Makamba: Nilikuletea kimemo umpe dada yangu u-DC ukanikatalia

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,344
Leo mzee Makamba amenifurahisha sana kwa kusema ukweli kwamba alimpenyezea kimemo Rais Magufuli ili ampe ukuu wa wilaya jamaa yake.

Mzee Makamba ameonyesha ukomavu na ushujaa wa hali ya juu kutoa kauli ile hadharani ili tu kutuma picha ya hali ilivyokuwa imefikia ndani ya CCM, kwamba ujanja ujanja na undugunaizesheni ulikuwa ukifanywa hata na wakubwa.

Amethibitisha kauli ya mheshimiwa Rais kwamba kwenye mchakato wa kuteua wakurugenzi wa maendeleo alitumiwa vimemo na watu na wengine wazito kabisa ili awape upendeleo watu wao lakini akawakatalia na wakati mwingine akiwatupilia mbali wao na wale waliokuwa mawakala wao.

Kwa kweli bila kumung'unya maneno safari hii Tanzania tuna Rais.
 
Mtanzania ni mrahisi kudanganywa kuliko mbwa. Sasa wewe wanasiasa wanapiga porojo zao na wewe kichwa kichwa umeingia kama panya buku! Chemsha akili walau kidogo...
 
Jamani ule ni ujumbe kwa magufuli akubali kushauriwa ila umefikishwa kwa njia ya picha inasemekana mgumu kupokea ushauri wazee wamemzunguka. Na ndivyo vitu wanavyoviogopa ccm jamaa HASHAURIKI.
 
amjambo wana Jamvi?

najua mtakuwa mefatilia mdebwedo wa uchaguzi wa mwenyekiti wa ccm Taifa, kuna mengi yamesemwa ila Mzee Makamba ameoensha dhaili kuwa yeye ni sehemu y tatzo la vimemo, tatzo lilirokuwa limeitafuna nchi yetu.

ila kwa upande mmoja tumeweza jua kuwa January Makamba fursa aliyokuwa nayo enzi hizo mpaka aliyonayo hivi leo ni nguvu ya vimemo, kutoka kwa Babake kwenda kwa rais Kikwete enzi hizo.

kwa kuwa alikubaliwa,ameendeleza tabia zake za kishenga ndani ya ikulu, akataka dada yake apewe

U-DC chinja chinja ya vimemo imekuta Ikulu ipo mikononi mwa Msukuma, kudadeki kimemo sjui kimetupwa wapi?

Bira kimemo, Makamba January angekuwa wapi?
 
Back
Top Bottom