Makamba Jr: CCM iko imara vyuo vikuu nchini

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), January Makamba, amesema chama hicho hakijatengwa na vijana wa elimu ya vyuo vikuu kama inavyosemwa na wapinzani. Makamba, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, alitoa kauli hiyo wakati akifungua kongamano la vijana ambao ni wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa vyuo vikuu.

Alisema tofauti na hoja zinazoenezwa na wapinzani kwamba vijana wengi, hususani wa vyuo vikuu hawaiungi mkono CCM, hawawezi kutishwa na maneno hayo ya mtaani.

“CCM bado kinawathamini vijana na ndiyo maana wanaendelea kukiunga mkono, umati huu unadhihirisha kwamba hatujapoteza umaarufu wetu katika vyuo vikuu nchini, wenzetu wanaoeneza propaganda hii wamepotoka.

“Wenzetu wanawatafuta na kuwajenga vijana katika dhana ya kuhatarisha amani, CCM tunataka vijana washiriki na kujadili siasa ya nchi yao nje ya vyuo,” alisema Makamba.

Alisema CCM ndiyo msingi wa amani ya nchi kwa sababu kimejenga msingi huo kuanzia kwa vijana wa chipukizi ambapo vijana wadogo wanafundwa uzalendo kwa nchi yao.

Katika kongamano hilo, makada mbalimbali wa CCM waliwakumbusha vijana hao wasomi kutobweteka na kuwaachia wenzao wa upinzani kutamba katika mitandao ya kijamii kwa kutoa hoja za kuupotosha umma kuhusu Serikali inayoongozwa na CCM.

Katika hatua nyingine, Kamanda mteule wa Umoja wa Vijana, Kata ya Kitunda, Godfrey Obonyo, alitoa msaada wa samani mbalimbali kwa ajili ya ofisi hiyo.

Katika makabidhiano hayo, Obonyo, aliwaasa vijana kuvitumia vifaa hivyo kwa ajili ya maendeleo ya chama na si vinginevyo.

Aidha, aliahidi kuwaunganisha vijana katika kampuni mbalimbali waweze kupata miradi ya kujitegemea na kuepuka na adha ya kutokuwa na ajira za kuaminika.

habari Mtanzania Jumapili.

baadhi ya picha za mkutano.
 
Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    128 KB · Views: 180
  • image.jpg
    image.jpg
    184.7 KB · Views: 202
  • image.jpg
    image.jpg
    209.5 KB · Views: 243
Kelele za chekechea wa kisiasa hazimzuii mtu mzima kuendelea na shughuli zake.

Wao wamebakiwa na cheap politics zinazokolezwa na spinning za kijinga na siasa zilizopitwa na wakati za kueneza sera zao za kutaka kufahamu nani ni msagaji na nani siyo msagaji.

waacheni waendelee na siasa zao za kilaghai, maji taka na kumwagia watu wasio na hatia tindikali.

Makada tuko busy tunafanya kazi tuliyotumwa na wananchi kupitia sanduku la kura 2010.

CCM tumedhubutu, tumeweza na sasa tunatenda.
 
Msomi mzima anashindwa utoa data kwenye speech yake, upuuzi mtupu back to the point, CCM haikubaliki anajidangya na kuwadanganya wengine, juzi kuliuwa na uchaguzi pale chuo cha usimamizi wa fedha, habari zilizokuwa zikisikika ni kuwa kuna wagombea wa uraisi wa serikali ya wananfunzi walipewa pesa mingi na CCM ili kufanikisha campaign lkn mwisho wa siku hao jamaa waliopewaa support na CCM walipigwa chini vibaya sana na kwa maana hy CCM ilishindwa harakati zake!

awadanganye wasiojua hali halisi, lkn ukweli ni wamba huko vyuo vikuuu ndo hawana chao.
 
Kesi yake ya uchochezi uliopelekea uharibifu wa mali za kiwanda cha majani ya chai cha Lushoto (tamka Ushoto) vipi ilishafunguliwa Mahakamani? Au wenye kiwanda wameshalipwa fidia za uharibifu na suluhu kupatikana nje ya Mahakama? Mlioko Ushoto tujuzeni basi.
 
Mkuu tumekusoma rai kwa viongozi wa ccm waendelee kuwatatulia vijana changamoto zinazowakabili vijana wanakipenda chama cha mapinduzi.
 
kujadili siasa nje ya vyuo?? inaonekana wazi kuwa makamba jr. anaitaji short course ya civics education. kuhusu kuwatafutia vijana ajira unasubiri mkutano wa ccm vijana kulisema hilo ?? mimi ningelikuwa ni yeye ningekwenda kuanza kwanza na vijana asilimia karibu 90 ya jimboni kwangu ambao hawana kazi
 
Msomi mzima anashindwa utoa data kwenye speech yake, upuuzi mtupu back to the point, CCM haikubaliki anajidangya na kuwadanganya wengine, juzi kuliuwa na uchaguzi pale chuo cha usimamizi wa fedha, habari zilizokuwa zikisikika ni kuwa kuna wagombea wa uraisi wa serikali ya wananfunzi walipewa pesa mingi na CCM ili kufanikisha campaign lkn mwisho wa siku hao jamaa waliopewaa support na CCM walipigwa chini vibaya sana na kwa maana hy CCM ilishindwa harakati zake!

awadanganye wasiojua hali halisi, lkn ukweli ni wamba huko vyuo vikuuu ndo hawana chao.
Niambie kwanza upo mkoa gani kabla sijajibu hii hoja yako ya uongo,unaongea habari za kusadikika.
 
Ccm vyuoni kama kawa tupoo tumejaaa kama nini. Mtabaki na hayo majungu but ukweli ndiyo huooo.
 
Ukiona mwanachuo ni muumini wa magamba ujue ni maslai si unajua baada ya chuo ajira ngumu.
 
Ni aibu na ujinga wa hali ya juu kijana mwenye akili timamu kuishabikia CCM....labd uwe na akili zi kijinga ndo utaishabikia CCM....lakin kama kijana ni mzalendo,ni timamu kuishabikia CCM ni kujidumaza na kudumaza taifa....UNawashabikia hwa wakina makamba ambao hwajui maisha ninini...wamekulia magorofani...hajui hata bei ya chumvi...ndo maana unaona hapo anasema CCM imewaletea maendeleo vijana...yeye anafikiri alivyoendelea ndo vijana wote wapo hivyo....
 
Vyuo vikuu au vyoo vikuu? Is that supposed to be some benchmark or something?

Vyuo vyenyewe vipi? Hawa watoto wa UDSM/ UDOM?
 
Without seeing vivid examples and possible data to support an argument, I only discover political heritage from this guy! I realized the truth of Dr.Kitima's proposition that shameful death of CCM is nearby 2015. He was the VC of SAUT-MWANZA and he argued with situational analysis from intellectual experiences, how about Makamba Jr?
 
Siasa ni kama makanisa kila mtu anaenda anakoamini. Kwani akina Mbowe wamekulia wapi? Kama c mgrfn! Na elimu yangu nije chadema nianze kupelekwapelekwa na kupigishwa viroba! Akaa!
 
Kelele za chekechea wa kisiasa hazimzuii mtu mzima kuendelea na shughuli zake.

Wao wamebakiwa na cheap politics zinazokolezwa na spinning za kijinga na siasa zilizopitwa na wakati za kueneza sera zao za kutaka kufahamu nani ni msagaji na nani siyo msagaji.

waacheni waendelee na siasa zao za kilaghai, maji taka na kumwagia watu wasio na hatia tindikali.

Makada tuko busy tunafanya kazi tuliyotumwa na wananchi kupitia sanduku la kura 2010.

CCM tumedhubutu, tumeweza na sasa tunatenda.

Wewe pia kada? Kujipendekeza kwingine aibu
 
Ukiona mwanachuo ni muumini wa magamba ujue ni maslai si unajua baada ya chuo ajira ngumu.
You just hit the point.
Ni kichaa pekee atakaye kuwa kwenye chama cha siasa ambacho hategemei kupata maslahi achilia mbali mwanachuo.

Hii ndiyo dhana nzima ya vyama vya siasa kuuza sera zao kwa wananchi ili wananchi wapime na kuchambua kipi chama kitakacho waneemesha kisiasa, kijamii na kiuchumi (kimaslahi).

Kama unashangaa kwa nini vijana wengi wako CCM, basi inabidi na wao wakushangae kwa kushangaa jambo ambalo ni CRYSTAL CLEAR.
 
Msomi mzima anashindwa utoa data kwenye speech yake, upuuzi mtupu back to the point, CCM haikubaliki anajidangya na kuwadanganya wengine, juzi kuliuwa na uchaguzi pale chuo cha usimamizi wa fedha, habari zilizokuwa zikisikika ni kuwa kuna wagombea wa uraisi wa serikali ya wananfunzi walipewa pesa mingi na CCM ili kufanikisha campaign lkn mwisho wa siku hao jamaa waliopewaa support na CCM walipigwa chini vibaya sana na kwa maana hy CCM ilishindwa harakati zake!

awadanganye wasiojua hali halisi, lkn ukweli ni wamba huko vyuo vikuuu ndo hawana chao.

NDOTO ZA MCHANA, Apatiwe idadi ya wanavyuo wote waliko karibu na eneo hilo aliko na aangalie waliomo humo ndani ni asilimia ngapi?. Tena sio wote walioko humo ndani wanaipenda pale wanawinda mafungu na fursa za kupunguza ugumu wa maisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom