Zee la shamba
Member
- Oct 17, 2007
- 55
- 3
Waliovunjiwa Tabata wapelekewa mchele mbovu
*Makamba akiri kuupeleka, asema ni bahati mbaya
*Aahidi kuubadilisha, aonya isichukuliwe kisiasa
Eben-Ezery Mende na Zamzam Abdul
WAATHIRIKA waliobomolea nyumba Tabata Dampo, Dar es Salaam, wamepelekewa msaada wa mchele mbovu na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Yusuph Makamba na kushindwa kuutumia.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa waathirika hao, Bw. Said Masoud (54), alisema wiki mbili zilizopita, Katibu Mkuu wa CCM aliwatembelea na kuwapa msaada wa mifuko 20 ya mchele na walipoutumia waligundua kuwa ulikuwa tayari umeharibika na haufai kwa matumizi ya binadamu.
Alisema baada ya kuutumia, walidhani mfuko wa kwanza ndio uliokuwa na matatizo, lakini walipofungua mfuko wa pili nao ulikuwa na tatizo hilo hilo na hivyo waliifungua mifuko yote na kubaini kuwa yote ilikuwa katika hali hiyo hiyo.
"Tunashukuru sana kwa misaada inayoletwa na watu kutoka kila kona ya Tanzania na pengine nje ya nchi, lakini kwa mchele ulioletwa na kiongozi wa CCM, tumeshindwa kuutambua. Mifuko yote 20 aliyotuletea tumeshindwa kutumia hata mmoja, yote ilikuwa imeharibika," alisema.
Aliwaomba wasamaria wema waendelee kuwafadhili kwa misaada mbalimbali hasa chakula, kwani wamekuwa wakila cha aina moja tu; ugali na maharage lakini kwa msisitizo kuwa pamoja na kwamba wako katika matatizo, watu wanaowapelekea msaada wa chakula wapeleke chakula ambacho kinafaa kwa matumizi ya binadamu.
"Kweli tumeathirika katika hili la nyumba, lakini akili zetu bado zina uwezo wa kufikiria na kutathmini hivyo tunaomba tusichukuliwe kuwa tumeathirika hata akili.
"Nasema hivyo, kwani wapo watu wenye mapenzi mema na wanaotuletea vilivyo sahihi, lakini wapo ambao siwezi kuwaita waasi, lakini wenye kufanya kejeli kutokana na tatizo lililotufika," alisema.
Akizungumza kwa njia ya simu kujibu malalamiko hayo, Bw. Makamba alisema CCM haina ghala, hivyo inanunua chakula kama watu wengine wanavyofanya na chakula kilichonunuliwa na CCM kilikuwa ni kwa ajili ya msaada wa wananchi hao na si vinginevyo.
Alisema kama chakula hicho kimeonekana kuwa na kasoro ni jukumu la kiongozi wa waathirika hao kutoa taarifa kwake, ili akirudishe kwa aliyemuuzia ili ampe chakula kinachostahili.
"Mimi na CCM hatumiliki ghala la chakula. Tunanunua chakula kama wanavyofanya watu wengine hivyo kama chakula ni kibovu wanatakiwa waniletee taarifa mimi, ili nikirudishe nilikokinunua na niwapelekee chakula kingine. Mpaka sasa sijapewa taarifa zozote kutoka kwa waathirika hao," alisema Bw. Makamba.
Akifafanua, alisema yeye akiwa kiongozi, hawezi kupeleka chakula kibaya kwa wananchi na kama hilo lilitokea ni la bahati mbaya tu.
"Nilinunua chakula kwa Zakaria nikawapelekea baada ya kuniambia wana matatizo yakiwamo ya masufuria na pamoja na mchele huo niliwapa pia magunia 10 ya maharage...inaonekana sasa suala hili linataka kugeuzwa la kisiasa," alisema Bw. Makamba.
Hata hivyo alisema walichopaswa kukifanya wananchi hao, kwanza ni kumshukuru kwa msaada huo na kisha wamwambie tatizo ambalo alikiri kutokuwa na habari nalo wakati msaada huo unatolewa.
Ila alisema alishawasiliana na waliomuuzia na wakaomba mchele huo urudishwe ili wapewe mwingine, baada ya muuzaji pia kubaini kuwa ni kweli mchele huo ulikaa ghalani kwa muda mrefu hivyo kuharibika.
Naye Grace Michael anaripoti kuwa hata hivyo jana, wakazi hao wa Tabata walisema hawamlaumu Bw. Makamba kwa msaada wa vyakula ukiwamo mchele ambao ulidaiwa kuwa ni mbovu.
Mwenyekiti wa Wahanga hao, Bw. Masoud alisema: "Sisi kwa kweli kwanza tunaishukuru CCM kwa msaada mkubwa ambao iliuleta hapa ambao hata Manispaa ya Ilala ambayo imehusika kwa kiasi kikubwa kutufikisha hapa tulipo, haijaufikia msaada huo ingawa lilijitokeza suala la mchele mbovu.
"Sisi tunaamini kuwa Bw. Makamba hakuwapo wakati unapakiwa bali wapo waliofanya kitendo hicho cha kupakia mchele mbovu, hivyo ni tatizo dogo tu la kibinadamu na wala hatuwezi kumlaumu bali tunamshukuru kupitia chama chake."
Bw. Masoud kwa niaba ya waathirika wa bomoabomoa hiyo aliomba vyama vingine navyo vijitokeze kupeleka msaada katika kipindi hiki kigumu kwani wao hawabagui msaada wa mtu yeyote.
Mbali na vyama pia aliomba wasamaria wema nao wajitokeze katika kutoa misaada yao mbalimbali ili kuwaepusha na kula vyakula vya aina
SOURCE: GAZETI MAJIRA