Makamba: Majadiliano na Wawekezaji wa Mradi wa Gas Til.70 yakamilika, Mkataba wa Ujenzi kusainiwa wakati wowote

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,992
49,655
Habari Wakuu

Serikali imesema imekamilisha majadiliano na wawekezaji wa mradi wa usindikaji wa gas asilia LPG wa Lindi wenye thamani ya shilingi Til.70 za Tanzania.

Waziri wa Nishati January Makamba amesema kinachosubiliwa Sasa ni nyaraka za utiaji saini ambapo wakati wowote kutoka Sasa mkataba utasainiwa na ujenzi utaanza rasmi kama ilivyopangwa..

Hongera sana Makamba endelea kuwapoteza wakosoaji wako na kuandika legacy ya Yako na Ya Mama..
Til.70 sio mchezo,tukipata walau til.15 kutoka humo basi ni boost kubwa sana ya Uchumi Wetu na itajengwa Imani kubwa Kwa uwekezaji mwingine mkubwa zaidi kutoka Kwa wawekezaji wengine..

-----
MAJADILIANO MRADI WA KUCHAKATA NA KUSINDIKA GESI ASILIA (LNG) YAKAMILIKA

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba, amesema kuwa, majadiliano yanayohusu Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia baina ya Serikali ya Tanzania na wawekezaji Kampuni ya Shell ya Uholanzi na Equinor ya Norway na washirika wao yamekamilika na kwamba sasa wataalam wapo katika kazi ya kuandika mikataba ya mradi huo.

Waziri wa Nishati ameyasema hayo tarehe 06 Machi, 2023 jijini Arusha wakati akitoa vipaumbele vya Wizara katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati ambapo pamoja na masuala mengine ya kiutumishi, Baraza hilo limepitia Mpango wa Bajeti wa Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/2024.

“Mazungumzo ya mradi huu wa LNG yamekamilika na wataalam kwa sasa wanaandika mikataba mikubwa miwili yenye masuala mengi ikiwemo ya kiufundi, Mkataba mmoja ni wa Nchi Hodhi (HGA) na mwingine ni mkataba uliounganishwa wa vitalu vya Gesi Asilia Namba I,II na IV ambavyo gesi yake itatumika kwenye mradi wa LNG, kila mkataba una takriban kurasa zaidi ya 600, hii si kazi ndogo ila nimewasisitiza wamalize kazi mwezi huu ili kuweza kuendelea na hatua nyingine za utekelezaji.” Amesema Makamba

Amesema kuwa mradi huo ambao uwekezaji wake ni zaidi ya Shilingi Trilioni 70 utaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi nchini na utaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazochangia katika usalama wa nishati duniani hivyo amewataka Watendaji wa Wizara ya Nishati kuendelea kusimamia utekelezaji wa mradi huo.

Makamba ametaja mradi mwingine unaoendelea kutekelezwa ni wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania ambapo kwa sasa shughuli mbalimbali za maandalizi ya ujenzi zinaendelea na mwezi uliopita Serikali imetoa kibali cha ujenzi wa bomba hilo kwa kampuni ya EACOP na kwa sasa inaendelea kukamilisha taratibu za kupata pesa za kutekeleza mradi huo ambazo zimefikia mwishoni.

Ameongeza kuwa, zoezi la ulipaji fidia kwa watu 9800 katika mkuza wa Bomba la mafuta zinaendelea ambapo mpaka sasa shilingi Bilioni 29.2 zimelipwa kati ya shilingi Bilioni 30 zilizokuwa zinahitajika kwenye ulipaji fidia na matarajio ni kwamba ujenzi unatarajiwa kuanza kabla ya mwisho wa mwaka huu.
 
Historia inakaribia kuandikwa,mradi huu utafungua milango ya wawekezaji wengine wakubwa Duniani na utakuwa mradi wa uwekezaji mkubwa Afrika na Duniani.

Wanaripoti The Reuters
 
Habari Wakuu
Serikali imesema imekamilisha majadiliano na wawekezaji wa mradi wa usindikaji wa gas asilia LPG wa Lindi wenye thamani ya shilingi Til.70 za Tanzania..

Waziri wa Nishati January Makamba amesema kinachosubiliwa Sasa ni nyaraka za utiaji saini ambapo wakati wowote kutoka Sasa mkataba utasainiwa na ujenzi utaanza rasmi kama ilivyopangwa..

Hongera sana Makamba endelea kuwapoteza wakosoaji wako na kuandika legacy ya Yako na Ya Mama..
Til.70 sio mchezo,tukipata walau til.15 kutoka humo basi ni boost kubwa sana ya Uchumi Wetu na itajengwa Imani kubwa Kwa uwekezaji mwingine mkubwa zaidi kutoka Kwa wawekezaji wengine..

Ni hatua nzuri

Mimi sitamlaumu Makamba wala Mama kwa any wrongdoing ya mradi huu.

Nitawalaumu Usslama Wa Taifa endapo kuna uozo unafichwa. Tuambiwe kwa namna yeyote jambo ambalo halipo sswa. Labda waamue kuunga juhudi za kuifilisi nchi

Maendeleo ni hatua. Hatuwezi kupinga kila kitu bali tunapinga utendaji na utaratibu mbovu unaogubika deals nyingi za serikali.

Tunahitaji financial muscles na miradi kama hii itupeleke huko. Lakini iwe miradi inayokidhi MASLAHI YA TANZANIA na siyo wachache bali sote tuonje keki ya Taifa kupitia projects maridhawa za serikali
 
Kwa hiyo Hawa qanaoripoti hawana uhakika ila wewe hapo au?
Acha kujisahaulisha bana wanasiasa wetu tunawajua when it's come to public popularity..!
 
Gesi itaisha kuchukuliwa bado watt wetu wanakaa chini ama wapo Mia darasa moja na mwalimu mmoja wa hesabu ama fizikia shule nzima ya wtt 2000+.

Pia bado zahanati zitakuwa hazina vitendea kazi na bado road za bush hazitakuwa rafiki kwa mkulima kusafirisha mazao mpaka kwa walaji.

Bado tutakuwa tunakopa kopa na tozo zitakuwepo Kama kawa.

Hapa msogwa Wana fungu lake la Mana Kama hawatajenga hotel ama apartments huko Europe sidhani Mana February Yuko hapo kwa maelekezo tokea chalinze. Cheki Ile timu chalinze ndio iko madarakani wale wa 2005-2015 Sasa utaongea Nini.

Yaani raslimali za Taifa zinaliwa na watu wachache mno yaani wanaishi kianasa kinyama huku down wanahenyeka Kama punda.

Watalaamu wa mafuta na gesi labda watapata Ajira. Kusaini na utekelezwaji Ni kazi mbili tofauti.

Hiii ishu ingekuwepo jpm nadhani Taifa lingenufaika. Mana jamaa akaingia lami zikafika ambapo hazijawahi fika tokea kuumbwa kwa dunia
 
Ni hatua nzuri

Mimi sitamlaumu Makamba wala Mama kwa any wrongdoing ya mradi huu.

Nitawalaumu Usslama Wa Taifa endapo kuna uozo unafichwa. Tuambiwe kwa namna yeyote jambo ambalo halipo sswa. Labda waamue kuunga juhudi za kuifilisi nchi

Maendeleo ni hatua. Hatuwezi kupinga kila kitu bali tunapinga utendaji na utaratibu mbovu unaogubika deals nyingi za serikali.

Tunahitaji financial muscles na miradi kama hii itupeleke huko. Lakini iwe miradi inayokidhi MASLAHI YA TANZANIA na siyo wachache bali sote tuonje keki ya Taifa kupitia projects maridhawa za serikali
Na hao usalama ni binadamu vile vile,wanaangalia upepo
 
Onyesha akili zako zilipo kwanza
Ndio mnapoharibu na kujionyesha kwamba wala hakuna mnachokijua sema mnatumiwa tu kuuandika maujinga ya wakubwa wenu humu, halafu hamna hata nguvu ya kuutetea huo ujinga.

Kamuulize hivi, mradi wa BLN 70 gas yetu kila kitu chetu wao wanakuja tu na mitambo yao, halafu tuambulie BLN 15 tu ni sawa?
 
Gesi itaisha kuchukuliwa bado watt wetu wanakaa chini ama wapo Mia darasa moja na mwalimu mmoja wa hesabu ama fizikia shule nzima ya wtt 2000+.

Pia bado zahanati zitakuwa hazina vitendea kazi na bado road za bush hazitakuwa rafiki kwa mkulima kusafirisha mazao mpaka kwa walaji.

Bado tutakuwa tunakopa kopa na tozo zitakuwepo Kama kawa.

Hapa msogwa Wana fungu lake la Mana Kama hawatajenga hotel ama apartments huko Europe sidhani Mana February Yuko hapo kwa maelekezo tokea chalinze. Cheki Ile timu chalinze ndio iko madarakani wale wa 2005-2015 Sasa utaongea Nini.

Yaani raslimali za Taifa zinaliwa na watu wachache mno yaani wanaishi kianasa kinyama huku down wanahenyeka Kama punda.

Watalaamu wa mafuta na gesi labda watapata Ajira. Kusaini na utekelezwaji Ni kazi mbili tofauti.

Hiii ishu ingekuwepo jpm nadhani Taifa lingenufaika. Mana jamaa akaingia lami zikafika ambapo hazijawahi fika tokea kuumbwa kwa dunia
Watu wenye mawazo negative mna shida sana, hata maisha yenu ni ya tabu hivyo hivyo..

Kwa hiyo gas isipovunwa ndio Watoto wenu watakaa kwenye meza mandawati au?
Kinachozuia Watoto wasikae kwenye meza na dawati unakijua?
 
Ndio mnapoharibu na kujionyesha kwamba wala hakuna mnachokijua sema mnatumiwa tu kuuandika maujinga ya wakubwa wenu humu, halafu hamna ata nguvu ya kuutetea huo ujinga.

Kamuulize hivi, mradi wa BLN 70 gas yetu kila kitu chetu wao wanakuja tu na mitambo yao, halafu tuambulie BLN 15 tu ni sawa?
Acha hadithi, onyesha akili zako zilipo kwanza.
 
Watu wenye mawazo negative mna shida sana,hata maisha yenu ni ya tabu hivyo hivyo..

Kwa hiyo gas isipovunwa ndio Watoto wenu watakaa kwenye meza mandawati au?
Kinachozuia Watoto wasikae kwenye meza na dawati unakijua?
Your biasennes, subjectivity, opinions, beliefs, thinking and assumptions aren't universal. You aren't objective in your thinking. May you prove it.
To be positive in negative situations is also negativity
 
Ni prove nini? Jibu hoja zangu kwanza hapo Juu Kwa swala uliloliibua.
 
Back
Top Bottom