Makamba Jr, Deo Filikunjombe, Dr. Kigwangalaah, Lugola wote ni wazee hawafai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba Jr, Deo Filikunjombe, Dr. Kigwangalaah, Lugola wote ni wazee hawafai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Precise Pangolin, Apr 14, 2012.

 1. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 11,827
  Likes Received: 1,273
  Trophy Points: 280
  Imenichukua muda mrefu kupata maana halisi ya neno uzee nilichogundua hata ukiwa na mawazo ya kizee hata Kama una umri wa miaka 18 wewe ni Mzee tuu. Hao niliowataja ni Kati ya wabunge waliopata kura kupitia Chama cha magamba kwa muonekano wa ujana lakini wamekua ndio wa kwanza kumpinga mnyika kwa kusema ndiyooooooo bungeni bila ya kusimama kutetea hoja au kupinga hoja kwa fact.Nashauri 2015 tusiwape kura zetu tena hawatufai ni wezi wa haki za watanzania Kama baba zao tu Pambaf!!!!!
   
 2. K

  Keil JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nilishasema na ninarudia kusema kwamba ndani ya CCM hakuna Wazee wala Vijana, wote wapo pale kulinda maslahi ya chama.

  Deo Filinkunjombe na Alphaxard Lugola walikuwa mstari wa mbele kupinga ufisadi unaofanyika kwenye mashirika ya umma. Lakini Mbunge anapokuja na hoja nzuri ya kutunga sheria ya kudhibiti matumizi mabaya ya fedha, wanakuwa wa kwanza kukataa.

  Kitendo cha mashirika ya umma kutopitisha bajeti zao bungeni kunasababisha wawe na matumizi mabovu. Matokeo yake POAC inapokuja kupita kukagua inakuta madudu, na wao hawana mamlaka ya kisheria kuwachukulia hatua viongozi wa hayo mashirika. CAG kila siku anaanika madudu yanayofanyika kwenye hayo mashirika na hakuna anayechukuliwa hatua.

  Bajeti za mashirika ya umma zinapitishwa na Bodi, wajumbe wa Bodi za mashirika manono kila wakikutana wanashikishwa mshiko wa kueleweka na kuna mashirika mengine wanapewa mpaka monthly allowances. Hata ATCL iliyokuwa chovu, ilifika mahali ikampa ofisi Mwenyekiti wa Bodi, as if anasimamia shirika on daily basis. Sasa bodi kama hizo hata kama wanaona kuna madudu, hawawezi kuuliza.

  Tuliona madudu ya BOT jinsi wajumbe wa Bodi walivyokuwa wanajidhalilisha kwenye ufisadi uliokuwa unadaiwa kwamba ulifanywa na Liyumba. Mahakama inawauliza, je mlipitisha? Mara oooh tulikuwa tunaletewa maamuzi ambayo yalishafanyika, hata kama yalishafanyika, kwanini mkubali kupitisha kitu ambacho ni madudu?

  Hizi Bodi mara nyingi huwa ni ulaji tu, hawana lolote la maana, wakati mwingine naona ni bora hata mashirika yakasimamiwa na Bunge kuliko kusimamiwa na Bodi. Maana Bodi ina wajumbe wachache sana, so ni rahisi sana kupofushwa/kuhongwa na matokeo yake wanapitisha kila kitu bila hata kuhoji.

  Finally, sakata la Jairo lilitufungua macho kwamba Wizara/Serikali inaweza kuagiza kwamba wanataka fedha kiasi kadhaa na zikatolewa bila kufuata utaratibu. Lakini kama bajeti zao zingekuwa zinapitishwa na Bunge angalau kungekuwa na woga kwamba Mkurugenzi anakuwa responsible kutoa maelezo kwa Bunge kwamba kwanini alitumia fedha ambazo hazijaidhinishwa na Bunge.
   
 3. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ulitegemea magamba wawakane magamba wenzao.
   
 4. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,028
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Like father like son
   
 5. Kijana leo

  Kijana leo JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,872
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  kuna wakati inabidi wasimamie ilani yao ya chama chama chao, ila wakiwa pembeni wanajifanya wapiganaji, 2015 kila m2 atauchukua mzigo wake mwenyewe.
   
 6. K

  Kikulacho Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 29, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Yaelekea wewe ni mpuuzi kabisa hata vijana huwajui na leo hii unawatai wazee kina Deo Filikunjombe duh we mwehu kweli, nenda shule na yaelekea hujajipanga katika hoja yako, Deo Filikunjombe ni Kijana nasi wana Ludewa hadi tuseme basi naona wewe umetumwa na Pindi Chana, kuja kuchafua hali ya hewa hapa JF.
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 11,827
  Likes Received: 1,273
  Trophy Points: 280
  Amekutuma umtete siyo atapiga tena magoti kuomba kura lakini hapati
   
 8. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwanza hawa jamaa walipita kimagumashi tu,2015 kula pesa piga chini ndio utakao kuwa wimbo nchi nzima.
   
Loading...