Makamba,Karembo,DC Kilosa,hii aibu!

Konzogwe

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
434
155
Ktk mapumziko yake pale Mikumi Morogoro mwisho wa mwaka 2007,Mkt CCM Taifa alikutana na tatizo sugu la kampuni ya maji ambalo lilipelekea apige simu kwa aliyekuwa waziri mkuu (LOWASSA) naye akampigia RPC Karembo naye akapiga kwa DC Kilosa na OCD. Basi mashangingi yakakutana pale veta mikumi kujadili swala hilo na akiwepo Hakimu mfawidhi wa wilaya bw Ndimubenya na kuamuru uongozi wa maji wa zamani uliokataliwa na wananchi usijihusishe na shughuli za maji kwani tayari kuna uongozi mpya uliowekwa kwa kufuata taratibu zote chini ya usimamizi wa serikali ngazi zote. Ajabu maamuzi ya hao waheshimiwa yamepuuzwa na huyu bwana ZUNDA asiyetakiwa anaendelea kukusanya pesa na yeyote anayekataa kulipa kwa uongozi huo ulioondolewa madarakani,bas anaenda jela. Had sasa ni wawili wamefungwa akiwemo mkt wa kijiji!...jamani maamuzi yenu yalikuwa batili?? Au je,mmewasaliti wanamikumi?? Wapenda haki si wataishia jela? Au hapo napo aende Mwakyembe? Ni aibu hii.
 
Back
Top Bottom