BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,355
- 8,042
Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Tanzania inahitaji dola 150 milioni za Marekani (Sh345 bilioni) kwa mwaka kujenga uwezo wa kukabiliana na athari za mabadili-ko ya tabianchi.
Makamba amesema fedha hizo zinatakiwa kutumika kujenga uwezo katika sekta ya kilimo, afya, miundombinu, nishati na maji hivyo kuziomba nchi zilizoendelea na wabia wa maendeleo kufadhili mchakato huo.
Waziri amesema hayo leo Jumatatu, Septemba 5, 2022 katika mkutano wa viongozi wa dunia unaojadili Programu ya Afrika ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Africa Adaption Summit) unaofanyika Rotterdam nchini Uholanzi.
“Nina furaha kuwa Kituo cha Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi Duniani (GCA) na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) zimeungana kuiendeleza Programu ya Kuharakisha Afrika Ina-kabiliana na Majanga (AAAP) ya mabadiliko ya ta-bianchi ukiwamo Uviko-19, ukame, ukosefu wa ajira na mafuriko,” amesema.
Katika mkutano huo ulioongozwa na Rais wa Sen-egal, Macky Sally na Mwenyekiti wa GCA ambaye ni Katibu Mkuu smtaafu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-moon, Waziri Makamba alimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.
Lengo kuu la mkutano huo ni kuwashawishi washirika wa maendeleo, taasisi za fedha na sekta binafsi kuchangia dola 25 bilioni zinazohitajika mpaka mwaka 2025 kufanikisha kuitekeleza pro-gramu hiyo.
Mbali na hilo, Makamba amesema Tanzania inahitaji dola 14 bilioni kugharimia utekelezaji wa mpango wa Taifa wa kupunguza athari za maba-diliko ya tabianchi kiasi kinachotarajiwa kupanda hadi dola 30 bilioni mwaka 2030.
Mkutano huo umefanyika kabla ya mkutano wa 27 nchi Wananchama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika Misri hapo Novemba.