Makamba Atoa Msaada Wa Mchele Mbovu Kwa Waliobomolewa Nyumba Tabata

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
Waliovunjiwa Tabata wapelekewa mchele mbovu

*Makamba akiri kuupeleka, asema ni bahati mbaya
*Aahidi kuubadilisha, aonya isichukuliwe kisiasa

Eben-Ezery Mende na Zamzam Abdul

WAATHIRIKA waliobomolea nyumba Tabata Dampo, Dar es Salaam, wamepelekewa msaada wa mchele mbovu na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Yusuph Makamba na kushindwa kuutumia.

Akizungumza na Majira Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa waathirika hao, Bw. Said Masoud (54), alisema wiki mbili zilizopita, Katibu Mkuu wa CCM aliwatembelea na kuwapa msaada wa mifuko 20 ya mchele na walipoutumia waligundua kuwa ulikuwa tayari umeharibika na haufai kwa matumizi ya binadamu.

Alisema baada ya kuutumia, walidhani mfuko wa kwanza ndio uliokuwa na matatizo, lakini walipofungua mfuko wa pili nao ulikuwa na tatizo hilo hilo na hivyo waliifungua mifuko yote na kubaini kuwa yote ilikuwa katika hali hiyo hiyo.

"Tunashukuru sana kwa misaada inayoletwa na watu kutoka kila kona ya Tanzania na pengine nje ya nchi, lakini kwa mchele ulioletwa na kiongozi wa CCM, tumeshindwa kuutambua. Mifuko yote 20 aliyotuletea tumeshindwa kutumia hata mmoja, yote ilikuwa imeharibika," alisema.

Aliwaomba wasamaria wema waendelee kuwafadhili kwa misaada mbalimbali hasa chakula, kwani wamekuwa wakila cha aina moja tu; ugali na maharage lakini kwa msisitizo kuwa pamoja na kwamba wako katika matatizo, watu wanaowapelekea msaada wa chakula wapeleke chakula ambacho kinafaa kwa matumizi ya binadamu.

"Kweli tumeathirika katika hili la nyumba, lakini akili zetu bado zina uwezo wa kufikiria na kutathmini hivyo tunaomba tusichukuliwe kuwa tumeathirika hata akili.

"Nasema hivyo, kwani wapo watu wenye mapenzi mema na wanaotuletea vilivyo sahihi, lakini wapo ambao siwezi kuwaita waasi, lakini wenye kufanya kejeli kutokana na tatizo lililotufika," alisema.

Akizungumza kwa njia ya simu kujibu malalamiko hayo, Bw. Makamba alisema CCM haina ghala, hivyo inanunua chakula kama watu wengine wanavyofanya na chakula kilichonunuliwa na CCM kilikuwa ni kwa ajili ya msaada wa wananchi hao na si vinginevyo.

Alisema kama chakula hicho kimeonekana kuwa na kasoro ni jukumu la kiongozi wa waathirika hao kutoa taarifa kwake, ili akirudishe kwa aliyemuuzia ili ampe chakula kinachostahili.

"Mimi na CCM hatumiliki ghala la chakula. Tunanunua chakula kama wanavyofanya watu wengine hivyo kama chakula ni kibovu wanatakiwa waniletee taarifa mimi, ili nikirudishe nilikokinunua na niwapelekee chakula kingine. Mpaka sasa sijapewa taarifa zozote kutoka kwa waathirika hao," alisema Bw. Makamba.

Akifafanua, alisema yeye akiwa kiongozi, hawezi kupeleka chakula kibaya kwa wananchi na kama hilo lilitokea ni la bahati mbaya tu.

"Nilinunua chakula kwa Zakaria nikawapelekea baada ya kuniambia wana matatizo yakiwamo ya masufuria na pamoja na mchele huo niliwapa pia magunia 10 ya maharage...inaonekana sasa suala hili linataka kugeuzwa la kisiasa," alisema Bw. Makamba.

Hata hivyo alisema walichopaswa kukifanya wananchi hao, kwanza ni kumshukuru kwa msaada huo na kisha wamwambie tatizo ambalo alikiri kutokuwa na habari nalo wakati msaada huo unatolewa.

Ila alisema alishawasiliana na waliomuuzia na wakaomba mchele huo urudishwe ili wapewe mwingine, baada ya muuzaji pia kubaini kuwa ni kweli mchele huo ulikaa ghalani kwa muda mrefu hivyo kuharibika.

Naye Grace Michael anaripoti kuwa hata hivyo jana, wakazi hao wa Tabata walisema hawamlaumu Bw. Makamba kwa msaada wa vyakula ukiwamo mchele ambao ulidaiwa kuwa ni mbovu.

Mwenyekiti wa Wahanga hao, Bw. Masoud alisema: "Sisi kwa kweli kwanza tunaishukuru CCM kwa msaada mkubwa ambao iliuleta hapa ambao hata Manispaa ya Ilala ambayo imehusika kwa kiasi kikubwa kutufikisha hapa tulipo, haijaufikia msaada huo ingawa lilijitokeza suala la mchele mbovu.

"Sisi tunaamini kuwa Bw. Makamba hakuwapo wakati unapakiwa bali wapo waliofanya kitendo hicho cha kupakia mchele mbovu, hivyo ni tatizo dogo tu la kibinadamu na wala hatuwezi kumlaumu bali tunamshukuru kupitia chama chake."

Bw. Masoud kwa niaba ya waathirika wa bomoabomoa hiyo aliomba vyama vingine navyo vijitokeze kupeleka msaada katika kipindi hiki kigumu kwani wao hawabagui msaada wa mtu yeyote.

Mbali na vyama pia aliomba wasamaria wema nao wajitokeze katika kutoa misaada yao mbalimbali ili kuwaepusha na kula vyakula vya aina

SOURCE: GAZETI MAJIRA
 
Makamba bwana na CCM yake . Anaonya mambo yasiwe kisiasa lakini yeye anayafanya ya kisiasa.Unajua Mungu anawapa laana hawa CCM. Hata mchele unapelekwa mbovu ? Aliutunza wapi na kwa muda gani ? Ama ndiyo ule umesemwa uko kurasini una badilishiwa mifuko na uenezwe madukani baadaye ?
 
Habari

Ni Vizurihabari Hii Isihusishwe Na Ccm Kwa Maana Makamba Alivyoenda Pale Ameenda Kutoa Msaada Yeye Mwenyewe Sio Kama Katabu Wa Ccm Au Mtu Wowote Wa Ccm.
 
Huo nao ni UFISADI mwingine, simaanishi kuwa Makamba ni FISADI bali naamnisha huyo mfanyabiashara aliyeuza huo mchele. Inakuwaje unapakia huo mchele tena mifuko 20 bila kujua kuwa ime-expire?????? Huo ni mfano mojawapo tu wa nini kinachoendelea nchini Tanzania. Hakuna ukaguzi wa mara kwa mara kwa hawa wafanyabiashara wenye maghala. Mimi nafikiri hawa watu wote wenye maghala ya kutunza vyakula, madawa n.k waundiwe sheria ambayo itawataka kupeleka taarifa kwenye vyombo husika kuwa wameingiza nini na muda wake unakwisha lini na wamehifadhi wapi.
Naamini serikali kama ikiwa serious inaweza kufanikisha hilo na wala msituambie kuwa HAKUNA FEDHA YA UENDESHAJI. Pesa iko nyingi tu mpaka watu wanaamua kujikwapulia tu bila idhini ya wananchi.

Hatuna uhakika kama Makamba alienda kutafuta mchele wa bei chee ili tu chama chake kionekane kama kimewajali wananchi hao halafu wakacheza deal ukionyesha mchele umenunuliwa kwa bei ya juu, WHO KNOWS ingawa naamini yeye binafsi hawezi kupeleka mchele angali anajua ni mbovu. Wajiangalie wenyewe what happened...!!
 
Makamba asijifanye hajui lolote,hayo machakula mabovu yanauzwa na haohao wafadhili wakuu wa CCM ambao siku zote ndio wanaotegemea kupeperusha bendera ya CCM ili mambo yawanyooke.
Hii ni muendelezo wa kuwatumia waTZ kwa manufaa yao kisiasa huku wakiwaua taratibu kwa SUMU,mikataba mibovu na kuwavunjia makazi yao.MAKAMBA AACHE POROJO TUMECHOKA
 
Hapa Makamba amenakiliwa akimtaja Zakaria kama ndiye aliyemuuzia mchele mbovu, jee akipatiwa taarifa rasmi anaweza kumchukulia hatua kama mhalifu anayewalisha WTZ chakula kibovu?. au ndio basi lilopita limpita ataomba abadilishie na kadhia imekwisha.
 
Habari

Ni Vizurihabari Hii Isihusishwe Na Ccm Kwa Maana Makamba Alivyoenda Pale Ameenda Kutoa Msaada Yeye Mwenyewe Sio Kama Katabu Wa Ccm Au Mtu Wowote Wa Ccm.
ACHA USANII WEWE!UTAMTENGAJE MAKAMBA NA CCM KATIKA SHUGHULI ZA KIJAMII? MMEANZA KUMKANA KWA VILE MCHELE UMEGUNDULIKA KUWA MBOVU? WALE WATU WA TABATA WANGETANGAZA KUWA MCHELE ALIOLETA MAKAMBA NI MTAMU SANA INGEKUWAJE? KAULI YENU INGEKUWA "CCM NDIO # ONE KWA KUTOA CHAKULA KIZURI"
HII NI AIBU NA UNYAMA WA WAZI KUWAPA SUMU RAIA WENYE SHIDA AMBAZO CHANZO NI MAAMUZI YA SERIKALI YA CCM.
 
Habari

Ni Vizurihabari Hii Isihusishwe Na Ccm Kwa Maana Makamba Alivyoenda Pale Ameenda Kutoa Msaada Yeye Mwenyewe Sio Kama Katabu Wa Ccm Au Mtu Wowote Wa Ccm.

SHY una matatizo sana .Kwanza umekuwa ndumila kuwili kila mara unawauza wana forum kwa hadithi zako za ajabu ajabu .Kama umechukua pesa CCM na kujifanya msemaji wao hapo endelea kusema bila ya kutoa maonyo .Unafiki wako unajulikana msaliti mkubwa .Unazua story kuzima story za kuokoa maisha ya watu .Wana JF hawajakusahau japokuwa wamekaa kimya ila wanakujua uko kazini.

Makamba unawezaje kumtofautisha na CCM kwenye hili jambo ? What message did he deliver to the victims from his Chairms who is our president ? Halafu unajiita Yona Maro Mchambuzi .Uchambuzi wenyewe ndiyo huu ?
 
Mkuu Lunyungu,usipate shida sana na huyu Yona Maro Mchambuzi.
Kwani mkuu hujui kuna wachambuzi wa Pumba? alikuwepo Mchambuzi humu JF naona kaingia mitini na uzandiki wake itakuwa huyu ambaye aliyofanya bado yako ktk nyoyo zetu?
 
Makamba asijifanye hajui lolote,hayo machakula mabovu yanauzwa na haohao wafadhili wakuu wa CCM ambao siku zote ndio wanaotegemea kupeperusha bendera ya CCM ili mambo yawanyooke.
Hii ni muendelezo wa kuwatumia waTZ kwa manufaa yao kisiasa huku wakiwaua taratibu kwa SUMU,mikataba mibovu na kuwavunjia makazi yao.MAKAMBA AACHE POROJO TUMECHOKA
Kamanda, lugha yako imekaa kushoto
 
SHY una matatizo sana .Kwanza umekuwa ndumila kuwili kila mara unawauza wana forum kwa hadithi zako za ajabu ajabu .Kama umechukua pesa CCM na kujifanya msemaji wao hapo endelea kusema bila ya kutoa maonyo .Unafiki wako unajulikana msaliti mkubwa .Unazua story kuzima story za kuokoa maisha ya watu .Wana JF hawajakusahau japokuwa wamekaa kimya ila wanakujua uko kazini.

Makamba unawezaje kumtofautisha na CCM kwenye hili jambo ? What message did he deliver to the victims from his Chairms who is our president ? Halafu unajiita Yona Maro Mchambuzi .Uchambuzi wenyewe ndiyo huu ?

SAMAHANI MIMI NAANDIKA KITU KUTOKANA NA NINAVYOJISIKIA NA NINAVYOONA MIMI MWENYEWE SIMUWAKILISHI MTU AU KIKUNDI CHOCHOTE CHA WATU NAOMBA NIELEWEKE HIVYO NA WAENDELEE KUAMINI HIVYO

UNAVYOSEMA MIMI MNAFIKI NA MANENO MENGINE WACHA USEME TU UKICHOKA UTALALA NAONA UNATAFUTA ATTENTION KAMA WENGINE WANAVYOTAFUTA ATENTION

MKUU LUNYUNGU HESHIMA NI KITU CHA BURE UNAPOONGEA AU KUANDIKA CHOCHOTE KILE KWANZA ANGALIA UNACHOANDIKA KITALETA ADHARI GANI KWA JAMII HUSIKA AU WAHUSIKA WA MJADALA AU KITU HICHO

ONA MIMI NINAVYOANDIKA NA KUSEMA CHOCHOTE SILETI FITINA SILETI DHARAU WALA CHOCHOTE KILE NAONGEA MIMI KAMA MIMI NATUMIA MAJINA YANGU KAMILI

NAOMBA NIISHIE HAPA

NAFIKIRI SASA UTAFIKIA WATU TUJIUZURI KUTOKANA NA DHARAU HIZI ZA WATU NA HATA MOD WA JF SASA HIVI NAONA WAMELALA WANAACHA WATU WAANDIKE KILE WANACHOJISIKIA NA SIO KUFUATANA NA MADA AMBAYO IKO HAPO JUU

MWAFRIKA WA KIKE NILISHAMWAMBIA ILE MADA NAONA IMEFUTWA KINYEMELA PIA ASHA ABDALA NILIMWAMBIA KUHUSU KUANDIKA VITU WASIVYOKUWA NA UHAKIKA NAVYO

TUTAFIKISHANA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA NA WATU KULAZIMISHWA KUTOA MAJINA YAO HUMU NA TAARIFA ZINGINE SHERIA ITAKAPOCHUKUWA MKONDO WAKE

NAOMBA TUSIFIKE HUKO NA SIPENDI KUCHUKUWA HATUA HIZO MIMI NI MWANACHAMA HURU WA JF NA KWA BAHATI NZURI NAJUANA NA WENGI NA NATUNZA HESHIMA NA MASILAHI YAO KWAHIYO SIPENDI KUHARIBIANA MOOD NA WASIFU WENGINE

AHSANTE
 
Nimegusa tu hapa na umesema yale wengi watakuwa wanashangaa kwa nini Lunyungu kaamua kusema yote haya .Sasa nadhani umetoa Mwanga kwa kila mmoja .Mimi nasema Shy wacha kukimbia kivuli chako we know you better .Vyombo vya sheria ? Mimi Cleophas J Lunyungu ? Poa tu .Ili mradi ujue kucheza vyema maana usidhani unayajua haya mwenyewe.
 
Habari

Ni Vizurihabari Hii Isihusishwe Na Ccm Kwa Maana Makamba Alivyoenda Pale Ameenda Kutoa Msaada Yeye Mwenyewe Sio Kama Katabu Wa Ccm Au Mtu Wowote Wa Ccm.

Posting zingine zinatia kichefu chefu hata kuzisoma, Shy wewe ni Msemaji wa CCM ama Makamba? huwezi tenganisha Makamba na CCM kwenye suala hili la kuvunjiwa nyumba na mchele mbovu...madhara ya kupewa rushwa hata kufikiri kidogo huwezi mkubwa?
 
Mwelezeni huyu .Leo anatishia kwenda polisi ? Kisa kesha wajua akina Mike wanapokaa so mtawanyanyasa kwa kuwakamata na kuwatisha ?Iko siku wewe cheza.
 
Nakataa,Makamba ametoa msaada kwaniaba ya chama-na nakuu"CCM haina ghala".
Jambo lengine anadai amenunua toka kwa Zakaria,nakubali kutokubali kwani huyo nimiongoni mwa wafadhili wakuu wa CCM.
Mnakumbuka ya Idd Simba huyo pia alipata tenda ya sukari,bila kusahau ule muswada wa Zakia Meghji ulotaka walipakodi wakuu(wafanyabiashara wakubwa) kuingiza bidhaa bila kukaguliwa walikuwa wanamaanisha mtu kama huyu.Basi Wana JF mkae mkijua CCM hainunui kitu,hupewa nahao wafanyabiashara ilikuwakinga.
Bahati mbaya Muhindi kachoka anayafanya haya kwavitisho na ubabe wa CCM-lakini kawaonyesha kwamba kachoka,dalili ya mvua ni mawingu sasa CCM WANAHARIBIKIWA.
 
Asante sana Muhunzi kwa maneno yako machache lakini Elimu tosha .
 
Habari zinazovuja sasa hivi zinasema kuwa Makamba ameitwa kwenye kikao na kuuliza na wakulu wa Chama kina Rostam Azizi kuwa kwa nini anakiabisha chama. Sasa swali hapa ni kuwa, nani ana hadhi ya kumuuliza Makamba kuwa anakiabisha chama kwa kutoa chakula kibovu kwa watanzania? - Mwizi na mkoloni Rostam au yule anayeuza nchi kwa wakoloni kwa bei ya karanga?
 
kwa taarifa tu,huyu zakaria ni mhindi wa pale kitumbini na ndio wafadhili wakubwa wa ccm na huo mchele makamba hakununua alipewa bure,ndio maana hakuna hatua zozote za kisheria zilizo chukuliwa na taasisi yoyote ya kiserikali kuhusiana na mchele huo,au yeye mwenyewe makamba halichukua hatua gani baada ya kuuziwa mchele mbovu?ila nilichokisoma ni kuwa wangemwambia ili akaubadilishe huo mchele na kupewa mwingine.
Lakini wanasahau bakhresa alichomewa ngano yake baada ya kuwafadhili cuf,kule znz.
 
Makamba masikini,

mambo yanaenda south kwa kila anachogusa!

Inawezekana kabisa kuwa kuna mpango wa makusudi wa kuwalisha sumu hao waliobomolewa nyumba ili wapotee kabisa - Unadhani kuwa Makamba hakujua kuwa kuna haja ya kuchunguza hicho chakula au aliyekitoa?
 
MWAFRIKA WA KIKE NILISHAMWAMBIA ILE MADA NAONA IMEFUTWA KINYEMELA PIA ASHA ABDALA NILIMWAMBIA KUHUSU KUANDIKA VITU WASIVYOKUWA NA UHAKIKA NAVYO

TUTAFIKISHANA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA NA WATU KULAZIMISHWA KUTOA MAJINA YAO HUMU NA TAARIFA ZINGINE SHERIA ITAKAPOCHUKUWA MKONDO WAKE

NAOMBA TUSIFIKE HUKO NA SIPENDI KUCHUKUWA HATUA HIZO MIMI NI MWANACHAMA HURU WA JF NA KWA BAHATI NZURI NAJUANA NA WENGI NA NATUNZA HESHIMA NA MASILAHI YAO KWAHIYO SIPENDI KUHARIBIANA MOOD NA WASIFU WENGINE

AHSANTE

Shy,

nimesubiria muda mwingi sana uende mahakamani lakini naona kimya. Nilichosema kuwa wewe unahusishwa kwenye ile skendo ya kuwakamata wana JF bado nastand by that na sifuti statement yangu so you can go ahead and do what you want!

haya mambo ya kutisha watu umeyatoa wapi tena? bado nakuuliza swali kama ulifaidika na nini wana JF walipokamatwa?
 
Back
Top Bottom