kuvunja nyumba za makazi yao kinyume cha sheria na baada ya hilo kwisha Serikali iwafidie maeneo yao kama itakua inayahitaji kwa sababu waathirika imeonekana walikua wanatambulika kisheria.

Makamba be CAREFUL
 
Jamani Hivi Ni Kwa Nini Tusipindue Nchi Ili Baada Ya Hapo Tuanze Kuheshimiana? Maana Yanayofanyika Tanzania Ni Kama Vile Nchi Isiyo Na Wenyewe Kila Siku Kukicha Ni Mambo Ya Hovyo Tu Tunashuhudia Yaani Kana Kwamba Hawa Watawala Hata Baada Ya Kuifilisi Tanzania Wakaona Haitoshi Na Hivi Sasa Wameamua Kuwachoka Watanzania
 
Hili linashangaza sana.Hivi hata Makamba darasa la nane anaweza kuwa mjanja kiasi cha kutudanganya hata sisi wana Forum?
Wananchi maskini wamevunjiwa nyumba ili deal la kuuza sehemu hiyo likamilike.Sasa Makamba anaposema wapatiwe viwanja kule Buyuni si ili kwamba viwanja sasa vipatikane kwa mafisadi wasio na huruma?
Tunaweza kudanganywa pengine na wengine sio wewe Makamba tunakufahamu saana tangu ukifundisha.Hela za ufisadihuo mbona zimeelekea Tanga, tafuteni ni za nani!!!
 
Jamani Hivi Ni Kwa Nini Tusipindue Nchi Ili Baada Ya Hapo Tuanze Kuheshimiana? Maana Yanayofanyika Tanzania Ni Kama Vile Nchi Isiyo Na Wenyewe Kila Siku Kukicha Ni Mambo Ya Hovyo Tu Tunashuhudia Yaani Kana Kwamba Hawa Watawala Hata Baada Ya Kuifilisi Tanzania Wakaona Haitoshi Na Hivi Sasa Wameamua Kuwachoka Watanzania

Although I do see the need for a political revolution,I do not see room for desperation leading to a military one.It is against the principles of reason.

Wanaotaka kupindua hawasemi kwenye public forums anyway.

What do you think this is anyway, 1-800-GET-INDICTED-FOR-TREASON hotline?
 
Pundit niliwahi kusema hapa kuwa haya ndiyo mambo yanayotushia heshima na kuharibu jina takatifu la JF. Nafikiri inabidi moderators wafanye kazi ya uhariri zaidi maana kuiacha post kama hiyo hapa ni kutudhalilisha sote humu kwa kuonekana hatuna akili. Tena huyu anayeandika huo utumbo inaonekana hata hajui maana ya maneno anayoyaandika. MoDs you need to censor these things, keeping silence only justifies what our foes contemplate about JF as well as their eventual actions! Responsibility and accountability should begin with us-and this starts by keeping our house in order so we can have the moral authority at raising our eyebrows at others.
 
Back
Top Bottom