Makamba awaponda wanaoandamana

Ortega

JF-Expert Member
Jan 4, 2011
844
209
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amesema maandamano si suluhisho la matatizo yanayotokea nchini na kwamba Rais anapaswa kupewa muda ili ayatatue.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana kabla ya kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa CCM, Aman Abeid Karume, ili azindue sherehe za maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa chama hicho, Makamba alisema maandamano ni ishara ya uvivu.

Alifafanua katika viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam kuwa maandamano ni uvivu kwa kuwa yanagharimu muda mwingi wa watu kufanya kazi za maendeleo.

Kwa mujibu wa Makamba, matatizo kama ya umeme na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali yanayoikabili nchi kwa sasa ni ya kawaida na yenye kutatulika, hivyo wananchi hawana budi kuvumilia ili watendaji husika wayatatue.

"Nchi yoyote haiwezi kutulia bila misukosuko ya matatizo kama haya ya umeme na mfumuko wa bei za bidhaa, ni ya kawaida na Watanzania mnapaswa kuwa wavumilivu na mumpe Rais muda ili pamoja na watendaji wake wayamalize…maandamano sio suluhisho," Makamba alisisitiza.

Katika hatua nyingine, CCM imekiri kupoteza majimbo yake ya Kawe na Ubungo katika uchaguzi wa mwaka jana kutokana na dharau iliyokuwa nayo kuhusu uwezo wa kisiasa wa wagombea wa vyama vya upinzani pamoja na kutojitokeza kwa wengi kupiga kura.

Hata hivyo, kimewasisitizia wanachama wake kuwa kitayarejesha majimbo hayo pamoja na kata 16 zilizochukuliwa na upinzani katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda alisema tathmini waliyoifanya kuhusu matokeo ya uchaguzi huo ndiyo iliyobainisha kuwa dharau iliwasababishia kunyang'anywa majimbo hayo na kosa hilo halitajirudia kamwe.

Naye Karume aliyezindua sherehe hizo na kutoa vyeti kwa watu waliokiwezesha chama hicho kushinda kwa hali na mali katika uchaguzi huo, alisema anaamini wapinzani watarejesha majimbo na kata walizozikopa kutoka kwa CCM kwa kuwa anayekopa hupaswa kurejesha.

Karume alisema, endapo hawatayarejesha kwa hiyari na kiuungwana, CCM haitasita kuwagongea hodi na kuwakumbusha kuyarejesha.

"Upinzani uliikamia sana Dar es Salaam na kutukopa majimbo yetu mawili na kata 16, tutayarejesha kwa kuwa uwezo wa kufanya hivyo tunao na nia tunayo, wapinzani ni wanafunzi wetu wa siasa hivyo lazima tuwe nao ili tuwafundishe, huku tukiwasoma, tusiwafukuze kwa kuwa tuliwakaribisha wenyewe mwaka 1992, tusiwachoke ili waturudishie kilicho chetu."

SOURCE: HABARILEO
 
...kuna mijitu iko nje ya wakati kabisa!!! kuandamana ni ishara ya uvivu?? basi wazungu ni wavivu zaidi yetu maana wao wanaandamana kuliko sisi waafrika na 'uvivu' huo umewaletea maendeleo na nafikiri si vibaya kugeza jambo hata kama baya ili mradi linaleta maendeleo. Nafikiri CCM wakiandaa mkutano au kongamano na Makamba akawa mmoja wa wahutubiaji, lazima wenye hypertension wanywe vidonge vya kushusha BP kabla Makamba hajaongea maana huyu jamaa ni ugonjwa wa moyo daima kwa kauli zake!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom