Makamba awatibua makatibu wa CCM mkoani Kilimanjaro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba awatibua makatibu wa CCM mkoani Kilimanjaro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, amewatibua makatibu wa wilaya wa chama hicho waliogeuka `wabeba mikoba' ya wanasiasa wanaotangaza nia ya kugombea ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

  Akizungumza na viongozi wa CCM wa wilaya na mkoa katika ziara yake mkoani Kilimanjaro, Makamba alisema baadhi ya makatibu wa chama hicho, wanakiuka kanuni na taratibu kwa kuwa sehemu ya wenye nia za kugombea ubunge.

  Makamba alisema tatizo la kuvunjika kwa maadili linakuwa kubwa ndani ya CCM, akitoa mfano wa ushiriki wa makatibu hao kushirikiana na wenye nia za kugombea ubunge kabla ya muda.

  Aliwataja baadhi ya makatibu hao kuwa ni Alan Kingazi wa Moshi Vijijini yenye majimbo ya Vunjo na Moshi vijijini.

  Mwingine ni Steven Kamote wa Moshi Mjini, kwamba wanashiriki vitendo hivyo na kuivuruga CCM.

  "Katibu anabeba mikoba ya wagombea, unatarajia nini, wewe ni Katibu wa wilaya na wagombea wote wanakuja kwako…umesahau kuwa wewe ni mteule wa Kamati Kuu ya CCM, unambebea hadi mikoba yake," alihoji.

  Alisema tatizo la ukiukwaji wa maadili na watu kufanya kampeni kabla ya wakati, linazidi kushamiri katika CCM.

  Hata hivyo alitoa muda wa siku kumi kwa makatibu hao na wengine kuacha mara moja tabia hiyo. "Kingazi (Katibu wa CCM Moshi vijijini), shame, shame on you," alisema akimaanisha ni aibu kubwa kwa Katibu huyo.

  Aidha, alisema CCM haitakubali viongozi wake kujidhalilisha na kukidhalilisha chama hicho kwa matendo yao.

  "Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete ameelekeza kuwa kiongozi yoyote atakayevunja maadili na kanuni za chama nimfukuze, halafu nitoe taarifa kwenye Mkutano Mkuu," alisema.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Braza angekuwa anafuatilia anachosema angejifukuza kwanza yeye mwenyewe kabla hajageukia wengine kwa kubeba mikoba ya mafisadi...
   
 3. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hivi sio yeye huyu Makamba ambaye alianza kubeba mikoba ya Rostam kule Igunga kwa kumtangaza kuwa ni mgombea wa ccm kwenye nafasi ya ubunge kabla hata ya kikao cha kura za maoni?
   
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwani si naye alishatuhumiwa kuwa mmoja wa mafisadi? Akapiga kelele wakamwambia ushahidi upo kedekede akibisha na aende mahakamani akaanikwe, akanywea nywiiiiiiiii!
   
 5. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huyu mzee ni MNAFIKI SANA, ukiona hvyo basi huyo jamaa anayepigiwa kampeni hamtaki yeye binafsi....kule bumbuli amewaita makatibu kata wote na akawapa kazi ya kumpigia kampeni mwanae January.

  ...alikuwa hajui kama anavunja sheria na kanuni za chama, na amewafukuza na kuwapa onyo wale makatibu wote waliokaidi agizo lake la kumtangaza mwanae....na yeye mwenyewe binafsi amekuwa akiwapigia simu badhi ya viongozi na wazee jimboni akiwataka wamsaide kijana wake....shame shame on yu Mzee Makamba...
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Hivi si Makamba huyu huyu aliyempigia debe Yusuf Manji kule kigamboni kabla ya muda muafaka mwaka 2005?

  Huyu mzee anazeeka vibaya hivi sasa anamtumia katibu wa CCM Lushoto kumbeba Januari Makamba katika kampeni zake chafu za kutangaza nia nia ya kugombea jimbo la Bumbuli.

  Nashukuru kuwa watu wa Bumbuli wamemshitukia huyu dogo Januari kwani wala yeye si wa jamii ya watu jimbo hili kwani ni huyu ni mtoto wa kufikia wa makamba na mama yake siyo mzawa wa jimbo hili. Mzee wacha unafiki.
   
 7. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #7
  Jun 8, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,454
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Pia kwa kumpigia kampeni JK
   
Loading...