Makamba kupongezwa, kuzindua shina mishemishe group Kariakoo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba kupongezwa, kuzindua shina mishemishe group Kariakoo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ustaadh, Jan 5, 2011.

 1. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Kariakoo Kaskazini, Kata ya Kariakoo, kimeandaa sherehe ya kumpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kwa uongozi wake uliotukuka ndani ya chama hicho.

  Sherehe hizo zitakazoambatana na uzinduzi wa shina la wakereketwa la Mishemishe Group, zitafanyika Jumamosi, ijayo kuanzia saa 9.00 mchana hadi saa 12.00 jioni katika eneo linalotazamana na kituo cha Polisi Msimbazi katika makutano ya mtaa wa Msimbazi na
  Jangawani.

  Mratibu wa sherehe hiyo, Shehe Majid Saleh alisema jana kuwa wapo viongozi wengi waliofanya vizuri, lakini wameamua kumzawadia yeye kwa kuwa wamemuona Makamba ni mtu makini, barabara, msema kweli na hatetereki katika uamuzi wake.

  Alisema kuwa Makamba atakabidhiwa tuzo maalumu na shina hilo na hati ya uongozi uliotukuka aliouonesha katika wadhfa huo na pia wazee wenzake watamkabidhi zawadi maalumu.

  Baada ya uzinduzi wa shina hilo lenye wakereketwa walio katika kikundi cha mama lishe na baba lishe cha watu 30 ambao wamekuwa wakijikwamua kiuchumi, Makamba atakabidhi kadi 300 kwa wanachama wapya wa CCM.

  ........................
  HONGERA NDUGU MAKAMBA!
   
 2. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  makamba, werevu mwingi mbele giza, uongoza uliotukuka wa kifisadi, katibu na mshauri wa mfalme juhaa
   
 3. n

  nndondo JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Ama kweli watu wanajua kujikomba, hivi huyo ni shehe wa ukweli anayemuogopa mungu, ama ni shehe wa kanzu? Huo utumishi wa kutukuka wa makamba uko wapi? Mimi ni kada mzuri sana wa ccm sasa huyo anayemfanyia makamba evaluation ni nani? Chama chetu hakijwahi kupata kiongozi mpuuzi, asiye na uwezo, asiyoe na maono, asiye na elimu kama huyu. Na hata mwenyekitiw ake anajua kinachomuweka ni uchawi tu aliomzidi bosi wake
   
Loading...