Makamba haogopi mtu ndani ya CCM isipokuwa JK na Msekwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba haogopi mtu ndani ya CCM isipokuwa JK na Msekwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 13, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,731
  Trophy Points: 280
  Imetolewa mara ya mwisho: 13.11.2008 1119 EAT

  • Kabwe afurahia sitofahamu CCM

  Na Said Mwishehe
  Majira

  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Bw. Zitto Kabwe amesema anafurahishwa na hali ya mvurugano inayoendelea ndani ya Chama chaMapinduzi (CCM) na hasa kauli zinazotolewa NA Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Yusuph Makamba.

  Kauli ya Bw. Kabwe imekuja siku moja tu baada ya Bw. Makamba kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema haogopi mtu yeyote ndani ya chama chake zaidi ya Mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Bw. Pius Msekewa.

  Makamba alitoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa za baadhi ya wabunge wa CCM kutaka kujenga hoja ya kumng'oa kwenye wadhifa wake wa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa madai kuwa amekuwa akikumbatia watu wasio na uwezo wa kukisaidia chama hicho.

  Akizungumza na Majira jana Dar es Salaam, Bw. Kabwe alisema kwa hali halisi CCM ipo katika wakati mgumu na hata kauli za Bw. Makamba zinaashirisha wazi kuwa hali ni mbaya ndani lakini yeye anapenda kuona hali hiyo ikiendelea.

  "Kitu ambacho kinaonekana hapa ni kwamba CCM sasa mambo ni magumu ndio maana hata viongozi wameanza kutupiana vijembe. Binafsi na CHADEMA kwa ujumla tunaomba hali hiyo iendelee na ikiwezekana mpasuko na mgawanyiko wa wanachama uwepo," alisema.

  Alisema kwa bahati mbaya hata siku moja hawezi kuiombea mema CCM na hali inayojitokeza sasa ni dalili kwamba hali yake itafanikiwa na CCM kusambarika.

  "Nilishatangaza hadharani kwamba CCM siipendi na nitafurahia kila aina ya jambo ambalo linaweza kusababisha mpasuko. Ndio maana ninasema kauli za Bw. Makamba ni bora zikaendelea kwani ndio mafanikio kwetu," alisema Bw. Kabwe na kuongeza kwamba ili demokrasia iweze kukua nchini lazima CCM isambaratike.

  Wakati Bw. Kabwe akiomba hali hiyo iendelee ndani ya chama hicho, baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na Majira kuhusu kauli za Bw. Makamba walisema inasikitisha kusikia kiongozi wao akitoa kauli za aina hiyo.

  Walisema kwa hali ilivyo sasa wao wanaogopa kutoa maoni yao kuhusu kauli za Bw. Makamba na kusisitiza kuwa wanaamini chama chao kina maadili hivyo vipo vikao ambavyo vinaweza kutumika kumjadili.
   
 2. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  bora aendelee kuharibu hivyo hivyo mpaka mwezi wa 2010 tuwapige chini. nguvu ya chadema tarime ijiandae kuhamia mbeya kwenye jimbo lililoachwa wazi.
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Nadhani katibu anajeuri ya kusema aliyosema, hawezi kusema hivi hivi tu bila sababu. Nafasi yake si ya kuchaguliwa ni ya kuteuliwa kwa hiyo kuwepo kwake kunategemea uamuzi wa mwenyekiti aliyemteua. Lakini ni aibu sana kwa kiongozi mkuu wa chama kutoa kauli kama hizo. Kwenye wakati huu mgumu kabisa wa chama alitakiwa kusimama kidete kuunganisha wanachama na sio kutoa kebehi na vitisho, nadhania atashangaa sana na yeye akiambiwa kuwa hawatishiki naye.
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  mASIKINI mAKAMBA MAANA MUDA UMEMPITA....CHAMA SI KILE ENZI ZA KIDUMU CHAMA CHA.............NA FIKRA ZA MWENYEKITI....PUMZIKA BABU MAKAMBA
   
 5. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Makamba aende akacheze Msondo..
   
 6. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2008
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kweli anakumbatia watu wasio na uwezo au yeye mwenyewe ndiye hana uwezo???? Au ni yote mawili.

  Bora wafarakane ili wawape nguvu wapinzani 2010!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mbona hamuogopi makamu mwenyekiti ZNZ lol??? Makamba anapenda kuongea vapour.. Manji alimnunulia nyumba yake ya serikali akiwa RC.. He is corrupt. He is Old and he is not too smart.. Uchawi tuu..
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ukiwa katibu mkuu wa chama unawajibika kwa nani?... Naona hapa watu wanachangia utumbo tu...
   
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Nov 14, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mwenyekiti or CC.. sjui but the constitution ya ccm should say... corruption ni utumbo?
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0

  Katika "strategic politics" Ukiisha tangaza hadharani kuwa wewe kama mpinzani unafurahia hali fulani katika chama kingine basi tunakuhesabu kuwa ume fail. Haikutakiwa kusema hadharani, kwani ni kuwaamsha na kuwafanya watafute solution mapema kabla mambo hayajawa mabaya. Ningekuwa mimi Kabwe ningekaa kimya tu naangalia jinsi ngoma ya mchezo inavyoenda bila kuwashika mkono. Hapa ni kwamba tayari CCM wataungana haraka sana kwa kauli kama hizi za kina Kabwe.
   
 11. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba hata ukiwaamsha haijalishi sana. Its too late. Hawa jamaa watakuwa wamekumbuka shuka kukiwa kumekucha kabisa. Yale mabaya yote ambayo watanzania wameyaona kuhusu serikali inayoongozwa na CCM yanatosha kabisa kusema sasa basi. Tumeona hali ya rushwa ya hali ya juu, ufisadi, mikataba feki na migomo kila siku. Kwa kila mtanzania mwenye akili, hii ni sababu tosha kabisa ya kuipiga CCM chini come 2010. Sio lazima Zitto atukumbushe kwamba CCM haifai. Tumeshajionea hali wenyewe na tutachukua hatua zinazostahili. Hili la mfarakano ndani ya CCM, ni climax tu ya matatizo yaliyomo ndani ya CCM kwa miaka mingi.
   
 12. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  KATIBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI, 2005


  Katibu Mkuu wa CCM, Sehemu ya 121 (1), (3)

  (1) Katibu Mkuu wa CCM atachaguliwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.

  (3)Na atafanya kazi chini ya uongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.


  Kazi za Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa, Sehemu ya 108 (22)

  Kazi za Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa zitakuwa: Kumwachisha au kumfukuza Uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.


  Makamba anaijua vizuri Katiba ya CCM - ndio wanaoiandika. Kusema anamwogopa Kikwete na Msekwa peke yake inakuonyesha Mzee has lost his marbles!
   
 13. M

  Mama JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Samahani naomba kuuliza, hiyo moja ya kazi au ndio kazi pekee ya halmashauri kuu ya sisiemu?
   
 14. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Makamba is so senile and needs to go so bad that I will devote only two lines or so at the very end to him.

  I am more concerned about the future of this contry than discussing some obsolete dinousars.


  When I summon my wits to rescue my bowels from the nausea of this ghastly and ghoulish level of unashamedly open scheudenfraude, with a possible similar past pronouncement, I shudder to think of a likely pattern yet am assured by - the so far - lack of an exacting precedent!

  To bestow recompense justice to this affair I will have to devote a keener piece on why such ill-reputed openness, in the guise of modernity, betray graver, latent, deeper and unhealthy regicidal tendencies.

  Despite the zeitgeist being for "shooting from the lip", Mr. Kabwe, the irresponsibility of your utterances may have largely been betrayed by your uncontrolled passion, a characteristic most uninspiring let alone statesman like.Diplomacy is a virtue and a vice depending on the occassion.In this case, the virtue is lacking, and the stately gravita is evaporating thinly into a blanketing dark cloud so ubiquitous it is transparent, that of losing focus of the issues and showing the people what you can do to help them and focusing on the downfall of your political enemies.

  This was one of the canonical flaws in the John McCain campaign, give the people a hope to continue to support you and your party.And if you don't like CCM that much, do something to expose their ills and let the people decide with a clear conscious.

  The passionate display of a gory appetite for destruction, far from a mere rhetorical nuance just to ascend the rungs of power, betrays a deep seated and even subconscious malady afflicting most of our politicians.

  To have the eyes set on the top job without a clue of what to do once that job is clinched.Kikwete took us down that route, we cannot bear irresponsible politicians anymore.

  This was most unstatesmanlike, most unstatesmanlike!

  On the other hand Makamba betrays the MO of CCM, leadership by "kuogopana"

  These clowns!
   
  Last edited: Nov 15, 2008
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Nov 14, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Makamba is a pugnacious purulent pugilist para-professional parlaying quasi-punditry perplexing politricks
   
 16. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2008
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 341
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Duuh! wana kiingilishi kigumu kweli.Wacha nende kwenye udaku!!!
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  wacha kutisha watu wewe....!
   
 18. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #18
  Nov 15, 2008
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Alah! mtu aliyetishika utamjua tu.....

  Weka basi na wewe vitu vyako tuvione....
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Anawajibika moja kwa moja kwa mwenyekiti ambaye ndiye alimteua, lakini hii sio tikiti ya kuwakejeli na kuwadharau wengine. Lakini akumbuke pia kuwa hata huyo mwenyekiti chama sio cha kwake. Anawajibika pia kwa wenye chama ambao nia wanachama anaotakiwa kuwaheshimu na kuwaogopa. sioni utumbo uko wapi hapa.
   
 20. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Pamoja na kuwa CCM inanekana iko kwenye crisis, ukitaka kujua kama watanzania wamelala zaidi kuliko chama, angalia chaguzi za kiteto na tarime. Sikutarajia hata kidogo idadi ya watu waliokipigia kura CCM iwe kubwa namna ile. Ingawa opposition walishinda tarime, kutoka na hali halisi ya chama nilitegemea margin ingekuwa kubwa kuliko ilivyokuwa, Kiteto same stroy sikutegemea kama wangeshinda, hapa unaona kuwa bado wengi tumelala. So kauli ya mh Zitto ina ukweli, lakini haibadilishi mambo. Mambo yatabadilika kama kweli opposition watatumia fursa hii.
   
Loading...