Makamba futa tarif 4 na tarrif 6, ambapo Bei ya unit moja ni sh 100 na sh 12 ilihali TANESCO wanaonunua zaidi ya 200

Basai wote tuuziwe sh 12 kwa unit
Mkuu Nishati ni gharama hata kama gharama hio sio pesa (ndio maana kuna vifaa energy efficient na matangazo ya don't waste energy) kwahio mkuu hizi tariff ndogo wameweka kwa watu wenye matumizi madogo sasa wakiweka pesa ndogo sana huenda watu wakaanza kufuja yaani wanaacha taa zinawaka au hata kutumia AC wakati milango ipo wazi....

Issue sio free bali ni affordable, na kwa watu ambao wamepewa limit ya unit 75 kwa mwezi matumizi yao sio ya kufuja ni kweli ni madogo..., kwahio hata Bwawa la Nyerere likianza kumwaga Megawatt Huenda tukafika huko ila hata huko itabidi kuwe na limit sio mtu mmoja unatumia umeme kama vijiji kumi sababu tu eti ni bei rahisi
 
Nachukua sana shirika la TANESCO ila sina la kufanya basi ipo siku tu maana hata TTCL waliwahi kuwa wanaringa sana....leo wanabembeleza sana wateja japo wateja hawana muda na TTCL....hata vizazi vijavyo ipo siku TANESCO itakuwa useless kwenye jamii ya watanzania
Hiyo ni point. Nakumbuka miaka ya 1980s na mwanzoni mwa 1990s tuliongea sana kuhusu mashirika ya nje kuwekeza katika umeme ili kuwe na ushindani lakini hatukufanikiwa, kwa kuwa hakuna ushindani TANESCO wanafanya wanavyotaka.
 
Unaye andika haya usha wahi kutafakari RISK walizo nazo fanyakazi wa Tanesco kwa
Aina ya kazi zao?

Acheni roho za kimasikini kila mfanyakazi ana bonus yake sehemu ya kazi. Sehemu nyingi za kazi wafanyakazi wana pewa BONUS ,TBL wana pewa bia kila mwisho wa Mwezi,Sigara wana pewa sigara kamo bonus,Kampuni za Simu wana pewa airtime,Saruji wana pewa Cement
Na polisi wanapewa nini ( risasi
 
Tanesco, wafanye mapatio ya Tariffs za matumizi ya umeme.Kwa maana tariffs hizi zinatumika ziliwekwa wakati ule Shirika linanunua umeme kwa bei kubwa kutoka dowan s,songas,IPTL ambako waliingia mikataba ya kifisadi,yenye kuwekwa minimum fixed rate ya kulipwa,kila mwezi, Shirika liwe limepokea umeme au halikupokea umeme kutoka kwa supplier.
Kwa kuwa,kuanzia June 2022 mradi mkubwa wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere -Rufiji utakaozalisha Megawatt zaidi ya 2,000 kwa gharama nafuu ya shs50 kwa unit utaanza,basi mchakato wa kufanya mapitio ya Tariffs uanze,ili kuwapunguzia makali ya maisha wananchi.

Faida
(1) Watu wengi wataweka na kutumia umeme kwa shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
(2) Utapunguza matumizi ya kuni na mkaa.(uhifadhi wa misitu).

Mapendekezo
(1). TANESCO iweke tariffs mbili tu, tariff namba moja umeme wa viwandani -Three Phase
(2). Tariffs two-Umeme wa majumbani single phase
(3) wafanyakazi wa TANESCO,waendelee kupewa bonus Kama ilivyo kwenye mkataba wa Hali Bora kati ya Mwajiri na wafanyakazi kupitia chama Chao cha wafanyakazi.
Kwa wafanyakazi ambao hawana nyumba,ninadhani Kuna utaratibu,unaotumika kuwapa motisha..
 
Sheria na kanuni za kijinga ndizo zinazosababisha wizi,rushwa na hujuma kila kona ya nchi.

Hivi kuna tatizo gani kwa bei ya umeme kuwa sawa kwa watumiaji wote.
Kama mtu ana matumizi makubwa atatumia zaidi na atanunua zaidi.
Mwenye matumizi madogo atatumia kidogo sio kupunguziwa bei tena kwa kufanya dili.

Yaani kwa bei hizo zinawafanya watu ndani ya Tanesco kupiga rushwa toka kwa wenye pesa ili wawekewe tarifu za chini kabisa wanunue umeme kwa bei ndogo.
Lakini Pia wafanyakazi wa Tanesco wanawaibia watanzania umeme.
Wafanyakazi wa Tanesco wengi hawanunui umeme wanapewa umeme mwingi sana kama bonas.
Sasa kwa wingi wao nadhani shirika ni lazima lipate hasara.


Hiyo ipo pia kwenye Mafuta ya Petroli ,diseli na mafuta ya taa.
Serikali inapata hadara kubwa sana kwa ujinga tu wa watu wabinafsi wasiojali maslahi ya taifa zaidi ya maslahi binafsi na siasa za kijinga.

Mafuta ya taa yanachanganywa sana na mafuta mengine kwa kuchakachua kwa sababu yana ushuru mdogo ukilinganisha na petrol. Sasa unajiuliza kwa nini kodi ya Mafuta ya taa isiwe juu ili kuondoa suala zima la kuchakachua na kuingiza taifa kwenye hasara ya kuwalipa wapiga dili ndani ya Ewura?

Simple ilikua umeme bei moja na Petrol ,diseli na mafuta ya taa yote bei moja 2300/- kwa mfano.

Mbona bando kwenye simu kila mmoja anapiga kwa gaharama inayotokana na matumizi ya na sio uwezo wa mtu eti ,kundi la kipato Fulani wakipiga simu au wakiweka bando bei iwe chini na wengine bei iwe juu.


Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
Nilidhan ungependekeza wananchi wote wapatiwe umeme kwa 100/unit ndo ingekua bizuri zaidi
 
Wabongo bwana!! Badala ya kulia umeme wa majumbani ushushwe bei nyie mna taka bei zirnde juu ati Tanesco wana pata hadara. Jema kwenu nyie ni lipi??
Hawa wapiga debe wa hivi karibuni Ni kundi limeanzishwa lituchanganye Kisha tukubafi Tanesco ibinafsishwe,hapo tayari bwawa la mwalimu nyerere litakuwa limekamilika ili tuupate umeme wa gharama ndogo,miundombinu ya umeme Hadi vijijini tayari kwa Kodi zetu halafu wanakuja na hadithi za kuua Tanesco ili watubamize!
 
Mkuu Nishati ni gharama hata kama gharama hio sio pesa (ndio maana kuna vifaa energy efficient na matangazo ya don't waste energy) kwahio mkuu hizi tariff ndogo wameweka kwa watu wenye matumizi madogo sasa wakiweka pesa ndogo sana huenda watu wakaanza kufuja yaani wanaacha taa zinawaka au hata kutumia AC wakati milango ipo wazi....

Issue sio free bali ni affordable, na kwa watu ambao wamepewa limit ya unit 75 kwa mwezi matumizi yao sio ya kufuja ni kweli ni madogo..., kwahio hata Bwawa la Nyerere likianza kumwaga Megawatt Huenda tukafika huko ila hata huko itabidi kuwe na limit sio mtu mmoja unatumia umeme kama vijiji kumi sababu tu eti ni bei rahisi
Mmmh! Sasa kama watafuja si matumizi yao ndo watalipa, umeme uwe bei chini kwa dunia ya Leo teknolojia inatumia umeme kwa Kila kitu Sasa ukiwa bei chini hata hili swala la ajira litapunguza ukosefu wa ajira kwa wingi maana kwenye kutumia umeme Kuna kazi nyingi sana na pia vitu vingi vya kuokoa muda vinatumia umeme.
 
Back
Top Bottom