Makamba azungumza kwa mara ya Kwanza Bungeni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba azungumza kwa mara ya Kwanza Bungeni.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Jul 22, 2008.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa Tangazo la Spika mchana wa leo ni kuwa jioni hii mbunge wa Viti maalum MH.Yusuph Rajabu Makamba ,na kwa mujibu wa tangazo hilo spika alisema kuwa kuna wabunge watatakiwa kusafisha njia na Makamba atakuwa mtu wa tano kuchangia.


  Sasa kuna haja ya kujua mbunge huyu wa viti maalum atachangia nini kwa mara ya kwanza tangu aingie kwenye Bunge .

  Leo ni siku ya hotuba ya kilimo hivyo huenda anakuja kutueleza kuwa ILANI iliposema kuwa kilimo kitakuwa kwa asilimia 20 ifikapo 2010 ilikuwa na maana gani.

  Nawatakia kulifuatilia bunge kwa umakini ili kujua huyu atachangia kitu gani.

  Atasema kuwa Zanzibar ni nchi?
  Atasema kuwa Nnape alichemka?
   
  Last edited by a moderator: Jul 23, 2008
 2. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hana lolote huyu
  atakaa kunukuu vifungu vya biblia na msaafu mahali ambapo apatakiwi references tena kwa makosa

  Huyu ndio anaprove failure ya Kikwete, Mimi sijui Kikwete alikuwa akifikilia nini eti kumpa mpaka ubunge mtu kama huyu.

  Nadhani Kikwete haelewi maana na umuhimu wa nafasi za ubunge wa kuteuliwa na ndio maana anatoa tu kwa watu ambao hawafanyi mambo yanayotakiwa kutokana na kuteuliwa kwao
   
  Last edited by a moderator: Jul 23, 2008
 3. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jamani jueni kuwa huyu ni mteuliwa wa Rais sasa kama mnaona hana lolote je?kumpa mpaka ukatibu mkuu ina maana kuwa alikosea ama ndio alimuona anafaa?


  Ila pia ni aibu kwa huyu katibu mkuu wa chama kinachotawala kukaa ndani ya bunge kwa zaidi ya miaka miwili kukaa bila hata kuchangia huku akiwa ndio mwenye jukumu la kuhakikisha kuwa ilani ya chama chake inafuatwa na serikali iliyopo madarakani.

  Tunasubiri kuona kama atailinda ilani juu ya kilimo ama atasema ya kwake.

  Nawawekea ilani ilisema nini kuhusu kilimo punde.
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Makamba is simply senile, ataishia kuimba pambio tu humo, figuratively or even literally.
   
 5. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,918
  Trophy Points: 280
  Kieleweke Mbowe aliwahi jusema hayo hapo chini....

  Je mawazo yamebadilika?

  Kweli Makamba ategemewe kusema nini?

  Nini ambacho hakijulikani hadi sasa hapa tulipo kuhusu ufisadi wa ccm?

  Nilipoona heading ya Thread nikadhani anakuja kuchangia hapa jf...Kumbe ni bungeni?

  Sasa kama ni bungeni unapingana na mawazo ya awali kuwa bunge ni mchezo wa kuigiza.
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Sura ya tatu.
  Sekta ya uzalishaji.

  31.Ili uchumi wa nchi yetu ukue kwa kiwango cha asilimia 10 ifikapo mwaka 2010 lazima angalau kilimo kifikie ukuaji wa angalau asilimia 20 ifikapo mwaka huo.Kwa lengo la kufikia kiwango hicho cha ukuaji wa kilimo ifikapo mwaka 2010 CCM itachukua hatua zifuatazo;

  c)kwa utengenezaji na upatikanaji wa mikokoteni ya kuvutwa na wanyama na vinu vya kisasa vya kukobolea na kusagia nafaka.

  Ntaendelea kuweka ilani juu ya kilimo.
   
 7. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jmushi sijaelewa maswali yako hata kidogo, umeweka hiyo makala ya Mbowe na kunuliza maswali kana kwamba unawasiliana na aliyeandika makala husika.

  Kwa taarifa zaidi ni kuwa sasa anachangia Nsanzuguanko na atafuatiwa na Mama Malecela then Makamba atafuata kuchangia kwa kina.
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,918
  Trophy Points: 280
  Jamani kama ni kweli ccm inapata bilioni tisa kwa mwaka(tena kwasasa inaweza kuwa zaidi)
  Naomba yule mwenye data aweke hapa ili tujuwe ccm ina wanachama wangapi na tulinganishe na pesa hizo!
  Hizo ni pesa nyingi sana...Halfu na maendeleo hakuna na huku serikali yenyewe ikiwa haifanyi kitu zaidi ya ufisadi.
  Tunaomba namba ya wanachama wa ccm halafu tuangalie ni wananchama wangapi wamenufaika na ruzuku hiyo na pia tujuwe wananchi wasiokuwa na vyama walinufaika vipi na pesa zao hizo walizopewa ccm.
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,918
  Trophy Points: 280
  Hapana..Ni makosa ya kiusomaji ama ya kimaandishi.
  Nita verify...Nilikuwa namaanisha kusema hivi...Kieleweke eeh! Mbowe alishawahi kusema Bunge ni kama mchezo wa kuigiza na hivyo wewe kama kieleweke unapingana na kauli ya Mwenyekiti wako kuwa bunge halina mpango na hivyo haina maana sana kuwa Makamba atasema nini kwani yeye kama kada wa ccm ataifagilia tu!

  Umesahahu hata bajeti ya kifisadi ilipitishwa na watu kama kina Killango na Chenge?

  Sasa kama kimaamuzi ni kitu kimoja huko bungeni na kikauli kwenye press ni tofauti na za kiukali tutafika kweli?

  Inawezekana kabisa wabunge wa ccm wameamuwa kutumia tactics nyingine kwa kujidai wako tofauti kwa kauli zao tata!

  Lakini at the end of the day bajeti husika inapitishwa!

  Hivyo kama tunajuwa uamuzi upi ni right..Then watakochesema hakitajalisha bali watakachoamuwa kwa kupiga kura zao huko bungeni.

  Ni mawazo yangu tu..Ila pia tutaendelea kumsubiri kwani hapa ni jf na awe makini na kauli zake kwani tushamjuwa.

  Cha muhimu ni..Je at the end of the day ni mwananchi MNUFAIKA?
   
 10. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jmushi mbona hapa tunazungumzia tendo la kihistoria la mbunge wa viti maalum kuzungumza kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa wewe unahamisha mjadala?

  Umewahi kusoma espionage of writting?
  Umewahi kupata elimu ya Mosad?

  Mama Kilango anachangia na kutaka kujua ni kwanini kilimo chetu kipo butu ,anasema kuwa ni kukosekana kwa mbegu,mbolea,teknolojia. ila yeye atajikita zaidi kwenye kuunganisha kilimo na viwanda vya usindikaji na hilo ndio linatufanya tunakuwa nyuma kiasi hicho.

  Kuna haja ya kujua huyu atasema nini kwani ilani yao imejipanga kukuza kilimo kwa asilimia 20 ifikapo 2010 sasa hiki ni kilimo kitakachokuwa kimekuwa kuliko popote pale duniani , kweli CCM kwa ilani hii wataweza kutufikisha nchi ya neema.
   
 11. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jmushi mbona hapa tunazungumzia tendo la kihistoria la mbunge wa viti maalum kuzungumza kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa wewe unahamisha mjadala?

  Umewahi kusoma espionage of writting?
  Umewahi kupata elimu ya Mosad?

  Mama Kilango anachangia na kutaka kujua ni kwanini kilimo chetu kipo butu ,anasema kuwa ni kukosekana kwa mbegu,mbolea,teknolojia. ila yeye atajikita zaidi kwenye kuunganisha kilimo na viwanda vya usindikaji na hilo ndio linatufanya tunakuwa nyuma kiasi hicho.

  Kuna haja ya kujua huyu atasema nini kwani ilani yao imejipanga kukuza kilimo kwa asilimia 20 ifikapo 2010 sasa hiki ni kilimo kitakachokuwa kimekuwa kuliko popote pale duniani , kweli CCM kwa ilani hii wataweza kutufikisha nchi ya neema.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,534
  Likes Received: 81,955
  Trophy Points: 280
  Babah, hata hivyo vifungu vya Biblia na Kuran havijui ni mbabaishaji tu. Yeye na JK aliyekuwa mbele hajulikani.
   
 13. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2008
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Unashangaa, Rais mwenyewe ni bomu sasa unategemea nini. Enzi za Mkapa watu hatukuwa tunajadili jinsi gani kazi inamshinda bali ni jinsi gani mikataba anyoingia na the so called wawekezaji itatuaffact vipi. Lakini sasa kwa JK swala hilo sio periority tena kwa vile hata mwelekeo wa nchi hatuujui. Imagine Katibu wa CCM kuwa Makamba, kuna jipya hapo au ni kutafutiana mlo tu??????
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,918
  Trophy Points: 280
  Haya tuone kama hilo tendo la kihistoria litaweza kubadili maigizo hayo ya bunge la ccm.

  Tena makamba!

  Tunasubiri kwa hamu kwasababu ni kweli issue ya kilimo na viwanda ni muhimu kupita kiasi...Just kama madini na utalii.

  Sisi Watanzania ni matajiri na hivyo hapo ndipo kwenye pointi na kufikiri kuwa Makamba atatuletea neema ni ndoto!

  Huyu mtu alimbusu Manji mnasema ana akili nzuri huyu?

  Huyu ndiye Yusufu yule yule aliyejipatia umaarufu kwa kupenda kutowa mifano ya Biblia!

  Ama kweli wajinga ndio waliwao.
   
 15. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Makamba ameanza kwa kusema kuwa amekaa kwa muda mrefu sana bila kusema kwani alikuwa shuleni, na kwa kuwa yeye amezoea kukaa kwenye mikutano ya pasua baba akifanya hivyo huko ataaibika.

  Leo ndio anamshukuru rais kwa kumteua na anasema kuwa deni la fadhila ni kulipa fadhila, uteuzi wake ulikuwa ni fadhila za rais.

  Anasema kuwa amesoma maandiko matakatifu kutoka kwenye biblia kuwa anayetamani uasikofu anatamani kazi njema ,na anayetamani usipika anatamani kazi njjema.

  Anampongeza waziri mkuu ,anasema kuwa siku njema huanza mapema ,ameanza vizuri.ila anasema kuwa pengo la jino la dhahabu limezibwa kwa dhahabu.

  Nabii Yeremia aliogopa sana ila akaambiwa kuwa atapewa maneno ya kusema na hivyo pinda hana sababu za kuogopa .

  Anawapongeza wabunge kwa kuwa wanatekeleza ilani ya chama na anataka kuwatoa hofu kuwa wakiendelea namna wanavyoendelea sasa kazi yao 2010 ni rahisi sana.

  Anasema kuwa atasema machache na sio makubwa sana, anaomba radhi kuwa mzee Ngombale alipokuwa anachangia alisema kuwa anampongeza rais kwa kuwa anasimamia ilani ya ccm.

  Siku mbili baadae alisimama mbunge mwingine kwa staili ya waandishi na kusema kuwa haya tunayosema tunayaona,tuanayasikia, na tunayafanyia kazi ila kesho yake magazeti yaakaandika mzee Ngombale kitanzini.
  unaweza ukawa na masikio lakini ukayaziba ukayatia hata na pamba ili usiyasikie mambo mazuri ambayo yanafanywa na ccm ,hata ukaambiwa kuwa pale dodoma panajengwa chuo kikuuu ukaweka kisogo wala usitake kuona, unaweza kukiona kitabu kizuri cha ilani ila usisikie, anachotaka kusema ni kuwa ukijua kulaumu sharti ujue kusifu ili wenzako wasikuone kuwa ni kilema kwani hata kwenye jimbo lako yapo ambayo yanafanyika .

  baada ya kusema haya naona nimpongeze rafiki yangu wassira na naunga mkono hoja.

  Humu ndani tuna mzee Ngombale aliandika maandiko mwaka 1972 kuwa siasa ni kilimo, kuna sera mbalimbali na azimio la iringa, atalitazama zaidi azimio la iringa la mwaka 1972, linasema kuwa watumishi wa kilimo hawawezi kuwepo kila kijiji wakati ulele wanapokuwa wanahitajika ila wanapaswa kuelekeza teknolojia ya kilimo.

  Anasema kuwa kazi ya kwanza ya kiongozi ni kujifunza kanuni za kilimo hana uhakika wassira anajua vipi kilimo, ni rafiki yangu hatanipeleka popote.

  Ukisoma hotuba ukurasa wa 20 anatuambia kuwa mwaka 2007 wataalamu wa kilimo waliajiriwa 337 ila lengo lilikuwa ni kuajiri 2500, ila anasema kuwa namna nziuri ya kufanya ni kuwa nchi hii ina viongozi wengi sana kuanzia shina,n.k, hivi ukilitazama shamaba la Lowassa linakuwa mfano?shamba la kapuya ni mfano? wabunge wenzangu tunaandika sana tunasema sana ila tatizo ni kuwa ugumu upo kwenye kutekeleza , tunakuwa kama mafarisayo ananukuu biblia na kuraan, enyi mlioamini mbona mnasema maneno ambayo hamtendi?wananchi wanatusikiliza hapa .

  Sera za CCM zinasema kuwa serikali inapaswa kuwatambua wakulima kwa kuanzisha mashindano ya kilimo hivi yapo? tunawaenzi wakulima wetu?kila mtu akiandika anayasema ila wa kuyatekeleza hakuna?

  Ilani ya uchaguzi 2005 inazungumzia tuzo ,zawadi kimikoa ...ananukuu ilani 31(b) .......
  sura ya 9 ibara ya 132, anasema ipo mikoa ambayo imeonyesha mifano ila hawajapewa tija na zawadi.

  amemaliza muda wake.
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kweli aslihajisahau akadhani anahutubia mkutano wa ccm
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Anamhoji Waziri wa Kilimo mikoa iliyoongoza kwa uzalishaji wa mahindi imeopata tuzo gani wakati chama chake ndicho kinachounda serikali iliyopaswa kuyafikiria hayo. anataka nani amjibu? Kama anaona serikali iliyoundwa na chama chake haifanyi kazi inavyostahili si ivunjiliwe mbali?!
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jul 22, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kweli supika hakumchomekea vijineno maana Sitta naye kwa kuchomekea tu.. hajambo..
   
 19. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2008
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  hapa alikuwa na maana tayari watanzania wameisha pata neema iliyohaidiwa na mwenyekiti wao?.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,918
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo hiyo alert yako ya Makamba ndiyo hiyo hapo juu?

  Na maneno niliyoyasema dakika chache zilizopita si ndiyo hayo hapo juu!

  Tena kwa ku NAKSHI kabisa....YUSUFU KWA MARA NYINGINE AMETOWA MFANO WA YEREMIA!

  Hivi huyu jamaa ni mkristo ama msilam?

  Maana matendo yake na maneno yake vinatofautiana!

  Nadhani huyu ndiye aliyewajaza viongozi wa dini ujinga kuwa JK ni mpango wa Mungu.

  Huu ni utapeli mtupu kwani makanisa hayo hayo yashamwalika RA na wachungaji pia kupokea RUSHWA!

  Jamii imegeuza mwelekeo...Sasa ni Utanzania kwanza kabla ya dini wala kabila.

  Na ujumbe wangu ni huu kwa viongozi wadini..Kama haki isipopatikana na JK akarudi madarakani..Basi nyie ni wasaliti MANABII WA UWONGO NA TUTAWACHOMA MOTO KABLA YA SHETANI MWENYEWE KUFANYA HIVYO HUKO JEHANAM!

  Mlikuwa na ushawishi mkubwa sana na ndio maana ushindi ukawa wa Tsunami kwa sababu ya RUSHWA na unajuwa WACHUNGAJI NA MAASKOFU WENGI WENU NI MATUMBO TU NA THIS TIME YATAPASUKA KAMA JK AKIRUDI MADARAKANI NA UFISADI USIPOPATIWA UFUMBUZI NA HAKI KUTENDEKA!

  Sasa hivi naandaa tu namna ya kuwamalizia mbali manabii wa Uwongo waliolifikisha Taifa letu hapa kwa unafiki na TAMAA!

  VIONGOZI WA DINI WAMETUMIKA SANA KUIANGAMIZA TANZANIA HILO WAJUWE NA MAPINDUZI HAYATAWAACHA KAMA WASIPOFANYA KAZI INAVYOTAKIWA!

  Kabla ya kujidai kwenda kuyaombea mapepo huko bungeni wengi wenu ni wa kuombewa hayo mapepo ya unabii wenu wa uongo yatolewe!

  Taifa litafikiaje mahali kama hapa na sisi tuseme ETI TUNA VIONGOZI WA DINI?

  Kungekuwa na viongozi hao wa dini wa kweli wenye kuijali jamii na wala si manyapara wa wakoloni wa kila aina...Basi Taifa lisingekuwa hapa lilipo!

  NA PIA HILO BUNGE NALO KAMA LINGEKUWA LA MAANA LISINGEPITISHA HAYA MAAMUZI YOTE YA KIFISADI na sheria za kifisadi zilizovunja KATIBA YETU!

  sHERIA ZILIZOAMULIWA NA bunge hilo mnalotaka tulisikilize!
   
Loading...